Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Afrika Kusini

24/04/2016

2509
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo jioni (Jumapili) ameonana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na huku akisisitizia udharura wa kuongezwa ushirikiano wa kila namna katika nyuga za kiuchumi na kisiasa amesema kuwa, ushirikiano wa nchi huru unapaswa kuimarishwa kwa kadiri inavyowezekana na nchi hizo inabidi zizidi kukurubiana licha ya baadhi ya madola kibeberu kufanya njama za kukwamisha jambo hilo.
Ayatullah Khamenei amesema hayo jioni ya leo Jumapili wakati alipoonana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini hapa Tehran na huku akisisitizia udharura wa kuongezwa kiwango cha ushirikiano wa kila namna katika nyuga za kiuchumi na kisiasa, ameashiria namna Tehran ilivyokata uhusiano wake mara moja na utawala wa ubaguzi wa rangi wa Makaburu wa Afrika Kusini mara baada ya kupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikata uhusiano wake na utawala wa Kizayuni wa Israel na utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini takriban kwa wakati mmoja.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbushia nafasi muhimu ya hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini katika kuanguka utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo na historia yake nzuri, ya kiudugu na kimapenzi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa, utawala huo dhalimu na ulio dhidi ya ubinadamu ulianguka kwa mapambano ya Nelson Mandela na wananchi wa Afrika Kusini, na kwamba kwa kazi yake hiyo, kwa hakika Mandela alipuliza uhai mpya katika mapambano ya bara zima la Afrika.

Amesema, mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Afrika Kusini ni mtazamo mzuri na kubainisha kuwa, uhusiano wa Iran na Afrika Kusini ni mzuri sana. Ameongeza kuwa, ushirikiano wa nchi hizo mbili katika jamii za kimataifa pia unasaidia sana. Pamoja na hayo amesema, bado uwezo wa nchi hizi mbili haujatumiwa ipasavyo kwa ajili ya kukuza mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara baina ya pande mbili.

Ayatullah Udhma Khamenei ameutaja ushirikiano wa Iran na Afrika Kusini katika Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM kuwa unaonekana kwa uwazi sana na kusisitiza kuwa: Ushirikiano huo ni kwa faida ya nchi zote wanachama wa NAM.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa, manufaa ya nchi huru yamo ndani ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika nyuga tofauti na inabidi kusimama imara kukabiliana na vizuizi vyote vinavyowekwa na baadhi ya madola ya kibeberu ili kukwamisha ushirikiano huo.

Kwa upande wake Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake kwa wananchi wa nchi yake wakati wa mapambano na ubaguzi wa rangi na kusema kuwa, wananchi wa Afrika Kusini kamwe hawawezi kusahau uungaji mkono huo wa taifa la Iran kwao.

Rais wa Afrika Kusini aidha ameunga mkono matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa, baadhi ya madola ya kibeberu yanatumia visingizio visivyokubalika kujaribu kuzuia ushirikiano na kuimarika uhusiano baina ya nchi huru lakini nchi hizo zinaweza kutatua matatizo mengi kwa kuungana na kuwa na kauli moja katika masuala ya kimataifa.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on April 25, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: