JUKUMU LA WENYE DINI TANZANIA NA TUKIO LA KUPATWA JUA

150320072056-15-eclipse-0320-super-169

Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua. Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.

(Qur’an, Sura ya 36: aya 37-40).

Uislamu ni dini iliyojengwa juu ya Ya Imani na Msingi wa Kujisalimisha Kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa kila kitu. Kila muumini anayejiita Muislamu anapaswa kwenye kila jambo lake kumtanguliza Mwenyezi Mungu na kulifanya kwa ajili ya kutaka radhi zake, na hii ndio tofauti kuu kati ya Uislamu na Dini zingine.

Septemba Mosi mwaka huu kwa mara nyingi Mwenyezi mungu ameamua kudhihirisha moja ya Alama za Uwepo wake, na hapa kwetu alama hiyo amechagua itokee Mkoani Mbeya katika Wilaya ya Mbarali Kata ya Rujewa, Siku hii Alama ya Uwepo wa Mwenyezi Mungu itakayoshuhudiwa ni tukio la kupatwa Jua kipete.

Tofauti na inavyoripotiwa tukio hili sio tukio la Kisayansi bali ni tukio la KIMUNGU linaloweza kuelezewa kwa fani ya sayansi ya Anga. 

Tukio hili Mwenyezi Mungu anataka kuwathibitishia wale wenye Imani dhaifu kuwa, Mungu yupo na ni yeye pekee mwenye Nguvu na Mamlaka ya Mwisho ya udhibiti na muongozaji wa matukio yote Ulimwenguni.

Kupatwa kwa Jua kipete ni ishara ya Kimungu na alama ya wazi kwa Wanaadamu kutumia milango ya fahamu zao hususani Macho kuthibitisha kuwa hakuna mwenye uwezo kushinda uwezo wake, hakuna ambaye anaweza kubadili makadirio yake bali kubwa zaidi kila kitu ulimwenguni hufamyika kwa kutii amri na maamuzi yake.

Lakini taarifa hizi za kupatwa jua kipete… Wakati fulani katika historia ya Mwanaadamu iliaminiwa kuwa ni tukio la ajabu na kuhusishwa na ushirikiana na uchawi, Watu wakalihusisha tukio hilo na Majini na viumbe wengine.

Imesimuliwa kwamba kulikuwa na kupatwa jua wakati Ibrahim, mtoto wa Mtume (S) alipofariki akiwa mtoto mdogo. Watu wakaanza kusema kwamba Mtume (s) kumpoteza mtoto wake wa kiume ndio sababu ya jua kupatwa kipete. Katika jitihada za kusahihisha fikra sahihi na mawazo hayo Mtume wa Allah (saw) akapanda katika mimbari {minbar} na baada ya kumtukuza na kumhimidi Mwenyezi Mungu, alisema: “Enyi watu! jua na mwezi ni miongoni mwa ishara za Mwenyezi Mungu. Zinatembea katika mihimili yake kwa kwa amri yake na na vyote viwili ni dhalili kwake. Kupatwa Kwa jua au Mwezi hakutokani na kifo au maisha ya mtu yeyote. Hivyo, basi kama kutatokea Kupatwa jua, Swalini kwa Mola wenu. “Baada ya hotuba hii, akashuka kutoka kwenye mimbari na pamoja na watu wengine akaswali swala ya kupatwa jua.[1]

Tunapata mafunzo mawili katika Kisa hiki, Kwanza ni tendo la Mtume kuwashajiisha watu kufikiri sahihi juu ya Matukio yanayojiri kidunia yanayomkumba mwanaadamu na kuondokana na fikra mbovu na finyu kuwa yanayotokea ni Laana, Uchawi au mazingaombwe. Kisha  tendo la mtume kuambatanisha ibada ya Swala maalumu ni funzo kuwa Fikra pevu na Uelewa sahihi ni Mambo muhimu na ya awali kuliko hata swala yenyewe inayoswali bila kuwa na fikra sahihi na utambuzi yakinifu. Pili Kwa kuwa alikuwa ni mtume wa Mungu alitumia fursa hii adhimu kusema ukweli na kuwaongoza watu katika Haki na kweli, ambapo watu wadanganyifu na waovu kwao ingekuwa labda ni fursa yenye faida kuteka mawazo ya watu kwa ajili ya Maslahi binafsi. wangeanza kuchambua na kutafsiri tukio hilo la asili kwa ajili kujifaidisha tamaa zao za kibinafsi na kujipatia umaarufu.

Imamu Sadiq (as) amesema kwamba baba yake alisema: “Tetemeko la Ardhi, Kupatwa Jua na Mwezi, upepo mkali na wakutisha, ni miongoni mwa dalili za siku ya Ufufuo. Wakati wowote utakaposhuhudia matukio hayo, Tafakari kuhusiana na Siku ya Kiyama, kimbilieni katika Misikiti (nyumba za Ibada), na simameni katika kuswali (kumuomba Mungu).[2]

Duniani hivi sasa matukio ya sampuli hii yamebadilishiwa malengo na dhamira yake na kufanywa kuwa ni matukio ya kitalii na kiburudisho, watu wamehamasishwa kusafiri kwenda kuona tukio husika, Watalii mbalimbali wanamiminika kwa lengo la Kufurahisha Matamanio ya Nafsi zao, Taifa linategemea kupata fedha za kigeni kupitia Wizara ya Utalii… Hili sio jambo baya lakini sio jambo muhimu na dhumuni kuu la Muumba wetu kutuletea tukio husika. Watu watakapomaliza Kushuhudia tukio la kupatwa Jua kipete, Wakafurahi na kushangilia kwa kupiga mirusi na Mayowe, Serikali ikaingiza Madolari ya fedha, pindi tukio litakapokamilika na kwisha huo utakuwa ndio mwisho wa furaha hiyo na itabikia kuwa kumbukumbu tu basi isiyo na Mahusiano na Mungu muumba.

…Je walioshuhudia Watakuwa wameathirikaje Kiroho, na Imani zao kwa Mungu muumba?

Endapo lengo la safari yetu kulekea Ludewa Septemba mosi, litaishi kwenye furaha na Uchumi tu ni muhimu kutahadharisha hapa kuwa faida kuu na lengo la tukio la kupatwa jua litakuwa halikufikiwa na hilo linasababishwa na kasumba ile ile ya kale ya kulitizama tukio hili la Asili kwa mtizamo finyu na kulihusisha na Imani potofu na au Maslahi binafsi ya kidunia pekee yake, na kasumba hii inatokana na taifa letu kunakili kila lisemwalo na Mataifa ya Magharibi na hivyo tukio zima kuathiriwa na kutawaliwa na mitizamo ya Maisha ya Kimagharibi, maisha yaliyojengwa juu dhana ya Usekula ambao huamini kuwa Lengo kuu pekee la kuumbwa Mwanaadamu na Maisha haya ya dunia na Matukio yake ni kufurahisha hisia za Mwanaadamu na kuishi Maisha furaha hapa duniani.

Ama watu wa Mungu (God-ism) wenye Imani ya Dini na wenye kutambua uwepo wa Mungu tukio hili kwao ni nyongeza ya uthibitisho wa kimaumbile kuwa Mungu yupo na angali anamiliki nguvu kuu katika kuendesha dunia hii. Tukio hili huwaongezea Imani na kuwaogofya kumuasi Mungu wao kwa kujua uwezo mkubwa alionao. Tukio hili ni ukumbusho wa dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa na kuombwa msaada, kwani yeye pekee ndiye anayemiliki vyote vilivyopo mbinguni na Ardhini, Tukio hili ni Bishara kuwa kama alivyoumba Mbingu na Ardhi kwa uwezo wake, ni kw uwezo huo huo na tamko lile lile la kusema Kuwa na ikawa, basi hatuna budi kujiandaa kwa Maisha ya baadaye (Akhera) kwani ni tamko lake hilo hilo akipenda anaweza Siku ya Septemba Mosi akayamaliza Maisha haya ya duniani. Kwetu Watanzania wakati huu uwe ni wakati wa kuthibitisha maneno matukufu yaliopo katika vitabu vya Muumba wetu wetu pale aliposema… Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa (Mathayo 25:13)

Kila mtanzania kwa imani yake amuelekee Mola wake kwa Maombi na atubie dhambi zake katika wakati huu ambapo Mwenyezi Mungu amechangua kupitisha Moja ya alama zake ndani ya Taifa letu. Kwa waislamu dini yenu imeweka utaratibu kamili wa namna ya kuyapokea matukiao haya na huu hapa ndio muongozo wa Ibada maalumu ya kusaliwa siku ya tukio husika

UTARATIBU WA KUSALI SALATUL-AAYAT (wakati wa kutokea Matukio Makubwa ya Kiasili)

Sala ya Ayaat ni wajibu zama linapopatwa jua au mwezi, wakati wa mtetemeko na kimbunga na radi, na vizuko vingine vya mbinguni au ardhini.

 1. Utanuwia, hali ya kuwa umesimama na umeelekea Qibla: Nasali Salatul-Ayaat Rakaa mbili Qurbatan Ila llahi Taala.
 2. Utasoma sura ya Al-Hamdu na sura nyingine, kisha utarukuu.
 3. Utainuka kutoka katika rukuu; utasoma Al-Hamdu na sura nyingine, halafu utasoma Qunuti na utarukuu.
 4. Utainuka kutoka rukuu. Na utasoma AI-Hamdu na sura, na utarukuu:
 5. Utainuka kutoka rukuu, na utasoma Al-Hamdu na sura, halafu utasoma Qunut, na utarukuu.
 6. Utainuka kutoka rukuu, na utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.
 7. Utainuka kutoka rukuu, kisha utasujudu sijda mbili kisha utasimama kwa rakaa ya pili.
 8. Utasoma Al-Hamdu na sura, na utasoma Qunut, halafu utarukuu.
 9. Utainuka kutoka rukuu, utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.
 10. Utainuka kutoka rukuu, utasoma Al-Hamdu na sura, na utasoma Qunuut, na utarukuu.
 11. Utainuka kutoka rukuu, utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.
 12. Utainuka kutoka rukuu, utasoma Al -Hamdu na sura, na utasoma Qunuut na utarukuu.
 13. Baada ya hapo utainuka kutoka rukuu na kusujudu sijda mbili, na utasoma Tashaahhud na Salaam.

Itakuwa Sala ya Aayat ni rakaa mbili kwa Qunuut tano, na rukuu kumi, nasijda nne. Baadhi ya mambo muhimu ya kufahamu kuhusiana na Sala ya Ayat

 1. Kila lililo wajibu katika swala tano za kila siku ni wajibu pia kwenye Sala hii kama vile utakaso {taharah}, kibla, nk
 2. Kusali Salat al-Ayat ni wajibu wa haraka na ni lazima kujiepusha kuichelewesha. 
 3. Itakapotokea tukio la kupatwaa jua, mtu anaweza kusali mwanzo wa kupatwa. Kama mtu atashindwa kutekeleza sala hii atakuwa ametenda dhambi, na ni wajibu juu yake kwa muda wowote maadamu yupo hai wakati wowote aiswali Swala aliyoiacha.
 4. Kama tukio la Asili (Kupatwa jua, Mwezi au Tetemeko la Ardhi) litatokea katika mji, wakaazi wa mji huo ni lazima kwao kusali swalat Ayat lakini wale wa Maeneo mengine sio lazima.
 5. Haijalishi ni Aina gani ya kupatwa jua kipete iliyotokea Swalat Ayat ni wajibu kuswaliwa kwa aina yoyote itakayotokea (Iwe ni kupatwa kamili, nusu au mzingo mwekundu wa moto)
 [1] Wasa’il ash-Shi‘ah, vol. 5, p. 144.[2] Wasa’il ash-Shi‘ah, vol. 5, p. 145.

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 31, 2016, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: