Mmoja kati ya viongozi wa kikundi cha Ikhwanul Muslimina ajiunga na Ushia+picha
Shirika la Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya Iraq siku ya Ijumaa vimetangaza habari ya mmoja kati ya viongozi wa kikundi cha Ikhwanul Muslimana nchini Misri kuwa amejiunga na madhehebu ya ushia nchini humo.
Kwa mujibu wa habari hii (Misbahu Al Radiniy) ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa kikundi hicho cha udugu wa Kiislamu nchini Misri amejiunga na madhebu ya AhlulBayt (a.s) alipokuwa amesafiri kwenda mji mtukufu wa Karbala katika haram ya Imam Husein (a.s)
Kutokana na habari ziliosambaa Misbahu Al Radiy ambaye pia ni katika viongozi wa umoja wa maulamaa wa kiislamu duniani ambapo siku ya Jumatano alitangaza rasmi kuwa yeye ni mfuasi wa madhehebu ya Ushia Ithnashiria.
Kujiunga kwa Sheikh huyo na madhehebu ya Ushia kumfanyika mbele ya Ayatullah Sayyed Murtadha Qazwiniy ambaye ni katika wanazuoni wakubwa wa mji mtukufu wa Karbala na Imam wa sala ya jamaa katika Haram ya Imam Husein (a.s).
Mwanazuoni huyo baada ya kumaliza sala ya jamaa alibahatika kupanda katika mimbari ya Imam Husein na kuwahutubia waliohudhuria katika Haram hiyo. Kutokana na mnasaba huo Hauza ya elimu ya Karbala imefanya sherehe katika Haram ya Imam Husein.
Mwanazuoni huyo ni miungoni mwa watu waliokuwa wakishirikiana na Yusufu Qardhawiy Mufti wa Misri mwenye asili ya Qatar , pia ni kiongozi wa kiroho wa Muhammad Mursiy Rais wa zamani wa Jamhuri ya Misri.
Posted on April 11, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0