FADHILA NA UTUKUFU WA KUMTEMBELEA DHARII (KABURI) TUKUFU LA IMAM RIDHA (A.S)
Posted by Asadiq Media
Wiki hii wapenzi wa nyumba tukufu ya Mtume (saww) na waislamu wote duniani wanasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ridha (A.S) mjukuu wa Mtume na Imamu wa nane (8) wa nyumba tukufu ya Mtume (Ahlulbayt) aliyezaliwaTarehe 11 Dul Qada 148 AH, Sawa na 765 A.D |
Kaburi tukufu la Imam Ridhaa (Rehema na Amani ziwe juu yake) lililopo katika mji wa Khurasan nchini iran limekuwa ni moja ya maeneo matakatifu katika uislamu, kwani limekuwa ni kivutio kikubwa cha Mapenzi na utakaso mkubwa kiasi hakuna kaburi la vipenzi vya Mwenyezi Mungu duaniani linafikia mapenzi na utakaso wake, kwani mamilioni ya Waislamu duniani huzuru kaburi lake ili kutafuta ukuruba na Mwenyezi Mungu kupitia Baraka za Imamu huyu.Mohammed ibn al-Mu’ammal anasema: “tulitoka pamoja na Imamu wa hadith, shemeji yake Abu Ali Al-Thaqafi na kundi la Masheikh wetu ambao wakati huo walikuwa wamekuja kumzuru Ali ibn Mussa ARidhaa, Tus Ibn Khuzayma akawa analitukuza eneo hilo huku akiwa na unyenyekevu mkubwa na akiomba msamaha kwa Mwenyezimungu karibu ya kaburi hilo kwa kiasi ambacho akatushangaza hata sisi. “Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amelichagua kaburi la rafikiye Imam Ridha, Amani iwe juu yake, kwa utukufu mkubwa, kwani amelifanya kaburi hili kuwa kambi kimbilio kwa wenye kupatwa na Matatizo. Watu walikuja kugundua maajabu haya makubwa. Misitari miwili ya beti za mashairi yameandikwa katika katika upande mmoja wa kaburi hilo ikisomeka kama ifuatavyo: Kama kuna mtu unaridhika kuona kaburi ambalo Mwenyezi Mungu huondoa Matatizo ya yule anayelitizama, basi aje katika kaburi hili hakika Mwenyezimungu amefanya kukaa ndani yake ni utukufu wa pekee sawa na kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. ( Al-Durr al-Nazim, p. 214). Hadithi nyingi zimesimuliwa na wasimulizi lukuki wakitaja utukufu wa kumtembelea Imam ridha hizi ni baadi yake:
|
Zipo hadithi nyingine nyingi zimetajwa na Maimamu waongofu; zikikokoteza watu kuzuru Kaburi la Imam Ridhaa (Rehema na Amani ziwe juu yake) na kuanisha thawabu na fadhili kemkem kwa ziara hiyo. |
About Asadiq Media
Media for publicise the message of Wilaya under Imam SwadiqPosted on August 16, 2016, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0