KHUTBA YA IMAM RIDHA (AS) ALIYOMUANDIKIA AL-MA’MUN (Usiache kusoma)

Wiki hii wapenzi wa nyumba tukufu ya Mtume (saww) na waislamu wote duniani wanasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ridha (A.S)  mjukuu wa Mtume na Imamu wa nane (8) wa nyumba tukufu ya Mtume (Ahlulbayt) aliyezaliwa Tarehe 11 Dul Qada 148 AH, Sawa na 765 A.D

emam-rezz

Al-Mamun alimuomba Imam al-Ridha, Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, amuandikie khutba ili akaisome kwa watu atakawaongoza katika swala, ndipo Imam (as) akaandika khutba hii:

 Sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, ambae ametokea pasipokuwa na kitu, wala sio kwa alivyoviumba hutegemea msaada, wala katika viumbe alivyoviumba , wala sio katika hivyo viumbe ameumba vitu bali alisema tu “kuwa” na kikawa

Ninakiri kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah, ambaye ni wa pekee na asiye na mshirika, amejitenga mbali na wenye kukinzana nae na kushindana nae wenye kumshirikisha na kumsingiza ana Mtoto, Na ninakiri pia kuwa Muhammad ni mja wake mteule na mtume wake mtukufu.

Alimtuma akiwa na Qur’an yenye maelezo (kamili), akaunganisha ufunuo (wahy), na upambanuzi wake uliotakasika (Furqan) kwa hayo akabashiria habari njema ya malipo (ya pepo) na akaonya dhidi ya Adhabu zake, Mwenyezi Mungu amrehemu yeye na watu wa nyumba yake tukufu.

Ninawausieni enyi waja wa Mwenyezi Mungu, kumuogopa/kumcha Mwenyezi Mungu, ambaye anayajua (matendo yenu) ya siri na ya dhahiri, na anajua mnachokificha, hakika Mwenyezi Mungu hawezi kuwacha hura bila kuwa na lengo; wala hakuwaumba bila sababu (maalum); na wala hatokuacha bila kukuwekea muongozo.

Tambua, Tambua ewe mja wa Mwenyezi Mungu! Allah (sw) amekutaka uwe na tahadhari (na adhabu) kutoka kwake, hivyo usiiweke (nafsi yako) katika majuto, usijitie katika ghadhabu zake na kujitumbukiza katika mateso ya moto wa Jahannam, hakika mateso ya moto huo ni mabaya na yenye kudumu, hakika makaazi mabaya ya kukaa; hakuna kutoka nje, Macho hayapati usingizi, Roho haifi wala haiwi hai; (Humo watakuwa) katika Minyororo na pingu, wakiwa katika adhabu na adhabu ya mfano huo, basi yule ambaye ngozi yake itaungua yote, tutaibadilisha kwa ngozi nyingine, ili aonje kina cha mateso na adhabu; hakika Mwenyezi Mungu ni mtukufu na mjuzi mno, Moto, (ambao) moshi wake utawazunguka kote, hivyo kelele zao humo hazitasikika, maombi yao hayatajibiwa, na humo hakutakuwa na huruma kwa kilio chao.

Kimbia Ewe mja wa Mwenyezi Mungu, kwa Mola wako kupitia nafsi hii yenye kuamgamia, katika siku zijazo, na kwa siku zilizopita kabla mauti hayajakukumba, yakainyakua nafsi yako, yakatia dhiki moyo wako na (mauti) yawe baina yako na kurudi. Muda gani! Kwa hiyo hapatakuwa na njia ya kurudi na hakuna mkaazi ya kufikia. Allah (sw) akulinde wewe na mimi kwa kile alichowalinda marafiki zake wema, akuongoze wewe na mimi kwa kile alichowaongoza waja wake wema”.

 

 Khutba hii inawataka watu kutenda mema, na kuacha yaliyo haramishwa, na kujiepusha kupupia dunia inawahadharisha na Adhabu mbaya ya Mwenyezi Mungu (Al-Durr al-Nazim, p. 215).

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 16, 2016, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: