FALSAFA YA IDDI AL-FITRI NI IPI?
Eid ni neno la Kiarabu lililotokana na neno mizizi ya-w-d. Kilugha lina maana tukio linalotokea mara kwa mara. Katika Uislamu inaashiria sherehe ya Uislamu. neno Iddi limetokea katika Qur’an mara moja likimaanisha tukio furaha linalojirudi rudia
Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku (5:114) Eid-ul-Fitr (Id al-Fitr) huunganishwa na mwezi Mtukufu wa Ramadhan. huashiria mwisho wa mwezi wa mfungo wa Ramadhan (siku ya kwanza ya mwezi wa Shawal). Eid-ul-Fitr ni sikukuu ya kipekee haina uhusiano wowote na tukio lolote la kihistoria wala haihusiani na mabadiliko ya majira au mzunguko wa msimu wa kilimo. Sio Sikukuu inayohusiana kwa njia yoyote na mambo ya kidunia.-Fitr (Id al-Fitr) huunganishwa na mwezi Mtukufu wa Ramadhan. huashiria mwisho wa mwezi wa mfungo wa Ramadhan (siku ya kwanza ya mwezi wa Shawal). Umuhimu wake ni wa kiroho zaidi. Ni siku ambayo Waislamu humshukuru Mola wao kwa kuwapa mapenzi, nguvu na uvumilivu wa kutekeleza Ibada ya Swaumu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Siku hii, katika ulimwengu wa Kiislamu, huleta shangwe na furaha. Furaha sio, kwa sababu tu ya kuondoka kwa Mwezi wa Ramadhani; ni furaha ambayo mtu anahisi baada ya mafanikio ya kumaliza kazi muhimu. Ni sherehe kwa kwa baadhi ya maeneo husherehekewa kwa likizo ya siku tatu inayoitwa Eid-ul-Fitr (Sikukuu ya Kufungua swaumu). Watu hubadilishana zawadi. Marafiki na familia hukusanyika na kuswali swala za Jamaa. Sikukuu ya Iddi Fitr ni malipo ya Mwenyezi Mungu kwa wale ambao walifunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Katika mwezi huu, mtu anapaswa kujaribu kuongeza maarifa yake ya kumjua Mwenyezi Mungu, kufanya vitendo vya ukarimu kwa masikini, Kuhuisha upya imani yake kuelekea Mola wake nah ii ndio itakuwa maana halisi ya Sikukuu. Maombi ya siku ya hii iwe ni sababu ya umoja na mshikamano wa Waislamu duniani kote. Katika siku hii atukuzwe Mwenyezi Mungu kwa huruma yake isiyo na mwisho. Dhana ya Siku ya Eid katika Uislamu haihusiani tu na sherehe za ubadhirifu, sikukuu za anasa, na kupeana mikono na marafiki. Bali Waislamu wanapaswa badala yake kujishughulisha na Ibada ya Mwenyezi Mungu na kumuomba akubali kupitisha matendo yao mema na kusamehe dhambi zao. Hii ni kwa sababu milango ya msamaha wa Mungu huwachwa wazi siku hii na Baraka zake na ukarimu. |
Posted on July 5, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0