KUSHEREHEKEA MAZAZI YA AHLULBAYT BAINA YA KUMREJEA MUNGU NA MABADILIKO

KHUTBA YA SALA YA IJUMAA
MASJID ALGHADIIR KIGOGO POST DAR ES SALAAM.
13 /05/ 2016

Maulana Samahat Sheikh Hemedi Jalala khatibu na Imam wa sala ya ijumaa Masjid Alghadiir Kigogo Post Dar es Salaam amezungumzia falsafa na mafunzo kutoka kwenye mazazi ya Ahlulbayt na maimamu wa waislamu ( i.e Mazazi ya Imam Hussein, Imam Sajjad, Imam Mahdi na Abul fadhil Abbas , Ali-al-Akbar Bin Imam Hussein), ambao tarehe zao za kuzaliwa kwa mujibu wa historia ya kalenda ya kiislamu ni tarehe za mwezi mtukufu wa shaaban mwezi ambao ni wa karibu na mwezi wa ramadhani na kuelezea ya kuwa kuna funzo kubwa na falsafa inayotoa darasa kwa waumini ya kuwa Allah anawataka wamrejee na wajiandae na mwezi mtukufu wa ramadhani kupitia nyota hizi takatifu ambazo zimezaliwa ndani ya mwezi huu wa shaaban ambao ni mwezi wa maandalizi kuelekea mwezi wa ramadhani kwa kufanya maboresho na mabadiliko ya kinafsi na kijamii. Katika kuelezea hilo alisemaIMG_20160513_125353.jpg

“Kuzaliwa nyota hizi tukufu za watu wa nyumba ya mtume katika mwezi huu wa shaaban, mwezi wa karibu na wa maandalizi kuelekea mwezi mtukufu wa ramadhani ni ishara ya kuwa Allah anatutaka turudi kwa Ahlulbayt (a.s) ambao ndio watu waliofunza dunia mabadiliko ya Nyanja zote za kidini na kijamii ili tuweze kuboresha hali zetu na kufanya maandalizi ya lazima na ya msingi ya kutuandaa kuelekea mwezi wa ramadhani, mwezi wa kufanya mabadiliko binafsi ya kinafsi, kidini na kijamii”.

Maulana Sheikh Hemedi Jalala aliendelea kusema kuwa Ahlulbayt chini ya kiongozi wao Mtume Muhammad (sa.w.w), mtume ambae hajawahi kukosea wala kumuasi mungu, wao ndio walimu wa mwanzo waliofunza mabadiliko, walifunza mabadiliko katika Nyanja zote za kimaadili na ndio maana mtume mwenyewe anasema ametumwa kuja kukamilisha tabia njema. Watu wakisoma watashuhudia mabadiliko ya kitabia ambayo mtume na Ahlulbayt walikua vinara na walimu wa mwanzo wa kutenda mabadiliko hayo, lau kama mtu atafungua jicho atampata mtume jinsi alivyoilea jamii na kuifunza thamani ya binadamu na hasa mtoto wa kike ambae alikua akizikwa hali yuko hai. Upole wa Imam Hassan, ukarimu wa Imam Ali, ushujaa na uaminifu wa Abulfadhil Abbas ni mafunzo tosha ambayo jamii inapaswa kujifunza na kuyatumia katika kubadilisha mambo yao mabaya na kuyaboresha. Maulana Alisema :

“Itazame dunia ya sasa ilivyo inahaja ya mabadiliko makubwa ya kitabia, leo hii biashara ambazo kamwe zilikua haziwezekani kufanyika hadharani zinafanywa kwa matangazo, jamii ya sasa imefikia wakati ambao yanafanywa mambo machafu baina ya wanaume kwa wanaume hadharani, la kusikitisha ni kwamba unawapata wahusika mara nyingine ni viongozi wa kidini, Jamii hii inahitaji kuwasoma Ahlulbayt a.s na kujifunza jinsi ya kurekebisha tabia zao na kuboresha hali ya jamii zao”

Maulana aliendelea kusema na kuzungumzia kuhusu swala la kuilea jamii, hasa jamii ya maskini, mayatima wajane na waliokatikiwa safarini na kusema:

“Misikiti ya sasa iko wapi na kuilea jamii na kutatua shida za wanaohitajia, Ukimsoma mtume ambae maisha yake ni darasa juu ya mabadiliko utapata msikiti wake ulikua na sehemu maalumu ya kuwaweka maskini na mayatima ili atatue shida zao, ndio maana ukimsoma Zahraa alipokua akimlilia baba yake alikua akisema “Nani atawaangalia mayatima, maskini na waliokatikiwa katika safari (ibnu sabil)” ”

Mwisho Maulana Sheikh Hemedi Jalala wito kwa jamii ya kiislamu kuwasoma Ahlulbayt na kuhamisha maisha yao na tabia zao nzuri kwenda kwenye jamii ili kuufunza uislamu halisi wa mtume kwani katika zama za sasa kuna watu wanaotumia jina la uislamu kuuwa na kuchafua dini. Maulana aliendelea kusema kuwa jamii ya kiislamu inapaswa kujipamba na upole, ukarimu na kuhudumia jamii kama vile ambavyo Ahlulbayt walikua wakifanya.

Katika kumalizia Maulana Sheikh Hemedi Jalala kama kiongozi mkuu wa Hawzat Imam Swadiq na Imam wa Masjid Alghadiir alitoa pongezi kwa uongozi wa wa Hawza kwa kufanya sherehe za Miiraj kwa kutembelea wajane na maskini pamoja na kuwasaidia, jambo hili ni la kuigwa kwani ni moja ya njia muhimu ya kumuiga mtume wa uislam.

Imehaririwa na
Kitengo cha Habari Hawzat Imam Swadi (a.s), AsadiqMedia.
S.L.P 67002, Dar es Salaam.
Email: asadiqmedia@gmail.com.
Website: imamswadiq.com/

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on May 13, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: