NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KIPINDI CHA GHAIBA YA IMAM
MAULANA SHEIKH HEMEDI JALALA AMEHUDHURIA HAFLA YA KUTUNUKU ZAWADI WASHIRIKI WA MASHINDANO YA UANDISHI.
Maulana Samahat Sheikh Hemedi Jalala Mudir wa Hawza Imam Swadiq (a.s) amehudhuria hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mehfil Abbas kwaajili ya kutunuku zawadi kwa wa shindig wa shindano la uandishi wa Insha inayohusiana na Bibi Fatima a.s na kuzungumza na mamia ya waliohudhuria kuhusiana na Imam wa wa zama, Imam Mahdi a.s ambapo alizungumzia NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KIPINDI CHA GHAIBA YA IMAM.
Maulana akiongea na wanawake ambao ndio asilimia kubwa ya waliohudhuria alisema:
Wafuasi wa dini nyingi wanaamini juu ya ujio wa mkombozi kabla ya mwisho wa dunia, sii waislamu pekee bali hata Budha, Wahindu, wakristo na mayahudi, kwa itikadi yetu sisi waislamu tunamsubiri mtu anaeitwa Mahdi ambae swala la kudhihiri kwake limekubaliwa na maulamaa wa pande zote baina ya Ahlusunna na Shia japokuwa kuna uwepo wa tofauti juu ya kuwa amezaliwa au la, Muhimu ni kwamba dunia haitoisha mpaka ifikie dini hii ya uislamu kuwa ni dini inayoongoza na watu wake ndio viongozi katika nyanja zote, Kudhihiri kwa Imam Alhujja Almadiy kutaifanya dunia iwe ni mahala pa maelewano masikilizano na Amani. Kwa akina mama ndio walezi wa watoto na akina baba pia napenda nizungumzie wadhifa wao na majukumu yao katika kipindi hichi cha Ghaiba.
Maulana Samahat Sheikh Hemedi Jalala alizungumzia kuwa miongoni mwa majukumu ya wanawake wakiislamu na khususan wafuasi wa Ahlulbayt a.s kama ifuatavyo:
KUMTAMBUA IMAM KWA HAKI YA KUMTAMBUA
Wanawake kwa nafasi yao kama walezi wana wajibu na wadhifa wa kumtambua Imam vizuri, Imam anatusuburi tuwe tayari, Anatusubiri tutengeneze jeshi kwaajili ya kudhihiri kwake, ni jukumu la wanawake kumtambua imam kwani wao ndio walezi na walimu wa mwanzo kwa watoto. Lazima waumini na hasa wanawake wajitahidi na wahakikishe maarifa yao juu ya imam wa zama ni makubwa, wanaitambua falsafa ya ghaiba ya imam na nini kazi yake atakapodhihiri ili wasaidie kutengeneza jeshi la Imam huku wakitimiza majukumu yao kipindi chote cha ghaiba. Ukisoma moja ya dua za Ahlulbayt a.s utapata kuna dua inayosema “Ewe Mungu nitambulishe hakika yako kwani usiponitambulisha hakika yako sitomtambua mtume wako, Ewe mungu nitambulishe mtume wako kwani nisipomtambua mtume wako sitomtambu kiongozi na hujja wako, Ewe Allah nitambulishe Hujja wako kwani nisipomtambua kiongozi na hujja wako nitapotea katika dini yangu
Hivyo jukumu kubwa na la mwanzo kabisa ni Maarifa juu ya Imam wa zama, Imam Alhujja Almuntadhar.
KUWAELEA WATOTO KATIKA KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA IMAM WA ZAMA.
Wazazi wanawajibu wa kuhakikisha wanawatengenezea watoto wao mahusiano mazuri na imam wa zamakwa kuwafunza dua muhimu za kusomwa kila siku za asubuhi sambamba na kutoa kiapo cha utii kwa kusoma Dua Al ahad kila baada ya swala ya asubuhi. Kila mahusiano yao na imam yatakapozidi kuwa makubwa basi wataweza kuwa mbali na tabia mbaya pamoja na madhambi na pia hii itakua njia nzuri ya kuwatengeneza kuja kuwa miongoni mwa wafuasi na wanajeshi wa imam.
KUWAFUNZA WATOTO UVUMILIVU JUU YA ITIKADI ZA WENGINE
Akina mama kwa jukumu lao la walezi wanawadhifa wa kufunza uvumilivu wa kiitikadi kwa watoto wao dhidi ya itikadi na Imani za dini nyingine ili kuwezesha hali ya Amani na maelewano kufikiwa katika jamii.
Pamoja na hivyo Maulana aliendelea na kusema watoto wanatakiwa kupewa malezi na kufunzwa subra hasa katika hiki kipindi cha maendeleo makubwa ya teknolojia ambayo yanachangia kiasi kikubwa katika kuharibu maadili ya watoto. Jamii ya sasa inahitaji malezi katika kila Nyanja hasa ukizingatia kuna uwelewa mbaya wa mafunzo ya kidini na kiitikadi na imepelekea hata watu kuchinjwa na wanaodaiwa kuwa ni waislamu baada ya sala.
Mwisho Maulana alipongeza juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali na kukabidhi zawadi kwa washiriki wa mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na Mahdi center Dar es Salaam.
Imehaririwa na Asadiqmedia, kitengo cha habari Hawza Imam Swadiq (a.s)
Posted on June 6, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0