NI IPI FALSAFA YA KUTOA ZAKKA ?

RUMUS TEPAT CARA MENGHITUNG ZAKAT FITRAH

Ni ipi falsafa ya kutoa zakka ?

Ni dhahiri kuna sababu tatu zenye umuhimu kuhusiana na kuwa na hazina ya Fedha za umma na kutoa Zakat (ambayo ni moja ya chanzo ya mapato yake), Kwanza, Uislamu haukuja kama mafundisho ya kimaadili, falsafa au kiteolojia pekee yake bali pia uislamu ulikuja kama dini kamili inayogusa Nyanja zote za Mwanaadabu iwe  kimaada, na Kimaanawi (kiroho). Pili, Uislamu, kutoka mwanzo wake wakati wa Mtume Mtukufu (s.a.w), alikuwa daima ukihusiana na uanzishwaji wa serikali, na Tatu, uislamu unatoa kipaumbele maalum katika kusaidia wasiojiweza na kupambana na tofauti ya matabaka katika jamii.

Bila shaka yoyote, kila jamii ina sehemu yake ya watu ambao wasiojiweza, wagonjwa, walemavu, yatima wasio na walezi na kama watu wengine nao wote wanahitaji kutunzwa na kuangaliwa.

Aidha, ili kulinda jamii kutokana maadui wenye nia mbaya pia ipo haja ya kuwa na jeshi kwa ulinzi wa Nchi na Mipaka, Jeshi ambalo gharama za kuliendesha hugharimiwa na serikali. Vivyo hivyo, pia kuna haja kuwa na mfuko wa hazina uliotegwa kwa  kwa ajili ya Mishahara na Stahiki za wafanyakazi wa serikali ya Kiislamu, kama vile mahakimu, Waalimu, kuendesha vituo vya kidini, Sule na Vyuo vikuu, Vyombo vya Habari na matangazo na vifaa vya uhabarishaji, ambavyo vyote haviwezi kupangwa na kusimamiwa bila uhakika na nidhamu ya kifedha.

Kwa sababu hizi, suala la Zakat, ambalo katika hali halisi ni aina ya ‘kodi ya mapato na uzalishaji’ na ‘kodi ya mali iliyotuama’, linapewa kipaumbele mkubwa katika Uislamu, kwa kiasi kwamba huwekwa katika daraja sawa sawa na vitendo muhimu zaidi vya ibada, kwenye nyakati tofauti tofauti Zakat imekuwa ikitajwa pamoja na swala na hata imefanywa kuwa sharti la kukubalika kwa swala!

Katika hadith, iliyopokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) inasema: “Yeyote yule, anayezuia  Zakat hata yenye uzito wa ratili (Carat) moja, Mtu huyo sio Mu’min wala Muislamu na hana heshima wala thamani!”

Cha kufurahisha zaidi, tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa mpangilio huu mzuri wa utozaji wa zaka uliowekwa na uislamu na vipimo vyake vilivyoainishwa, laiti kila Muislamu angelitoa zaka yake kama ilivyo agizwa, pasingelikuwepo katika jamii ya waislamu mtu yeyote Maskini mwenye kuhitajia msaada.

Imamu Sadiq (A.Ş) anasema: Kama watu wote wangalitoa Zaka ya mali zao, hakuna Muislamu angebakia masikini na mwenye kuhitaji msaada. Watu hawawi masikini, mafukara, wenye njaa isipokuwa ni kutokana na Ubahili wa walio na ukwasi!

Kutokana na riwaya hizi inaweza kuonekana wazi kuwa lengo la kutoa zakat ni sababu tosha ya ulinzi wa Mali na uimarishaji wa msingi yake, Kiasi kwamba pindi watu watakapoghafilika wakapuuza kanuni hii muhimu ya Kiislamu, Mipasuko na mifarakano huibuka miongoni mwa jamii kiasi kwamba hata mali ya tajiri asiye na hatia itaingia katika hatari.

Imesimuliwa kwamba Imam Musa b. Ja’far (A.Ş) alisema: “Linda mali yako kwa njia ya zaka.”

Maana hiyo hapo juu pia imesimuliwa katika riwaya zingine zilizo ripotiwa kutoka Mtume Mtukufu (s.a.w) na Amiril muumina (A.S)

Na Sheikh Naser Makarem Shirazi

Imetafsriwa: AbuuJawad

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on July 4, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: