MAZAZI NA UTOTO WA IMAM HASSAN (S.A)
03/06/2016 | |
Uongozi wa chuo cha dini cha Imam Swadiq (as) kilichopo kigogo polisi post, Dar es Salaam chini ya kiongozi wake wa kiroho Mawlana Sheikh Hemedi Jalala tunatoa mkono wa Heri na Pongezi kwa Mtoto pekee wa mtume Bi fatma Zahraa kwa kuzaliwa mwanae wa Kwanza Imam Hassan Mujtaba. Salamu za pongezi zimwendee Mtume (saww), Imam wa Zama Mahd (A.T.F.S) na Kiongozi wa Waislamu Ayatollah Sayyid Ali khamenei na Marajii wote duniani. Heri na fanaka ziwafikie waislamu wote na wapenda Amani duniani kote. Hongera kwa kuzaliwa Imam Hassan Mujtab (s.a)Jina: Hasan (s.a) – Imam Mtoharifu wa pili (2)Hadhi/Wasifu wake: al-Mujtaba
Baba yake: Imamu Ali Imamu (a.s) Imam Mtoharifu wa kwanza (1) Mama yake: Bibi Fatima Zahra (a.s) binti pekee wa Mtume Mohammad (saww) Kuzaliwa: Madina siku ya 15 ya Ramzan Mwaka wa 3 Hijiria sawa na (624 A.D) Kifo: Madina akiwa na umri 47, Tarehe 28 Safar 50 Hijiria sawa na (670 A.D) Sababu ya Kifo/Mazishi: Alikufa shahidi kwa kutegeshewa Sumu na kuzikwa katika makaburi ya Baqi huko Madina. Majina yake mengine: al-Sibt, al-Sayyid, al-Zaki, al-Mujtaba, al-Taqi. Kuzaliwa kwake: Katikati ya Mwezi wa Ramadhani, Mwaka wa Tatu (3) ya Hijrah, Mtoto alizaliwa katika nyumba ndogo ya matope ya Imam Ali (A.S). Mtume Muhammad (amani iwe juu yake na familia yake), kwa niaba ya Mwenyezi Mungu alimpa jina lake kuwa Hassan. Imam Hassan (s.a) alilelewa mapajani mwa baba yake Imam Ali (s.a) na Mama yake Fatima Zahra (S.A) na kujifunza masomo kutoka shule ya babu yake Mtume Muhammad (saww). Imam Hassan (s.a) alikuwa na thamani kubwa na hadhi mbele ya macho ya Mtume Muhammad (saww). Kama vile, siku moja Mtume Muhammad (saww) alikuwa juu ya Mimbari, akitoa hotuba kwa watu, akasikia sauti yake akilia. Akashuka Mtume kutoka katika Mimbari, akaenda kumbembeleza, na kisha akarudi kuendelea na Mawaidha. Wakati watu walipomuuliza sababu ya tendo hilo. Yeye (saww) akasema kila kisikiapo sauti yake akilia mimi hukosa utulivu”. Mtume Muhammad (saww), alikuwa anapomaliza kuswali jamaa pamoja na watu, humuinua Imam hassan (s.a) na kumueka katika Mapaja yake na kusema, “Yeyote anayenipenda, lazima ampende mtoto huyu pia”. Wakati mwingine, Mtume (saww) alikuwa akimbeba mtoto huyu begani kwake na kusema, “ni matumaini kuwa Mwenyezi Mungu atautakasa umma kupitia yeye”. Au yeye (saww) alikuwa akisema, “Kila anayependa Hassan (as) na Hussain (as) ananipenda mimi na mtu mwenye kuweka chuki na ana uadui dhidi yao pia ana uadui na mimi “….”Hassan (as) na Hussain (as) ni Mabwana wawili wa vijana wa peponi” Kisha Mtume Muhammad (amani iwe juu yake na familia yake) alisema, “Hassan (as) na Hussain (as) ni pete mbili za Arshi, pepo ya Mungu Inajivuna na kujifakharisha kutokana na wao”. Imetafsiriwa na Abuuzahraa |
Posted on June 21, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0