KHUTBA YA IJUMAA MASJID ALGHADIIR

KHUTBA YA SALA YA IJUMAA YA KWANZA YA MWEZI WA RAMADHANI 1437/2016

Khatibu wa sala ya ijumaa Msikiti wa Alghadir Kigogo Post Dar es Salaam Maulana Sheikh Hemedi Jalala amezungumzia Umuhimu wa dua na swala zima la kumlilia na kumuomba mwenyezimungu hususan katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani. Katika kuelezea fadhila za mwezi mtukufu wa ramadhani na faida zake kwa waumini Maulana Sheikh Jalala amefasiri maneno ya DSC00198mtume ambayo yaelezea umuhimu wa dua yanayosema “na inueni mikono yenu kumuomba mola wenu kwani dua zenu(ndani ya mwezi huu wa ramadhani) zinajibiwa na matendo yenu yanakubaliwa ”.

Maulana Sheikh Hemedi Jalala akizungumza na mamia ya waumini waliohudhuria sala ya ijumaa msikiti wa Ghadir ulioko Dar es Salaam Kigogo Post Tanzania amesema “Mwezi huu mtukufu wa ramadhani ni mwezi ambao dua zinajibiwa hivyo ni wakati rasmi wa kumuelekea Mwenyezimungu mtukufu kwani mafunzo ya mtukufu mtume yanatufunza ya kwamba dua ni silaha ya muumini. Kwa hakika kila ambae anaemtegemea Mwenyezimungu na kumuomba yeye pekee hakuna kinachoweza kusimama dhidi yake.”

Maulana aliendelea kuelezea umuhimu wa dua kwa kunukuu kisa cha Imam wa sita wa waislamu, Imam Jaafar Swadiq (a.s) alipoitwa na mfalme huku mfalme akiwa anania ya kumuua, Imam aliingia katika jumba la mfalme huku midomo yake ikionekana kutikisika (akiwa anaongea polepole). Mfalme alikua ameshaweka mtu maalumu wa kumuua imam pindi atakapoingia lakini ajabu mfalme alishuka kutoka kiti chake na kumpokea kwa heshima….Baada ya muda imam akaondoka, maswahaba zake wakamuuliza ulikua ukisema nini ulipoingia mbele za mfalme maana tuona midomo yako ikicheza kama mtu anaesema kitu, Imam akawajibu ya kwamba nilikua ninasoma dua, nilikua ninamuongelesha mola wangu, Leo mfalme alikua amedhamiria kuniua lakini kwa Baraka na nguvu za dua haikuwezekana. Mfalme upande wake alipoulizwa ni kwanini hakutekeleza dhamira yake alijibu na kusema alipojia mbele zangu abuu Abdillah alikuja na sura yenye heshima kubwa, utukufu na haiba hivyo nikashindwa kumuua. Yote haya yanaonyesha umuhimu na uzito wa dua.DSC00201

Sambamba na hivyo Khatibu wa sala ya ijumaa ambae pia ni Kiongpzi mkuu wa chuo cha theolojia ya dini ya kiislamu cha Imam Swadiq (a.s) aliendelea kubainisha ya kuwa waumini wanaruhusiwa kuomba kwa lugha yeyote sii lazima kiarabu na kwamba kuomba na kumuelekea Mungu ni kipimo cha utii, unyenyekevu na Imani. Maulana alisema “Kushikamana na dua kuna faida nyingi lakinini kubwa ni kubadilisha hali mbaya za watu, hivyo waislamu na waumini wote wanapaswa kuyakumbuka makundi maalumu katika dua zao”.

Maulana Sheikh Hemedi Jalala aliendelea kusema “Jamii yetu ina watu mbalimbali wnye matatizo, wengine ni wagonjwa na wengine ni mayatima, maskini, mafakiri wajane na wanaoishi bila ndoa, Haya ni makundi ambayo yanahitaji huruma na kuombewa ili hali zao ziboreke pamoja na hivyo tusiwasahau wenzetu waliotangulia mbele ya haki. Mwezi wa ramadhani ni fursa muhimu ya kuomba umoja baina ya waislamu ufikiwe kwani mizozo ndani ya umma wa kiislamu inatudhoofiha na kumaliza nguvu zetu. Ni muhimu kukubali tofauti zetu na kusubiri na kuvumiliana kwani haitokaa ikawezekana Tanzania nzima masuni wote wakabadilika kuwa mashia,wala mashia kubadilika wote kuwa answaru sunna au watu wa Twariqa. Muhimu ni kuishi huku tukiamini ya kwamba kutofautiana ni asili ya kimaumbile. ”

Maulana Sheikh Hemedi Jalala aliendelea kuzungumzia umuhimu wa dua huku akitoa wito kwa watanzania wote khususan waislamu ambao wako katika mfungo wa ramadhani kutumia fursa ya kujibiwa dua zao katika mwezi huu kuomba umoja wa kitaifa na umoja wa watanzania ubaki salama kwani kupitia hili tunaweza kuifanya Tanzania kubaki kuwa ni kisiwa cha Amani.

Maulana Sheikh Jalala aliendelea kusema : ”Ndugu zangu watanzania, waislamu na wasikuwa waislamu umefika wakati wa kutumia kila fursa kuomba utulivu na Amani ya nchi yetu, katika mazungumzo yangu nimewahi kukemea na kulaani matukio mabaya ya kikatili yaliyotokea Katika mapango ya Amboni na tukio la Mwanza, Katika nchi yetu hatukuwahi kusikia mtu anachinjwa hivyo tutumie mwezi huu kumuomba Mungu matukio kama hayo yatokomee kabisa katika nchi yetu”.
Mwisho Maulana Sheikh Hemedi Jalala ametoa wito na ujumbe kwa vijana ya kwamba wasiwe watu wa mwanzo wanaoweza kutumika katika uvunjifu wa Amani na kuwasihi wamrejee mola wao na wamuombe kwani hakuna ibada kubwa kama kumuomba mungu na kumnyenyekea.

Imehaririwa na Asadiq Media,
kitengo cha Habari na mawasiliano Hawza Imam Swadiq (a.s)
B.pepe: asadiqmedia@gmail.com
Web: imamswadiq.com/

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on June 10, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: