Hadhrat Masouma (A.Ş), Msimulizi Mkubwa na maarufu wa Ahadith za Mtume (saww)

photo_2016-08-05_09-00-24

Wasimulizi wa Hadithi za Mtume, “Muhaddith” kutoka kwa Mtume Muhammad (S.A.W.) na Maimamu Maasum (A.Ş) wanabeba haki kubwa juu ya shingo zao kwa ummah huu wa Kiislamu; na lau sio juhudi zao kubwa, mafundisho haya ya Kiislamu yasingeweza kufika kwetu.
Mtume mtukufu (s.a.w) alikuwa akiwashajiisha na kuhamasisha masahaba wake kusikiliza na kusimulia Hadith, akisema: “Mwenyezi Mungu ampe nuru mja yeyote ambaye anasikiliza maneno yetu na kuyahubiri” . Imamu Jafar al-Sadiq (as) akizungumzia sual hilo hilo amesema “Kama mtu atajifunza hadith moja kuhusu Halali (Inaruhusiwa) na Haramu (Marufuku) kutoka kwa mtu mkweli, ni bora kuliko Dunia nzima, Dhahabu na Fedha zote zilizomo ndani yake” .
Aidha miongoni mwa wasimuliaji wa hadith, tunapata pia wapo wanawake wema ambao majina yao matukufu yameandikwa miongoni mwa Muhaddith, maarufu zaidi kuliko wote, miongoni mwao ni wanawake wa familia ya Mtume (A.S). Na kati ya hao, Binti Masouma (A.S) ni mmoja ya wanawake hao wema, ambaye amepokea na amehadithia hadith, kwa mtiririko (silsila) wa wapokezi, kutoka bibi yake Bibi Fatimah Zahra (S.A.), na kutokana na utukufu wa Mapokezi yake, watu wa madhehebu yote ya Mashia na Masunni wamezizingatia hadithi zake kuwa ni hadithi sahihi, moja ya hadith hizo ni kama ifuatavyo:
Hafidh Shams al-Din Jazari (aliyefariki 833 AH), mmoja wa wanachuoni wa madhehebu ya Kisunni, ameandika kitabu muhimu sana chenye jina “Asna al-Matalib fi Manaqib Sayyidina Ali bin Abi Talib (A.S)”. Ndani ya kitabu hicho wakati akisimuliwa baadhi ya hadith inayohusu tukio la Ghadir (Kuchaguliwa Imam Ali kuwa mrithi wa mtume), amerejea hadith kutoka Bi Fatimah (A.S) ambayo miongoni mwa mtiririko wa wapokezi waliopokea hadithi hiyo yumo Binti Masumah (a.s). Katika Hadith hiyo, Binti Fatimah Masouma (as) anasimulia kwa kusema: “Je, mumesahau maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika siku ya Ghadir ambapo alisema: “Mtu yeyote ambaye mimi ni Mtawala wake (Mawla), Basi Ali (a.s) ni Mtawala wake wake (Mawla) ‘na pia alisema: “Wewe (Ali) kwangu mimi ni kama Harun kwa Musa. ”
Hadith hii pia imesimuliwa na Muhaddiths mengine wa kisunni, kama vile Amritsari na Shoukani, kwa maneno yanayofanana sawa sawa na mlolongo wa wapokezi kutoka kwa Binti Masumah (a.s). Kwa rejea za Shia, wanazuoni kama vile Mir Hamed Hussain na Allamah Amini pia wameisimulia hadith hii kutoka chanzo kimoja. Kwa mujibu wa taarifa hizi, Binti Masouma (a.s.) amekuwa akitambuliwa kama Muhaddith miongoni mwa Wanamke kote katika Shia na Sunni, na hadith kadhaa zimesimuliwa kutoka kwake, mfano moja ni huo tulioutaja hapo juu.
Sisi, Waislamu, tuna fahari kubwa kwamba Hadith za Mtume Muhammad (SAW) na zile za Ahl al-Bayt (AS) zimesimuliwa na kutufikia sisi kwa njia ya watu kama hao wema, na ni juu yetu kwa kuchangia sehemu yetu katika kulinda kueneza masomo hayo.
*Kipande hiki kimechukuliwa kutoka katika Kitabu: “Ukarimu Binti wa nyumba tukufuya Ahl al-Bayt (A.S)”, kilichoandikwa na Ali Akbar Mahdipour.
________________________________
1-Muhaddith ni cheo katika uislamu, akimaanisha yule anajua na anasimulia hadithi za, mtirirko wa wapokezi (Sanad), wa awali wapokezi maarufu
2- Sunan Ibn Majah, vol. 1, p. 85- Al-Ghadir na Allamah Amini, vol. 8, ukr. 154
3-Wasa’il al-Shia, vol. 27, p. 98
4-mlolongo wa wapokezi maana yake ni seti ya watu ambao wamesimulia Hadith kutoka moja hadi mwingine.
5-Asna al Matalib, uk. 49 & 50

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 5, 2016, in Habari na Matukio, Hotuba na Mawaidha and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: