MANENO YA BUSARA KUTOKA KWA IMAM HASSAN (SA)

3_b

21/06/2016

Imam Hassan (a.s) anasema: Enyi watu, yule ambaye anashauri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na akayachukulia maneno yake kuwa mwongozo hakika Allah (sw) atamuongoza katika njia ya haki, atamlipa mafanikio kwa uongozi sahihi na atamuongoza katika yalio mema. Kwa hakika Watumishi wa Mwenyezi Mungu ni wamehifadhiwa huku adui yake yupo katika waoga na kukata tamaa.

Kuwa na hadhari ya Mwenyezi Mungu kwa kumtaja yeye sana, na Muogope yeye kwa njia ya Uchamungu, na jikurubishe kwake kwa mbinu na njia ya utii, kwa hakika yeye yu karibu na mwenye kujibu maombi.

Mwenyezi mungu mtukufu anasema: “Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka” (Qur’an, 2: 186)

Muitikieni Mola wenu na kumuamini kwa sababu ni makosa makubwa kwa mtu yeyote ambaye anautambua utukufu wa Mwenyezi Mungu kisha akafanya kiburi. Utakatifu wa wale ambao wanatambua ukubwa wa Mwenyezi Mungu upo katika kumtii yeye, Heshima ya wale ambao wanakiri utukufu wa Mwenyezi Mungu ni kujidhalilisha kwake, na usalama wa wale ambao wanatambua nguvu ya Mwenyezi Mungu ni katika kuridhia maamuzi yake na kuepuka kumkana baada ya kukiri Imani na kujitenga na upotofu baada kupata mwongozo.

Hakika unapaswa kujua ya kwamba huwezi kutambua Uchamungu kabla hujatambua sifa za Muongozo, huwezi kukamatana na Kitabu (Quraan) kabla ya kujua wale ambao wamejitenga nacho, na huwezi kusoma Kitabu (Quraan) vizuri kabla ya kujua wale ambao wameipotosha.

Baada ya kujua haya yote, utajua uzushi (Bidaa) na Misimamo mikali, utaona walivyoghushi dhidi ya Mwenyezi Mungu na upotofu, na utawajua jinsi gani walidhalilika wale walionguka. Hebu usikubali wajinga kukushirikisha katika ujinga wao.

Yatafute haya kutoka kwa watu walio sahihi, kwa maana wao ni mwanga ambao elimu hutafutwa na ni viongozi ambao mifano yao lazima kufuatwa. Kupitia wao, maarifa yalisalia na ujinga ulififia mbali. Usamehevu wao huashiria kutokujua kwao, Matamshi yao ya hekima huashiria ukimya wao, na muonekano wao huashiria kujificha kwao.

Hawapingi haki wala hawapo kinyume nayo. Mila tofauti zilikuwepo kabla yao na uamuzi wa Mwenyezi Mungu ukapita kabla yao. Hili kwa hakika ni mawaidha kwa wale ambao watakumbuka. Wakati utasikia unapaswa kuelewa, si tu kwa uhusiano. Wasimuliaji kwa hakika wapo wengi wakati wenye kuzingatia ni wachache. Allah ni Mmoja aombwaye msaada.

MAONYO YAKE:
Unapaswa kujua kwamba Allah (sw) hakukuumba wewe bure na hatokuacha upite bure bure. Amekuwekea kikomo cha Mauti yako na kukupangia Maisha yako ili kila mwenye akili atambue wadhifa wake na kutambua kwamba chochote ambacho Mwenyezi Mungu amekuruzuku kitakuponyoka bila kizuizi na chochote kitokacho kwake hakimpunguzii chochote.

Allah amekuokoa na mbio za kutafuta riziki ya ulimwengu huu, amekupa muda wa kutosha kumuabudu yeye, na akakutaka umshukuru, na akakuamrisha kumtaja yeye, akakuasa kumuogopa yeye, na akafanya suala la Kumcha yeye ndio kusudi kuu la kuridhika kwake.

Hakika, Uchamungu ni mlango wa toba zote, kichwa cha hekima zote, na heshima ya hatua zote. Uchamungu ni njia ambayo ushindi na mafanikio hufikiwa.

“Mwenyezi Mungu anasema: Hakika wachamungu wanastahiki Ushindi” (Qur’an 78:31)

Na Mwenyezi Mungu atawaokoa walio wacha Mungu kwa sababu ya vitendo vyao wema.. Hapana ugumu utakaowagusa, wala hawatahuzunika (Qur’an 39:61).

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu mcheni Mwenyezi Mungu na kujua kwamba yeyote anaye mcha Mwenyezi Mungu ataepushwa na mambo ya uchochezi na Mwenyezi Mungu atamuongoza katika mambo yake, na kumuandaa kwa kwa ajili ya muongozo wake, atamuunga mkono kwa hoja, na kuung’arisha uso wake, na kutimiza matumaini yake yote pamoja na wale ambao hupokea fadhila za Mwenyezi Mungu, kama vile manabii, mashahidi na Watu wema. Wao ni marafiki bora mtu anaweza kuwa nao.

Chanzo: Tuhaf al-Uqool

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on June 21, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: