Usiku wa cheo “Laylat Al-Qader” 

Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema mwenye kurehemu

Usiku wa nguvu au kama inavyojulikana “Laylat Al-Qader” ni usiku wenye fadhila na utukufu, ambao Mwenyezi mungu ameuruzuku waja wake na hususan ummah huu, ni moja ya usiku mtukufu sana na malaika hushuka na kuwazunguka waumini wote na kuwapa Amani, baraka na zawadi; zaidi ya hayo ni usiku ambao matendo mema mazuri hulipwa zaidi ndani yake na hakuna usiku ambao ni bora zaidi kuliko usiku huu, na kufanya ibada katika usiku huu ni bora kuliko miezi elfu moja.

Mbali na hilo, ni usiku wa huruma na unyenyekevu, na katika usiku huu, ndipo Quran tukufu ilishushwa, ikibeba kanuni za mambo mema na muongozo wa kufuzu ubinadamu, na ufunuo wa baraka. Aidha, katika usiku huu, Mungu huamua mambo ya watu, na malaika hushuka na Jibril ndani yake.

Imesimuliwa katika Majmaee Al-Bayan kutoka kwa Ibn Abbas (sa) anasema:

“Katika usiku huu wa nguvu (Laylatul Qadr), Malaika walio katika Sidrat al-Muntaha hushuka, na baadaye Malaika Jibril hushuka pia akiwa ameshika mabango, bango moja huliweka katika kaburi langu na jingine juu ya mji wa Yerusalemu na jingine katika “Msikiti mtakatifu” (Al-Masjid al-Haram) na moja katika mlima Tur Sinai na kisha huwasalimia waumini wote isipokuwa wale ambao ni walevi na hula nyama ya nguruwe na wale ambao wametiwa madoa na Saffron.” 

Na imesimuliwa kutoka kwa Mtume Muhammad (Amani iwe juu yake na familia yake) akisema: “Yeyote anayekesha usiku wa laylatul Qader atasamehewa Madhambi yake yote”. kisha akaongeza kusema katika usiku huu Shetani hawezi kumtawala yeyote na hawezi kumfanya mtu afanye uovu na hakuna mchawi anaweza kupenya.

usiku huu una hadhi kubwa na daraja ya juu na hii linaweza kujulikana kwa namna malipo na thawabu za matendo mema huongezeka kwa kila tendo lifanywalo, ndio sababu Mtume Muhammad (Amani iwe juu yake na familia yake) akasimulia mazungumzo yaliotokea kati ya Mussa ( AS) na Mwenyezi Mungu katika mazungumzo hayo Nabii Mussa (sa) aliomba kwa kusema: “Mola wangu, nataka kuwa karibu na wewe, Mwenyezi Mungu alijibu… Mussa, aliyekaribu na mimi ni yule ambaye anakesha katika usiku wa Laylatul Qadri, Mussa akaomba tena; nataka huruma yako, Mungu alijibu… Nitawasamehe wale  ambao watakuwa na huruma kwa Maskini, akasema tena, Mola wangu, nataka kuwa katika njia ya haki, akamjibu akisema yule mmoja wenu anayetoa sadaka kwa watu maskini katika usiku wa Laylatul Qadr atakuwa katika njia ya Haki Kisha nabii Mussa akaongeza kuuliza… Mola wangu, nataka unioteshee mti katika pepo yako tukufu, akajibiwa: Atakayenitaja na kunisifu katika usiku wa nguvu ataoteshewa Mti katika pepo, akaongeza kuomba akisema, Mola wangu nataka radhi zako, Mwenyezi Mungu akamjibu: Radhi zangu zitamfikia yule atakayeswali rakaa mbili katika usiku wa nguvu (Laylatul Qadr)”

Ni vema kufahamu kuwa ni katika usiku huu mkubwa na Mtukufu, tukio kubwa lilitokea ambapo Amiri wa Waumini Imamu Ali (A.S.) aliuawa Shahidi tukio hilo ni tetemeko lililotikisa Msingi wa Muongozo. Imamu Ali Khamenei kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran akimzungumzia Imam Ali (SA) anatutaka kufarijika na kujifunza kutokana na tukio hilo akisema: “Basi na tumfanye Ali ibn Abii Talib (A.S) kuwa kiigizo chetu bora katika kila kitu tunachokifanya, na tunapaswa kufanya kazi nzuri ya kuwa kama yeye, kisha akauliza “Hivi tunadhani kwamba sisi ni Mashia na Ali (AS) ni Imamu wetu wakati hatujishughulishi sana  na uhusiano wetu na Mola wetu?

Akaendelea kueleza kuwa … “Imamu Ali (AS) alijitolea maisha yake yote katika kumuabudu Mwenyezi Mungu, ambapo kutoka awamu ya kwanza ya uongozi wa Imamu Ali kupitia kwa Mtume Muhammad (Amani iwe juu yake na familia yake) mpaka siku aliyopata shahada ya kifo chake hakuwahi kuzembea kumuabudu mola wake na kumsifu yeye pekee;

Imam Ali (AS) alidumisha uhusiano wake na Mola wake katika hali zote, iwe katika furaha au katika huzuni, katika vita au amani, wakati wa usiku na wakati wa mchana, awapo msikitini na katika uwanja wa vita, katika kipindi cha tawala na katika kipindi cha hukumu … Baadhi watu hujidai kuwa Imamu Abuuzahraa:
Ali (A.S.) ni Imamu wao, lakini hawako tayari kusema mambo ambayo yatawaudhi watawala wale wenye kiburi na Amerika …

Kwa wale wasemao kwamba wao ni Mashia wa Imamu Ali na yeye ni Imam wao, ni nini maana halisi ya Uimamu kuhusiana na hayo”.

Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on July 5, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: