Siku ya Mabinti Duniani: kwa Munasaba wa Kuzaliwa kwa Binti mtukufu Fatemah Masouma.

5c6b01b0667449270ea712bc26a25f2d

Katika mji mtakatifu wa Madina, ndani ya Nyumba takatifu walikuwa wakisubiri kuwasili kwa mtoto mchanga aliyekuwa anategemewa.

Katika nyumba ya Imam Kadhim (A.S.), Najma, mke wa Imamu kwa hamu kubwa alikuwa akisubiri kuwasili kwa mwanawe mpendwa; alikuwa akihesabu usiku na mchana. kadiri muda ulivyokuwa unasogea nyumba Imamu ilizidiwa na furaha.

Hatimaye, siku na wakati ukawadia, tarehe 1 ya Dhil-Qa’dah 173 (A.H) wakati Allah alipomruzuku Imamu wa Saba (7) Musa Kadhim (A.Ş.) ruzuku tukufu ya mtoto kike. Kuja kwa mtoto huyu na kufumbua jicho lake ndani ya nyumba ya Imamu ilileta furaha kubwa ndani ya familia ya Imamu na  macho ya mtoto huyu yaliokuwa yaking’aa.

Watu wote wa nyumba tukufu ya Mtume walikuwa katika furaha kubwa isiyo na kifani kwa kuzaliwa kitoto hiki kichanga na zaidi ya Imamu, hapakuwa na mtu yeyote mwenye furaha kumzidi mkewe Imam  Bi Najma.

Hii ni kwa sababu Binti huyu alikuwa ni mtoto wake wa pili ambaye aliruzukiwa, baada ya miaka 25 iliyopita, kwani ni katika mwezi huo wa Dhil-Qa’dah, Bi Najma alijifungua mtoto wa kiume ambaye baada ya baba yake alikuja kuwa Imamu na alikuja kubeba jukumu la Uimamu na kuongoza ummah wa Waislamu.

Ndiyo! Hiyo ilikuwa ni Mwaka 148 (A.H.), wakati Imamu wa nane (8), Ali (A.Ş.) alizaliwa na ambaye alipewa jina la Ridha. Najma alikuwa katika furaha kubwa isiyo na kifani kwa kupata mtoto wake wa kiume wa kwanza na baada ya miaka kupita siku kama hii ya leo Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema aliwaruzuku tena yeye na mume wake Imam Musa Kadhim (A.Ş.) ruzuku ya  binti na dada kwa Imam Ridha (A.Ş).

Imamu Musa Kadhim (A.Ş) alimpa binti yake huyu mchanga jina la Fatima, kwa sababu ya mapenzi yake na ukuruba wa pekee aliyokuwa nao na bibi yake Fatimah Zahraa (S.A). Kiasi cha Usafi wa Bi Fatima Zahraa, na ucha Mungu wake ilikuwa ni kama vile kwamba baada ya kufariki kwake sifa hizi zote zilihamishiwa kwa Binti (Mtakatifu) “Masouma”. Hii ni kwa sababu kama alivyokuwa Baba yake, muda wote alijiweka mbali na maovu yote na madhambi.

Jina hili la Fatemah, lilikuwa ni jina lenye historia kubwa na lililokuwa likikumbukwa sana miongoni mwa watu wa Ahlul bayt ambao walikuwa na kumbukumbu nyingi za huzuni na furaha kwa maisha walioishi na Bibi Fatima Zahraa (Mke wa Imam Ali) (sa) wakati wa Maisha yake matukufu.

Ilikuwa ni utamaduni kwa  mtu yeyote aliyechagua jina la Fatimah na kuwapa binti zao, walikuwa wakiwapa heshima mabinti zao sawa na vile mtume (S.A.W.) alikuwa akimpa heshima na kumpenda binti yake Fatima Zahraa. Mtume alikuwa kamwe hakuwahi kumpuuza wala kumdhalilisha. Imamu Musa Kadhim (A.Ş.) pia alifuata barabara mila hii na alikuwa akimpenda sana binti yake huyu mdogo na kamwe hakuwahi kushindwa kuonyesha na kueleza wema wake na upendo wake kwa binti yake huyu.

Fatima Masouma alikuzwa na kulelewa chini ya uangalizi wa baba yake na mama yake mpendwa na alikuwa siku hadi siku akijifunza mambo mapya kutoka kwa wazazi wake wawili hao.

Kama baba yake Fatima Masuma alikuwa Imamu wa Waislamu na mtu aaliyekuwa akiongoza katika ucha Mungu wake na usafi wa moyo, basi mama yake Masuma pia alikuwa ni Mama mchamungu na mwaminifu ambaye alikuwa amehitimu masomo yake muhimu ya Uislamu kutoka katika darasa la wifi yake na mke wa Imamu Jafar Sadiq (A.Ş). Kwani katika siku hizo alikuwa ndiye mwanamke mwenye akili zaidi miongoni mwa wanawake wote na ilikuwa ni kwa sababu hiyo mama yake Imamu Kadhim (Hamideh) akamuomba amchumbie na kumuoa.

Binti huyu mtukufu Fatimah Masouma alitumia vizuri fursa hii na kufaidika kusoma kutoka kwa baba yake, kaka yake na Mama yake mchamungu. Maisha yake yote ya usichana yalikuwa ni maisha yaliyojaa mafunzo sahihi ya Uiislamu. Kila Ijumaa waislamu walikuwa wanatabia ya kuja nyumbani kwa Imamu wakitokea Madina na maswali yao ya kidini wakitaka Imamu awajibu. Baada ya kupata majibu ya maswali yao kutoka kwa Imamu Kadhim (A.Ş), walirudi katika mji yao wakiwa na furaha kubwa. Kwa bahati mbaya, pindi ambapo Imam Kadhim alikuwa mbali na Imam Ridha (A.Ş.) alikuwa pia hayupo. Waislamu kwa kushindwa kupata majibu ya maswali yao walikuwa wakirudi majumbani kwao wakiwa na masikitiko makubwa sana na unyonge.

Mara moja Bi Fatimah Masouma aliposhuhudia huzuni hii katika nyuso za waislamu alishindwa kujizuia na akazidai na kuzichukua karatasi hizo kutoka kwao na kujibu maswali yao yote. Waislamu walifurahi sana na kuondoka. Wakiwa njiani nje kidogo ya mji wa Madina walikutana na Imamu Kadhim (A.Ş) na waislamu wakamwarifu juu ya yote yaliyotokea huku nyuma nyumbani kwa Imamu. Imamu akawaomba azitizame hizo karatasi ili ajiridhishe na majibu ya Binti yake na baada ya kusoma alionyesha furaha yake, na akamsifu kwa umahiri na elimu yake kwa kutamka sentensi fupi akisema “Jalia baba yake atolewe Kafara kwa ajili yake.”

Tunatoa Mkono wa Heri, Pongezi na Fanaka kwa kumbukumbu ya kuzaliwa Binti huyu Mtukufu, Bint Fatima Masouma na Kwa Mabiti wote wa kiislamu duniani katika siku hii tukufu ya kuzaliwa kweke.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 4, 2016, in Habari na Matukio, Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: