USANIFU WA ULIMWENGU MPYA WAJITOKEZA KWENYE GHASIA ZA MASHARIKI YA KATI

 

USANIFU WA ULIMWENGU MPYA WAJITOKEZA  KWENYE GHASIA ZA MASHARIKI YA KATI (New global architecture emerges out of ME chaoscapture171

Mwandishi: Zafar Bangash

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Marekani Condolezza Rice aliyaelezea mashambulizi ya Wazayuni ya Julai-Agosti, 2006 dhidi ya Lebanon kwa tabasamu la kubwa kama “uchungu wa kuzaliwa kwa Mashariki ya Kati Mpya.” Hakuweza kudhania kwamba hali hiyo ingegeuka kuwa tofauti kabisa na vile alivyotazamia. Leo hii sio tu kwamba kuna sura mpya katika Mashariki ya Waislamu (pia inajulikana kama Mashariki ya Kati) lakini usanifu wa ulimwengu pia umebadilika kabisa. Wamejitokeza wasanifu wapya ambao hawapo tayari kabisa kukubali maoni y kipekee ya Marekani katika mambo ya ulimwengu.

Hili ni dhahiri kabisa kwa namna ambavyo matukio yamejitokeza nchini Syria, nchi ambayo imekumbwa na vurumai na mauaji kutoka nchi za kigeni kwa miaka mitano. Ni kweli, miundombinu ya nchi hiyo imeharibiwa lakini lengo la msingi nyuma ya uhalifu huu – la kuingusha serikali ya Rais Bashar al-Asad – limeshindikana kutokana na mchanganyiko wa mambo ambayo yanatoa ishara kwenye mwelekeo wa baadae wa matukio.

Vurugu zinazoendelea nchini Syria zimesababisha kutokeza kwa kambi mbili ambapo mojawapo ya hizo kambi mbili ni kambi ya uchokozi na nyingine ni kambi ya upinzani. Wachokozi wamepania vibaya kuipindua serikali ya al-Asad ambapo vuguvugu la upinzani, kama jina linavyoashiria, nao umepania na kudhamiria vivyo hivyo kutokuruhusu litokee jambo hilo. Wachokozi ni pamoja na mabeberu na Wazayuni na mawakala wao (makundi ya kigaidi) na serikali vibaraka  (Saudi Arabia, Uturuki, Qatar na Jordan). Kundi la harakati za wapinzani ni pamoja na Iran ya Kiislamu, Hizbullah, Russia, na kwa kiwango kidogo Iraq na China.

Wakati wa vita hivi vilivyolazimishwa kutoka nje ambavyo vimedumu kwa miaka mitano, majeshi ya Syria yalizidishwa zaidi na kuwa katika hali ya kujihami. Majeshi hayo ilibidi yalirudi nyuma na kujikita kwenye majiji (isipokuwa Aleppo tu, hata hivyo jiji hilo pia linakaribia kukombolewa). Licha ya hili, hapakutokea mapungufu ya kiwango kikubwa katika majeshi ya Syria. Ni kweli, kwamba jeshi la Syria lilipata hasara kubwa dhidi ya mamluki waliokuwa wakifurika kwa wingi kupitia mpaka wa Uturuki, wakiwezeshwa na kusaidiwa na jeshi la Uturuki, lakini jeshi la Syria halikuvunjika.

Usaliti wa Bani Saud:

Serikali ya Saud imetoa msaada wa kifedha na pia kulipia kuwapatia silaha mamluki. Silaha za kivita zilizonunuliwa kutoka Croatia zilisafirishwa kwa ndege za CIA hadi Jordan na halafu kupelekwa Syria kimagendo. Wasaudia pia wanaeneza propaganda yao yenye sumu ya utakfiri na kupelekea watu kukatwa vichwa, kuliwa viungo vya watu, na kufanyika ubakaji kwa kiwango kikubwa. Ukatili kama huo ulisababisha mageuzi makubwa ya kifikra miongoni mwa Wasyria wengi, hata wale ambao walikuwa wapinzani dhidi ya serikali. Kama mbadala wa al-Asad ungekuwa ni ukatili namna hiyo, wasingetaka kuwa nao huo.

Serikali ya Syria wala haikusambaratika, kama ilivyotokea Libya. Kwa kweli, uzoefu ambao mabeberu wameupata nchini Libya ambako serikali ilivunjika haraka, ulisababisha wao kushindwa kusoma alama za nyakati na hali ilivyo nchini Syria. Walidhani na serikali ya Asad pia ingeporomoka katika kipindi cha miezi michache tu kama sio mapema zaidi ya hapo. Hiki kilikuwa kiitikio cha kawaida ambacho kilisikika mnamo siku za mwanzo wa vita. Operesheni kadhaa za udanganyifu wa kutumia bendera (hususani mashambulio ya kikemikali mahali paitwapo Ghouta mnamo mwezi wa Agosti, 2013) yaliyopangwa na Wasaudi na Waturuki kwa lengo la kuishawishi Marekani iishambulie Syria moja kwa moja, pia zilishindwa.

Umoja wa Upinzani:

Ilikuwa ni katika hatua hii ambpo Iran ya Kiislamu ilifanya uamuzi wa kistratejia wa kuja kuisaidia Syria ambayo ni mshirika wake kwa namna yenye kujitokeza zaidi (Iran na Syria zina ushirikiano wa kistratejia na mkataba wa kiulinzi). Mpaka sasa Tehran imekwishatoa msaada wa kisiasa, kiuchumi na pia washauri wa kivita kwa serikali ya Syria katika kushughulikia vita vilivyochochewa kutoka nje.

Kwa kuwa na historia ndefu ya uhusiano wa nchi hizi mbili, Tehran haingeweza kumwacha mshirika wake katika kipindi chake cha kuhitaji msaada pamoja na kwamba mwelekeo wao wa itikadi ni tofauti kabisa. Syria ilikuwa nchi ya tatu, baada ya iliyokuwa Umoja wa Soviet (Urusi ya zamani) na Pakistan kuitambua Jamhuri ya Kiislamu mnamo Februari 1979 kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Zaidi ya hayo, Damascus iliiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu wakati dhalimu wa Iraq Saddam Hussein alipoanzisha vita yake ya uvamizi (1980-1988) kwa kuungwa mkono na mabeberu, Wazayuni na madikteta wa Arabuni katika jaribio ambalo halikufanikiwa la kuiangamiza Dola ya Kiislamu ambayo haikuwa na uzoefu wowote bado wakati huo. Pia Syria imekuwa na umuhimu mkubwa katika kurahisisha msaada kwa kundi la upinzani la Kiislamu la Hizbullah nchini Lebanon ambalo linakabiliwa na uvamizi na ukaliwaji wa kizayuni.

Palikuwepo na mambo mengine yaliyokuwa yanaendelea katika ngazi ya kimataifa ambayo pia yalikuwa na umuhimu vivyo hivyo. Russia na China zilikataa kuruhusu azimio lingine kupitishwa kwa haraka kupitia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama ilivyofanyika kwa Libya mnamo 2011 (UNSC Resolution 1973) ambalo lililazimisha kuwepo na ukanda usiopita ndege. Mabeberu na Wazayuni walitumia azimio hili kujiingiza katika kudondosha mabomu na kufanya mauaji ya halaiki katika nchi hiyo ya Afrika ya Kaskazini. Sasa hivi Libya ipo katika vurugu mchafukoge. Syria ni muhimu sana kistratejia kuruhusu ifanyiwe kama ilivyofanyiwa Libya. Russia ina kituo cha wanamaji hapo Tartus na ingekuwa ni hasara kubwa kwa Moscow kukifunga kituo hicho katika bahari ya Mediterrania kama mabeberu na Wazayuni wangefanikiwa.

Kizazi cha Saud na Urusi (Russia):

Mabedui wa Najdi pia wamehusika tangu siku ya kwanza, pamoja na mabinamu zao wanaowatii, Wazayuni, katika kuidhoofisha Syria. Ambapo inajulikana zaidi kabisa kwamba Wasaudi ndiyo wanaounga mkono wakubwa wa ugaidi, walitoa utibitisho huo kwa mara nyingine tena wakati mkuu wa usalama wa Saudia – Bandar bin Sultan alipokiri kwa Rais wa Russia Vladimir Putin wakati wa mkutano wao mnamo Julai, 31, 2013. Bandar, mtu wa tabia ya rushwa, alimwambia Putin: “Ninaweza kukupa uhakikisho wa kulinda michezo ya Olimpiki ya wakati wa baridi – Winter Olympics katika jiji la Sochi lililopo karibu na Black Sea mwaka ujao (2014). Makundi ya Chenchen ambayo yanatishia usalama wa michezo hiyo yanadhibitiwa na sisi.” Hili limethibitishwa kupitia maelezo ya kidiplomasia ambayo yalivujishwa ya mkutano wa mwaka wa 2013 ambamo Bandar alitafuta ushirikiano wa Russia kuhusu masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na Syria, akamwambia Putin kwamba kama Moscow ingeacha kumuunga mkono al-Asad, basi Riyadh ingeipatia Russia mabilioni ya dola katika manunuzi ya silaha.

Kufuatana na nyaraka hizo hizo zilizovujishwa, Putin hakuchukulia tishio hilo kwa urahisi na inasemekana alimwambia mgeni huyo kutoka Saudi: “Tunajua kwamba ninyi mmeyaunga mkono makundi ya kigaidi ya Chenchen kwa kipindi cha muongo moja mpaka sasa. Na huo msaada, ambao umeutamka kwa uwazi sasa hivi, hauendani kabisa na malengo ya kawaida ya kupambana na ugaidi wa kimataifa ambao umeutaja. Sisi tunapendelea kuendeleza uhusiano wa kirafiki kwa mujibu wa kanuni wazi na zenye nguvu.” Maofisa wa Russia wanaojua mazungumzo hayo, walithibitisha kwamba Putin alikasirika. Alikatisha mazunumzo hayo haraka na akamuonesha Msaudia huyo mlango wa kutokea.

Njama za Saudia, ambazo zilifanyika kwa matakwa ya mabwana zao mabeberu na Wazayuni za kuhujumu ushawishi wa Iran ya Kiislamu katika kanda hiyo zimekwenda kinyume na matarajio yao. Badala yake, machafuko ya Syria yameileta Russia na China karibu zaidi na Iran. Ushirikiano huu mpya, japokuwa sio rasmi, umetoa changamoto yenye nguvu sana kwa ubeberu na Uzayuni. Kwa kufutiwa vikwazo vilivyowekwa kinyume cha sheria, Iran ya Kiislamu imefanya haraka sana kuchukua nafasi yake halali katika mpango wa kidunia. Iran imetambuliwa kama dola yenye nguvu katika kanda hiyo kushinda dola nyinginezo ambayo bila msaada wake hakuna matokeo mazuri yanayoweza kupatikana katika kanda hiyo. Na Tehran haikufanya hivyo kwa kutoa vitisho; yenyewe imesimamia juu ya kanuni na kuonesha uwezo wake na kuzisimamia kwa udhihirishaji wa nguvu, kama ukihitajika.

Uchochezi wa Kimadhehebu:

Katika vyanzo vya habari vya nchi za Magharibi, upinzani wa Saudia dhidi ya Iran umewekwa katika muktadha wa uhasama kati ya Sunni na Shia. Msimamo huu ni wa kimakosa kabisa kwa sababu kadhaa. Hawa Mabedui wa Najdi ambao wanakalia Rasi ya Arabuni hawawakilishi Waislamu wa madhehebu ya Sunni. Wala hawawakilishi Malafi, pamoja na kwamba wao kwa kutaka kuficha tafsiri hasi ya Uwahhabi, wao hujiita wafuasi wa Salafi. Iran kamwe haijajiwasilisha kuwa yenyewe ni mwakilishi wa madhehebu ya Shia; uongozi wa Iran kwa kawaida unazungumzia kuhusu umoja wa Waislamu. Kweli, wapo wafuasi wa madhehebu ya Shia ambao uoni wao kiakili ni finyu hata nchini Iran lakini wao hawamo katika mamlaka za kufanya maamuzi.

Katika viwango vya kisiasa na kistratejia, Saudi Arabia haiwezi kuwa kushindana na Iran ya Kiislamu. Kizazi cha Saudi (kwa jina jingine Nyumba ya Saudi) ni watu wasiostaarabika kutoka jangwani na licha ya kuishi kwenye makasri kwa miongo kadhaa, mwenendo wao usio wa kiadilifu haujasafika kwa vyovyote vile. Tabia mbaya ndiyo kinasabu (DNA) chao.

Wakati wao wanajiingiza kwenye ukatili uliovuka mIpaka dhidi ya watu dhaifu na wasio salama kama vile wafanya kazi wa nyumbani kutoka Kusini na Kusini Mashariki ya Asia, ambao kiasili ni waoga. Wao huishi wakati wote wakihitaji ulinzi kutoka nje. Kwa miongo michache ya uwepo wao, walikuwa wanawategemea Waingereza. Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, wakawa vibaraka wa Marekani. Sasa kwa kuwa mwelekeo wa Washington umehama kutoka Mashariki ya Waislamu na kuelekea Asia ya Mashariki, Bani Saudi sasa wamechukua ulinzi kutoka kwa Wazayuni. Ushirika wao wa siri sasa umekuwa hadharani.

Muungano wa Kiuchumi wa Eurasia:

Kizazi cha Saudi, hata hivyo, ni wachezaji wadogo sana katika mandhari kubwa ya siasa kidunia. Zaidi ya hayo, maisha yao ya kujiweka pembeni nayo pia yanakwisha. Ni utokezaji wa ushirikiano mpya na kwa hiyo, mashirika mapya yenye nguvu ambayo yataunda maendeleo katika karne ya 21. Sasa hivi dunia haielekei upande moja tu kisiasa bali ina mielekeo mingine na Iran ya Kiislamu ikiwa na wajibu muhimu humo.

Na sababu zake ni hizi hapa.

Russia imeibuka kutoka kwenye mapigo ya kisaikolojia iliyoyapata kama matokeo ya kifo cha Shirikisho la Kisoshalisti la Kisovieti. Viongozi wake sio wapumbavu kama alivyokuwa Boris Yeltsin; bila kujali maoni ya mtu kuhusu sera zao, uongozi wa Kremlin unajiendesha kwa heshima na kujiamini. Pia wanajua namna ya kulinda maslahi yao.

Russia chini ya Putin imesonga mbele katika kuimarisha nafasi yake katika Asia ya Kati, ambayo inaitwa “nchi jirani ya nje.” Russia imefanya hivyo kupitia hatua zilizorekebishwa. Mathalani, pendekezo la kuanzisha Umoja wa Kiuchumi wa Ulaya na Asia (Eurasia Economic Union (EEU), ambao umeundwa juu ya Ueropean Union, halikutoka Moscow lakini lilitolewa kwanza na Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan alipokuwa anatoa mhadhara kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Moscow State University mnamo mwaka 1994. Ilichukua miongo miwili kabla ya mkataba kusainiwa mnamo tarehe 9, Mei, 2014 wa kuanzisha umoja huo. Hata hivyo, muungano huo ulijumuisha nchi tatu tu: Belarus, Russia na Kazakhstan. Muungano huo ulianza kufanya kazi mnamo tarehe 1, Januari, 2015 na kwa sasa ulijumuisha nchi za Armenia na Kyrgyzstan pia. Huu ni ushirikiano wa uchumi wa kibiashara tu lakini muunganiko wake umeendelea zaidi kuliko ule wa Umoja wa Ulaya kwa sababu nchi hizi kabla ya hapo zilikuwa sehemu ya Shirikisho la Kisoshalisti la Kisoviet na hivyo zilikuwa zimeungana kwa namna ya utatanishi.

Chama cha Ushirikiano wa Shanghai:

Shirika jingine ambalo ni la umuhimu mkubwa ni lile la Shanghai Cooporation Organization (SCO). Kama linavyodokeza jina, ushirika huu ulianzishwa Shanghai mnamo mwaka 2001 na wanachama wake wa sasa ni pamoja na China, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Russia, Tajikistan, na Uzbekistan. Katika mkutano wake wa mwisho uliofanyika huko Ufa mnamo Julai 10, 2015, Pakistan na India nazo pia zilikubaliwa rasmi kuwa wanachama kamili. Mchakato huu utakamilishwa mnamo mwaka huu wa 2016. Iran nayo pia imealikwa kujiunga na shirika hili ambalo sio linaunganisha kanda hii kiuchumi tu lakini pia kisiasa na kijeshi. Afghanistan itakuwa mwanachama kamili kama na wakati ambapo mapigano yakikoma nchini humo.

Umuhimu wa Oganaizesheni ya Ushirika wa Shanghai unaweza kuonekana kulingana na idadi ya watu. Kwa sasa hivi una takriban watu bilioni 1.42. Kwa kujiunga Pakistan na India kama wanachama kamili hivi karibuni, idadi ya watu itaongezeka maradufu na kujumuishwa kwa Irani kutafikisha jumla ya idadi ya watu kuwa bilioni 3. Hiyo itakuwa takriban nusu ya idadi ya sasa ya watu duniani katika kanda ambayo inanyanyuka kwa kumiliki madini mengi na rasilimali za nishati. Ukanda wa Eurasia utakuwa ndio kichwa ama injini ya ukuaji wa kiuchumi wa dunia.

Mkondo Mpya wa Hariri: 

Sehemu nyingine ya tatu ya shirika hili linalojitokeza ni Ukanda mmoja, Ari ya Mkondo mmoja ya China, (One Belt, One Road Initiative – ambayo inajulikana pia kama Mkonda Mpya wa Hariri). Ni mojawapo ya miradi mikubwa ya kiuchumi wenye tamaa kubwa ulioanzishwa katika historia ya zama hizi ambao utaunganisha Asia ya Kusini-mashariki na Asia ya Kusini na Kati. China imeahidi kuwekeza mamia ya mabilioni ya dola katika mradi huu. Mradi wa The China-Pakistan Economic Corridor (wenye kibandiko cha bei cha dola bilioni 46) – ni sehemu ndogo tu ya mpango wote wa uwekezaji. Iran ya Kiislamu imeomba rasmi kujiunga kwenye mradi huu mkubwa wa miundombinu. Mwezi Mei uliopita Raisi Putin alitangaza rasmi muungano wa Eurasia Economic Union infrastructure na Silk Road Initiative (Muungano wa Uchumi na Miundombinu wa Ulaya na Asia na Mkondo wa Ari Hariri).

Umuhimu wa Eurasia Economic Union, The Shanghai Cooperation Organization na The Silk Road Initiative ni kwamba mashirika haya yanaziunganisha nchi ambazo mipaka yao inaegemeana. Nchi hizi zinaunda sehemu kubwa ya ardhi yenye rasilimali nyingi za kushangaza sio tu katika rasilimaliwatu lakini pia katika rasilimali za madini na nishati. Uwezo wa kiuchumi wa nchi hizi hauwezi kusisitizwa zaidi.

Ni uwezo wa kiuchumi na matumizi yake yanayofaa ndio unaojenga nguvu ya kijeshi. Kwa kweli, nchi zilizo nyingi hutumia (au hutumia vibaya) nguvu zao za kijeshi kwa lengo la kuongeza manufaa yao ya kiuchumi. Hili linatoa maelezo kwa nini nchi kama Afghanistan na Pakistan zinalengwa kwa sababu zinazo rasilimali nyingi za madini ambazo madola makubwa ya kinyonyaji yanazitamani.

Iran ya Kiislamu na Kanda Hii:

Pale ambapo faida za Iran kujiunga na Eurasia Economic Union, The Shanghai Cooperation Organization na Silk Road Initiative ziko dhari, Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran itatoa nini badala yake? Hapa ni orodha ya haraka hapa chini.

Iran ya Kiislamu sio tu kwamba inaleta nguvu ya idadi ya watu milioni 80 lakini katika idadi hiyo ni walio wengi bado ni vijana, wenye elimu, na waliohamasishwa sana. Kiwango chake cha wanaojua kusoma na kuandika ni moja ya viwango vikubwa duniani: 82% katika idadi ya watu wazima, na 97% miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 na 24. Iran ya Kiislamu imepiga hatua kubwa katika teknolojia ya uhandisi na ulinzi na pia utafiti wa kuanzia kwenye shina. Mafanikio haya yalipatikana kama matokeo ya vikwazo vilivyokuwa kinyume cha sheria ambavyo Iran iliwekewa kwa kipindi cha miongo na viligeuka kuwa neema njema iliyofichika.

Dunia inaitambua Iran kama ni nchi ambayo ni tajiri kwa mafuta na akiba ya gesi. Hii ni kweli kwa sababu Iran ni nchi yenye akiba kubwa ya gesi duniani na pia ni nchi ya nne duniani kuwa na hifadhi kubwa ya mafuta na ambayo inaweza kuongezeka kwani visima vingine zaidi vya mafuta vinaendelea kugunduliwa. Lakini hata hivyo, rasilimali yake ya nishati, haiakisi taswira halisi.

Iran ina akiba kubwa ya shaba duniani; ongeza na madini ya boksiti inayotoa almimi, makaa ya mawe, chuma, risasi, na zinki na taswira bora zaidi inajitokeza. Pia kuna akiba yenye thamani kubwa ya alumini, kromiamu yenye rangi nyingi, dhahabu, manganizi, fedha, bati, na tungsten – madini ya kutengeneza chuma cha pua. Machimbo yake ya dhahabu hayajatumika yote kwa ukamilifu. Na nani ambaye hajasikia kuhusu mazulia ya Iran (Mazulia ya Uajemi na hadithi za kale) na pia karanga za kiajemi. Lazima izingatiwe akilini kwamba Iran imepanua utengenezaji wa bidhaa zake kiuchumi na sio kwamba inategemea mapato ya mauzo ya mafuta na gesi tu nchi za nje.

Kuondolewa kwa vikwazo haramu sio tu kwamba kumipa Iran fursa ya kupata mabilioni ya dola ya fedha zake zilizoshikiliwa kwa nguvu lakini patatokea mlipuko wa shughuli za kiuchumi wakati nchi inaelekea kwa haraka kuwekeza katika ugunduzi wa mafuta na gesi, manunuzi ya vitu vya tiketi kubwa kama ndege za abiria na vitu vingine vingi. Sasa Iran ipo tayari kwa kuanzia kuruka. Hata kabla ya vikwazo kuondolewa rasmi, palikuwepo na mafuriko ya watalii kutoka nchi za jirani – walio wengi wakiwa mahujaji. Hali hii itanyanyua juu maendeleo ya mahoteli na usafirishaji.

Kuungana kwa Iran na sehemu kubwa ya ardhi kubwa ya Eurasia na pia kujiunga na Silk Road Initiative kutafanya kanda hii kuwa kitovu cha uchumi cha dunia. Kuna uhamiaji mkubwa katika mambo ya dunia na ukuaji wa uchumi una mwelekeo wa kuwa na matokeo yenye athari kubwa kisiasa vilevile.

Karibu kwenye usanifu wa dunia mpya katika dunia yenye mwelekeo zaidi ya moja.

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 4, 2016, in Uncategorized. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: