UNAFIKI NI MZIGO WA LAZIMA WA UOVU

84ea6133-5890-4f14-a9c9-f4c314a32f84

(Hypocrisy is the necessary burden of villainy)
By: Abu Dharr – Crescent International – March 2016

Kila mara sisi tunapoamua kuandika kuhusu suala la Kiislamu mbali ya utawala wa kitajiri wa Saudia, jambo hili la ajabu huja na maamuzi na sera ambazo hutuacha sisi tusiwe na chaguo bali kutoa mwanga wa nuru ya ukweli kuhusu mwenendo wake wa kisiasa usiofaa.

 Mwezi uliopita mfalme wa Saudi Arabia mwenye kujawa na ubeberu alijitokeza na kusema “….Ufalme wa Saudi Arabia huwa hauingilii mambo ya (dola) zingine, na kwamba unayo haki ya kujilinda wenyewe, na kwamba Wasaudi wanawahimiza wengine wasiingilie mambo yetu (Wasaudia) ya ndani!!” Tazama ni nani huyu anayezungumza? Mfalme huyu anazungumza wakati huo huo ambapo Ufalme wake unakusanya wanajeshi 150,000 kuhinikizwa na kuingilia kati mambo ya dola huru inayoitwa Syria. Chumba cha vita nchini Saudia kinabuni mipango ya kupeleka majeshi kutoka nchi zingine nchini Syria: United Arabian Emirates, Jordan, Misri, Sudan, na Uturuki, kuzitaja chache tu. Washauri wa kijeshi wa Kizayuni na kibeberu na wafanyakazi kwa wakati huu wanaingia na kutoka kwa makundi katika nchi hiyo ya Kiislamu kuutayarisha ufalme wa Saudia kwa ajili ya nafasi ya kuongoza mashambulizi katika dimbwi la mkwamo wa Syria. Tayari kitu kinachokaribia kutokea ni operesheni ya Northern Thunder (Ra`d al-Shimal). Wasaidizi wa Saudi wa Uzayuni-Ubeberu wamevurugwa katika jambo la hatari la kijeshi ambalo limekwenda kombo katika mojawapo ya nchi masikini sana hapa duniani: jirani yake upande wa kusini Yemen. Na sasa Uturuki ina sifa yenye mashaka ya kuwa mwanachama wa NATO ya Marekani na kuwa NATO ya Saudia.

Propaganda ya Saudia inasema kwamba shambulio lao la kijeshi ndani ya Syria ni kwa lengo la kutokomeza ISIS, ambao katika mabano sio chochote zaidi ya wanafunzi wa kijeshi na wafuasi wa madhehebu ya Uwahhabi. Sababu halisi ya mpango huu wa kijeshi unaoongozwa au labda tuseme unaofadhiliwa kifedha na Saudia ni kupindua serikali ya Damascus kwa kuwashikiza na kuwapa silaha wapinzani wa serikali nchini Syria. Jambo lote hili la Saudia kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine huru linakuja baada ya uhalisia ulipoanza kuzama kwenye akili za maofisa wa Saudi “kujifunika shuka wakati jua limechomoza”: wao na wapiganaji wao mamluki wanashindwa katika vita vya Syria.

Taswira ya yule afisa na mwanadiplomasia mtulivu wa Saudia imefunguliwa ndani ya kichwa chake. Watendaji wa Uzayuni wa nchini Saudia wamefadhaika, wamekorogwa na wamekasirika siku hizi kama ambavyo haijapata kutokea hapo kabla. Watawala wa Saudia sasa hivi ni shirikisho la kulipa kisasi. Miaka mitano iliyopita imewafyeka wafalme wa Saudia na tabaka tawala makumi ya mabilioni ya dola yasiosemeka bila kutaja kule kupungua kwa nguvu ya mamlaka laini ya Saudia ambayo ofisi zake za kibalozi zilitumia katika ulimwengu wa Waislamu. Shirikisho hili la kulipa kisasi lenye kituo Saudia linajitangaza lenyewe kuwa ni “Sunni” na katika kufanya hivyo linavuna mabaki ya mwisho ya ujinga miongoni mwa Waislamu. Hii ni kukaa mbali baina ya kile ambacho fedha inaweza kununua na ni yupi ambaye anaweza kudhibitiwa na Wazayuni kwa upande mmoja, na kujitawala wenyewe Kiislamu, uhuru, na ukombozi ambao unawasilishwa na Iran ya Kiislamu na uwanja wake wa ushawishi ambao unaenea kuanzia Asia ya Kati hadi Bahari ya Maditeranean.

Tunasita kusema hili lakini ukweli unapaswa uenee: Uturuki watoa maamuzi wake wa wakati huu wamejinasisha kwenye ufidhuli wa Saudia. Maneno ya marehemu Nejmettin Erbakan yanahuika ambapo takriban miongo miwili iliyopita aliwaonnya wale ambao wangekuja kuwa viongozi wa Uturuki wa siku za usoni (AKP) kwa kuwa kwao wenye kuangalia maslahi yao na kusaliti kanuni za Uislamu.

Giza la usiku linatoweka na wale waliokuwa wakifanya maamuzi gizani sasa wanafichuliwa. Ushirika wa kijeshi wa Arabuni na Uturuki ambao unajificha nyuma ya kidokezo cha kimadhehebu wa “Usunni” sio lolote bali ni njama za Wazayuni na Mabeberu kwa lengo la kuwaingiza Waislamu wengi sana wa madhehebu ya Sunni na Shia kwenye jukwaa la operesheni za kijeshi nchini Syria na Iraq ili wawe wanauana wenyewe kwa wenyewe na kuwatoa Wazayuni wa Israel na walio chini yao kwenye jukumu la kuhusika hali ya kivita kama hiyo ya mauaji makubwa.

Mfalme Salman – muuzaji wa vita – lazima atakuwa anateseka kutokana na maumivu makali ya maradhi ya akili, wazimu, na uzuzu pale anaposema kwamba Saudi Arabia haiingilii mambo ya ndani ya nchi zingine ambapo ipo vitani kikamilifu ndani ya Yemen na inajitayarisha kuingia kwenye jungu kubwa la vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria.

Kwa wale ambao bado hawajazama kwenye propaganda ya Saudi ya umadhehebu, tunauliza: ni kitu gani kinachoipatia Saudia mamlaka ya kuanzisha vita vya uvamizi nchini Yemen na – kama inavyoelekea – baada ya muda mfupi itaanzisha vyingine nchini Syria ambapo sio Yemen ama Syria ambazo zinakalia eneo la Saudi Arabia? Kwa kweli, Saudi Arabia inakalia eneo la Yemen tangu katikati ya miaka ya 1930. Lakini, halafu, Israel inakalia visiwa viwili vya Saudi Arabia vilivyopo karibu na Ghuba ya `Aqabah. Kama Wasaudia wangekuwa kujikaza wanaume wa kutosha hasa wangeanzisha vita vya kuyakomboa maeneo yao yanayokaliwa na nchi nyingine. Lakini usitarajie hilo kutoka kwenye kundi la watawala ambalo huchukua amri zao kutoka Tel Aviv na Washington.

Hivi maafisa wa ngazi za juu wa Saudi wamefikiria kuhusu hili la kuingilia mambo ya ndani ya Syria hivi karibuni? Hivi wanasema kweli ya dhati? Saudi Arabia imekuwa vitani kwa mwaka mzima na nchi masikini na iliyofukarishwa ya Yemen ambayo haina miundombinu ya kijeshi ya kuzungumzika na bado Saudi Arabia hawana uwezo wa ushindi wa vita hivyo! Kwenda nchini Syria na kukabiliana na jeshi la Syria ambalo limepata uzoefu ya mapambano wa miaka mitano na utayari sambamba na silaha za kivita za kisasa kutoka Urusi, ukiunganisha na msaada wa Urusi, Iran na Hizbullah katika masuala ya kijesh na kilojistiki – hivi waziri wa ulinzi wa Saudia na maluteni wake ambao ni vijana wamefikiria kwa umakini kuhusu mandhari haya? Au wanachukua amri zinazo kuja kutoka Pentagon na IOF (Israel Offence Force) kwa pupa?

Litakuwa ni tamthilia hasa kuwaona Wahhabi walioandikishwa jeshini kwa mujibu wa sheria (wapiganaji wa jeshi la Saudi Arabia) wanaoelekea Syria wakiwa na Wahhabi waliojiajiri wenyewe- kama wasemavyo maofisa wa Saudi, wanakwenda Syria kupigana na ISIS. Hivi afisa wa Saudi ambaye ni Muwahhabi alioko nchini Syria yupo tayari kumuua ndugu yake au binamu yake – ambaye ni “gaidi” mwingine wa kiwahhabi ambao wote walisoma na kuhitimu kwenye shule ya masomo ya juu na chuo kimoja? Itakuwaje kama baadhi ya masajenti au maofisa walioandikishwa na Saudi wakiacha vikosi vyao vya kijeshi na kujiunga na ndugu zao ambao ni jamii ya “takfiri”? Au kwa namna nyingine, mpango huu utafanyikaje?

Vyombo vya habari vya Israel inawezekana viliwashangaza wajinga vilipoonesha wananchi wao kitendo cha kihistoria cha kupeana mikono baina ya Mtoto wa Mfalme Turki al-Faisal, aliyekuwa mkuu wa usalama wa taifa wa Saudi, na Moshe Ya`alon, aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel. Mtoto huyohuyo wa Mfalme wa Saudi mwaka jana alipeana mikono na Waziri wa Nishati wa Israel Yuval Shteinitz. Upeanaji wa mikono safari hii ulifanyika Munich nchini Ujerumani kwenye mkutano wa kimataifa. Kitendo hiki cha kihistoria cha kupeana mikono na kwa moyo mkunjufu hadharani baina ya maofisa wa ngazi za juu wa Israel na Saudi Arabia kilifuatia na hotuba ya hitimisho la mkutano iliyotolewa na Ya`alon, ambamo aliizungumzia “Mashariki ya Kati.”

Ya`alon alizungumzia kuhusu uhusiano wa Israel na Saudi Arabia na pia uhusiano wa Israel na nchi zingine za Arabuni ambazo hazina uhusiano rasmi wa wazi na Isreal. Ya`alon alisema kwamba Waisrael hudumisha idhaa za mawasiliano na nchi fulani za Arabuni ambazo ni jirani na Israel na zenye mtazamo wa “Sunni.” Ya`alon alisema: “Sizungumzii kuhusu Jordan na Misri tu. Ninazungumzia kuhusu nchi za Bara Arabu – nchi za Ghuba ya Uajemi na nchi zilizopo Afrika ya Kaskazini….Ni jambo la kuhuzunisha kwamba nchi hizo hakuna hata moja hapa kusikiliza kile ninachotaka kusema.” Waziri huyu wa Israel aliwakumbusha waliohudhuria kuhusu maslahi ya pamoja baina ya Israel, Marekani, Ulaya, na serikali za “Kisuni”. Kwanza na mbele kabisa miongoni mwa maslahi haya ni mgogoro na Iran. Waziri huyu wa Israel alisema, “Tunaichukulia Saudi Arabia kama kiongozi wa nchi zenye mtazamo wa ‘Usunni’ dhidi ya Iran.” Aliendelea kusema, “Sisi tunaichukulia Iran kama nchi ovu dhidi yetu (sisi Waisrael) na serikali zenye mtazamo wa ‘Usunni.’” Na kufuatana na ripoti iliyopo kwenye gazeti la Haaretz la Israel, mtoto wa mfalme (Turki) alithibitisha tamko la Ya`alon kwamba “…kuna uhasama baina ya serikali za ‘Kisunni’ kwa upande moja, na Iran pamoja na Muslim Brotherhood kwa upande mwingine…”

Inaonekana kama vile historia inajirudia yenyewe. Wahenga wa jahilia wa Kizazi cha Saud walikuwa na nguvu sana katika ushirikiano wao na Yahud, katika kipindi cha mpendwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anapambana kwa ajili ya uhuru, usawa, na haki, yaani kwa ajili ya Uislamu. Tunajua kutokana na historia yetu kwamba ushirika wa Yahud na Waarabu wa Ahzab ulikoma baada ya kushindwa hawa Waarabu Wayahudi na Wayahudi Waarabu. Somo la kuchukua hapa ni: serikali ya Saudi inauchukulia maisha ya Waislamu kuwa sio kitu cha muhimu na uhai wa Wayahudi kuwa ni kitu cha muhimu kabisa.

Sasa barakoa ya kitambaa inafunuka kwenye nyuso za wasaliti wa Saudi. Matamshi yameanza kujitokeza ambayo yalikuwa ni mwiko kutolewa hadharani kabla ya hali mgogoro wa Syria kuwalazimisha maopereta wa Saudia na Israel kuonesha picha ya uhalisia wao. Uingereza na Marekani haziwezi tena kuficha hali halisi ya wahalifu wawili wa kidini Katika Nchi Takatifu ya Kusini ya (Arabuni) na Nchi Takatifu ya Kaskazini ya (Palestine). Tabaka la mwisho ambalo linalinda hawa mapacha wawili wa kisiasa ni umadhehebu. Na umadhehebu huu utabanduliwa kwenye nyuso mbaya za Uzayuni na Uwahhabi. Vyombo vya habari vya Kiyahudi na Vyombo vya habari vya Kiarabu sasa vimeanza kutoa matamko yenye ushahidi wa kutosha yanayotolewa na maofisa katika nchi za Kiarabu ambazo zinachezewa na Uzayuni na Palestine ambayo inakaliwa na Uzayuni. Sasa tumeanza kusoma na kusikia matamko kama hayo, “Sisi (Waisrael) na ‘Sunni’ tupo kwenye handaki moja dhidi ya Shia; na Iran ni tishio kwa tawala zetu…. Sisi (Waisrael) tutaendelea kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Syria kuhusu lojistiki na matibabu kwa majeruhi wao katika hospitali zetu….Sisi (Waisrael) na Misri na Jordan na nchi za Ghuba ya Ajemi, na nchi za Afrika ya Kaskazini ni muungano mmoja…. Hakuna tena mgogoro wa Palestine na Israel; kwa usahihi zaidi ni mgogoro wa ‘Sunni dhidi ya Shia’….Sisi (Waisrael) tunashirikiana na ‘Sunni’ dhidi ya Iran na Hizbullah kwa sababu wao ni tishio kwa tawala zetu.”

Mwisho kabisa, na tuulize swali hili kwa wasaliti hawa na wahalifu wa kivita katika Bara Arabu: Kama ninyi ni wawakilishi wa Sunni, na mnajiita wenyewe ni walinzi wa madhehbu ya Usunni, sasa kwa nini hata hamjafikiria wala hata kujinong`oneza wenyewe kwa wenyewe kuhusu kuikomboa Palestine? Hivi si kweli kwamba Wapalestine walio wengi ni Sunni? Hivi hawapo Wapalestine ambao ni Salafi na Wahhabi? Wapo Wapalestine wengi sana ambao ni Salafi na Wahhabi kuliko Wapalestine ambao ni Shia. Sasa basi kwa nini hamjafikiria kuwasaidia na kuwaunga mkono ndugu zenu ambao ni Sunni? Jibu ni rahisi: hamwachukulii hao kama ni ndugu zenu. Na sababu ya ninyi kuwafanya mfanye kila liwezekanalo kuwapiga “Shia” ni kwa sababu Shia mnaotaka kupigana nao ndio hao ambao walishinda mifarakano na umadhehebu na sasa wapo njiani kuwakomboa “Sunni” wa Palestine. Mnaweza kuishi na Palestine inayokaliwa na Uzayuni mnayoweza kuishi nayo – lakini sio na fikira kwamba “Sunni” wa Palestine atakombolewa na Shia (asiyeendekeza umadhehebu) kuwaruhusu Wapalestine ambao ni Sunni kurudi na kuishi majumbani mwao na miji yao, ambapo ninyi mlitumia sehemu ya maisha yenu mkishiriki kwenye hafla, mnacheza kamari, uzinzi, na kuugeuza Uislamu uwe wa Kizayuni. Yote haya ni mambo ambayo yanatia wasiwasi kwenu kwamba kwa ghadhabu mnaandaa vita kubwa ambavyo vitafanya vibaya na baada ya hapo mtapelekwa kwenye shimo la Abu Lahab na Abu Jahl ambako ndiko masikani yenu.

MWISHO

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 11, 2016, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: