Mjue Ali Ridha (as) ~Imam wa Nane (8)

RezaShrine

Mjue Ali Ridha ~(as) Imam wa Nane (8) wa nyumba tukufu ya Mtume (saww)

Wiki hii Wapenzi watu wa nyumba tukufu ya Mtume (saww) na waislamu wote duniani wanasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ridha (A.S) mjukuu wa Mtume na Imamu wa nane (8) wa nyumba tukufu ya Mtume (Ahlulbayt).

Imam Ridha (as) alizaliwa tarehe 11 Mwezi wa dhul Qa`dah, 148 A.H, katika mji wa Madina.  Jina lake la kwanza akiitwa Ali na Abu al-Hassan ni jina lake la utani na Ridha ni jina lake kuonyesha utukufu wake. Imam alikuzwa na kilelewa chini ya uangalizi wa baba yake mpaka akawa kijana barobaro. Alipata faida ya mafunzo na maelekezo ya masomo kutoka kwa baba yake kwa muda wa miaka Thelathini na moja (31) mpaka baba yake alipochukuliwa na mtawala wa zama zake Harun Rashid na kumhamishia Baghdad kwa mateso na dhiki za ndani ya gereza kwa muda miaka mine (4) na hatimaye kufariki. Imam Ridha alikuwa na umri wa miaka 35 pale alipoteuliwa kuwa Imamu rasmi kwa amri ya baba yake mtukufu Imamu Musa Ibn Jafar.

Imam Ridha alibahatika kuona kipindi kifupi cha mwisho cha utawala wa Harun Rashid ambaye ndiye aliyemuua baba yake. Mtawala huyu Harun Rashid pia alijaribu kutaka kumuua Imam Ridha (a.s)  lakini hakufanikiwa. Baada ya kufa Harun mwanae Amin na Maamun wakapigana vita kugombea kurithi kiti cha utawala Maamun akamuua nduguye na kuibuka mshindi  na hatimaye kujitwalia kofia ya Ufalme na kujitangaza kuwa Khalifa wa dola ya kiislamu.

Mara tu baada ya kukalia kiti cha ukhalifa, Maamun kwa kufuata mila iliyowachwa na Muawiya alipaswa kumtaja mrithi wake wa kiti cha ukhalifa. Hapo Maamun akatuma ujumbe Imam Ridhaa aje makao makuu yake, Marwi, Maamun akatuma mjumbe Madina kwenda kumchukua Imam na akatoa maelekezo ya njia ya kupita na akatuma vikosi vya jeshi katika msafara huo. Njia aliyoichagua haiikuwa njia ya kawaida iliyozoeleka ambayo mashia wengi walikuwa wakiishi. Wakiwa tayari wamemchukua Imam, njiani msafara huo ulifika katika mji uitwao Nishapur. Hapo wanawazuoni na wasomi mbalimbali wa dini wakakusanyika na  na kumtaka Imam asimame walau dakika chache awafundishe hadith ya Mtume. Imam akawasomea hadithi maarufu iliyopewa jina “Mnyororo wa Dhahabu”  akisema…  Baba yangu Musa Al-Kazim amenisimulia mimi kutoka kwa baba yake Ja’far al-Sadiq kutoka kwa baba yake Mohammed Al-Baqir kutoka kwa baba yake Ali Zaynul Abedin kutoka kwa baba yake, shahidi wa Karbala kutoka kwa baba yake Ali ibn Abii Talib anasema: “Kipenzi changu na furaha ya jicho langu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameniambia mara moja, kuwa Jibrail alimwambia kutoka kwa mola wake mtukufu ” Tamko (kalima) LA ILAHA ILLALLAH  ni ngome yangu, yeyote atakayelitamka ataingia katika ngome yangu, na yeyote aingiaye katika ngome yangu ataokolewa na adhabu yangu.”

Vitabu vya historia vimebainisha kuwa wale wanahistoria walioiandika hadithi hii idadi yao inafikia elfu Ishirini.  Watu wakaanza kutamka Kalima wakati imamu alipounyanyua mkono wake  na kuendelea na safari  huku akisema “Ndio bila shaka Kalima ni ngome ya Mwenyezi Mungu. itakayokupa ulinzi sahihi lakini kwa sharti moja pekee nalo ni Ututii na kutufuata sisi Maimamu watoharifu katika Kizazi cha Mtume (saw)” Alipofika Marw, Maamun akamlazimisha imamu kukubali kuwa mrithi wake wa ukhalifa Imam akakubali shingo upande.

Kisha Mamun akafanya sherehe kubwa kusherehekea  tukio la Imam kukubali kuwa mrithi wake wa Ukhalifa. Katika hafla hiyo Imamu alitoa hotuba fupi sana akisema… “Baada ya kumhimidi Mwenyezi Mungu alisema “Sisi tunahaki juu yenu iliyoidhinishwa na Mtume, na nyinyi mna haki pia juu yetu; hivyo basi mkitekeleza wajibu wenu kwetu, tutalazimika kutekeleza wajibu wetu kwenu.”  

Kisha Mamun akaamrisha sarafu mpya ya fedha  ichongwe ikiwa na jina la Imam Ridha, Aidha Imamu alikuwa akijua hivi ni vitimbi tu na havitadumu muda mrefu. Baada ya muda mfupi vikaanza vitimbi, Maamun akanza kumfanyia ujasusi Imamu akimchunguza kila mwenendo wake. Badala yake Imamu akaitumia barabara fursa aliyopewa kusambaza mafunzo ya Uislamu sahihi na wa kweli. Ukumbi wa kasri ya Maamun ikawa inatembelewa na Maelfu ya watu na Imamu akawaathiri sana fikra zao. Hadith zake zikawa zinaandikwa kwa wingi. Maamun ambaye alikuwa mpenzi wa majadiliano ya kitaaluma alikuwa akialika na kupanga mijadala ya kielemu  na wataalamu na wanazuoni kutoka Ugiriki, Italia, India n.k wakija katika hekalu lake na kufanya majadiliano na Imam kwa lengo la kutaka kumuabisha Imam na kumdhalilisha mbele ya wanazuoni.

Siku moja mwanazuoni wa kiyahudi aliletwa na Maamun kujadiliana na Imam. Mwanazuoni huto akauliza: “Unawezaje kumkubali Muhammad ni mtume wa Mungu wakati hakuwahi kuonyesha miujiza yoyote?  Imam akamjibu muujiza mkubwa wa Mwenyezi Mungu ni Akili ya Mwanaadamu inakubali dhana kufikirika ndani yake na kutafakarika. Uislamu umesisitiza mno juu ya fikra ya Mwanaadamu. Watu wanapaswa kumkubali Mwenyezi Mungu kwa kutumia Fikra zao na sio kwa kupitia Miujiza.” Mwanazuoni huyo wa kiyahudi alikosa maneno ya kuzungumza baada ya jibu hilo.

Miongoni mwa Mafunzo ya Imamu pia alikuwa akisistiza zaidi juu ya umuhimu wa kumkumbuka kwa wingi Imam Hussein (as). Lakini wakati wote Maamuni hakuwa mkweli juu ya tabia yake kwa Imam. Alipoanza kuona utukufu na umaarufu wa Imamu ukiongezeka kila uchao, hilo likaanza kumsumbua na kumkasirisha hususan kwenye tukio ambalo alimtaka Imam kuongoza swala ya Iddi wakati yeye Maamun alipokuwa mgonjwa. Alijionea mwenyewe pale ambapo hata kabla Imamu hajafika Msikitini watu tayari walikuwa wamekwisha panga mistari mirefu njiani wakipiga Takbira na ilikuwa kama vile hata kuta zote za Marw zilikuwa zikipiga takbira, ilibidi amtaka imamu arudi nyumbani kwake siku hiyo.

Kuna taarifa tofauti tofauti zimeeelezea namna ambavyo Imama Ridha aliuwawa na Maamun. Moja kati ya taarifa hizo ni kuwa Imam alikuwa akipenda sana kula Zabibu na hivyo Maamuni akamletea zabibu zenye sumu. Imamu aliathiriwa sana na sumu na kuugua mahutihuti na baada ya siku mbili ikiwa ni Tarehe 29 Mwezi wa Safar 203 AH. Alipata shahada na kufariki. Imamu alikufa na kuacha Mtoto mmoja tu aliyekuja kurithi kiti chake na kuwa Imam wa Tisa (9) kwa jina Muhammad al-Taqi (a.s).

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 16, 2016, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: