Historia ya Kaburi la Imam Musa Kadhim (A.S.) na Imamu Muhammad Taqi  

Kadhmain hivi sasa

Makaburi ya Maimamu wawili Musa Kadhim na Imam Muhammad Taqi (as) yalivyo sasa hivi.

Yeyote anayetembele mji wa Baghdad akitokea upande wa Kazkazi atakumbana na Minara minne ya dhahabu afikapo eneo liitwalo Kadhmayn, hayo ni makaburi ya Maimamu wawili wa nyumba tukufu ya Mtume (saw) Imam Musa Kadhim (A.S.) na Imam Muhammad Taqi Jawad (A.S.) Hawa ni Maimamu watukufu Imam wa Saba (7) na wa Nane (8) kwa mfuatano kutoka Kwenye nyumba tukufu ya Mtume. 

Ni utamaduni wetu kuomba kupitia Makaburi hayo mawili kuomba kupata Tiba ya Maradhi yetu na kuomba wasila wao kwa Mwenyezi mungu kusamehewa Madhambi yetu na kutimia mahitaji yetu.

Staili ya ujenzi iliyopo sasa ya Makaburi hayo ni ya tangu karne ya  16 na imekuwa ikihifadhiwa vema na kuboreshwa na kubadilishwa kila zama. Majengo haya yanawakilisha  ukarabati uliofanywa na Shah lsmail I Safavi (1502-1524), japo sultani wa Uturuki, Suleman Mkuu, aliuteka mji wa Baghdad na kubakia hapo kwa miezi mine (4) mwaka 1534, alitembele makaburi haya matukufu na imesemekana alichangia sana katika kuboresha urembo wa makaburi hayo ya Kadhmayn.

Marumaru za guba mbili ziliwekwa mwaka 1796 na Shah Agha Muhammad Khan, ambaye alikuwa miongoni mwa mtawala wa kwanza wa Ufalme wa Qajar wa Iran mwaka 1870, Kisha Nasr-al-Din Shah akaja kuboresha Marumaaru zake za dhahabu katika moja ya kuba zake na minara yake. Inafurahisha kwani tarehe za Maboresho yote hayo zimechongwa ndani ya Marumaru na zinaonekana.

Kama tutakumbuka kuwa Maimamu hawa wawili waliozikwa hapa waliuwawa kishahidi mwanzoni mwa karne ya Nane (8), ni wazi basi imepita zaidi ya miaka 700 ya historia ya makaburi yao kusimuliwa, Maimamu hawa waliishi Miaka ya mwanzo kabisa ya Mji wa Baghdad, wakati ambao ukuta wa Mtawala Mansur uliokuwa umeuzunguka mji upande wa Magharibi wa Mto Tigris bado angali ulikuwa umesimama. 

Kuna Makaburi mengine upande wa Kaskazini Magharibi ambayo yalipewe majina mengi tofauti kama “Lango la Syria”, au “Abbassiya”, au “Lango la Nyasi”

Maimamu hawa wawili wamezikwa karibu kabisa na makaburi haya ya kale yaliopo upande wa Magharibi, lakini zama ambazo Yakubi aliandika, Mkoa mzima wa kaskazini ulifanywa kuwa Makaburi ya Makuraish.

Maimamu hawa wote walitiliwa Sumu kwa mpango uliofanywa na watawala wa Kikhalifa wa zama zao.

Lakini ni muhimu kuashiria hapa kuwa Mazishi ya Imam Muhammad Taqi, yaliongozwa na muakilishi wa familia ya Mfalme tukio ambalo bila pingamizi liliashiria utukufu wa Imam ambapo katika Kaburi lake aina fulani ya kuba ilijengwa.Hili litabakia ni kumbukumbu ya Historia juu ya Nafasi wqliyokuwa nayo Maimamu wetu kwenye kuathiri jamii zao japo zilitawaliwa na watawala waovu.

Lakini kuhusiana na umuhimu uliokuwepo hapo zamani kwa mtu kutembelea Makaburi haya Mawili, Taarifa tulizo nazo ni kutokana na mapokeo ya riwaya zilizopokelewa na Imamu wa Nane (8) na wa Kumi (10). Riwaya hizi hutoa Majibu kwani inasemekana zilinukuliwa wakati wafuasi wa Maimamu hao walipokuwa wakiuliza kuhusiana na Fadhila na Utukufu wa kufanya ziyara kwenda Kadhmayn.

Imesimuliwa kuwa Imam Ali Reza (A.S.), ambaye maisha yake huko Baghdad yalikuwa ni katika kipindi cha Khalifa Harun Rashid, Imamu alikuwa akiwaambi wafuasi wake Mashia Wampelekee Sala na salamu na kumtakia rehema baba yake Imam Musa al-Kadhim, na akiwaasa wasiache kufanya hivyo hata “Nje ya ukuta wa kaburi au msikiti ulio karibu”  kama mamlaka ya mtawala wa Kisunni yatakuwa makubwa na kuwazuia watu kufanya hivyo katika kaburi lenyewe. Kutokana na riwaya hii inaashiria kuwa aina fulani ya mjengo ulikuwepo katika makabuiri hayo zama hizo kuashiria kaburi la Imam Musa na lilikuwa limezungukwa na Ukuta.

Vile vile kauli kama hiyo pia imesemekana iliwahi kusemwa miaka michache baadaye na Imam Ali Naqi (A.S.), ambaye wakati wa Uimamu wake ulianza kipindi cha mwisho cha Ukhalifa wa Muutasim ambaye alijiingiza katika Anasa kubwa, mpaka kipindi cha machafuko dhidi yao na Mutazali chini ya Ukhalifa wa Mutawakkil. Maelezo haya ya kuzuru kaburi la Imam yametolewa na Majlisi.

Picha zinaonyesha historia ya Kaburi la Imam Muhammad Taqi huko Kazmain Iraq.

Kadhmain1Kadhmain2Kadhmain3Kadhmain4Kadhmain5Kadhmain6Kadhmain7

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on September 1, 2016, in Habari na Matukio and tagged , , , , , , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: