KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI MWAKA MPYA WA KIISLAMU NA KUMBUKUMBU YA IMAM HUSSEIN (a.s).

Muharram ni mwezi wa kwanza katika mwaka wa kiislamu, mwezi wa kwanza miongoni mwa miezi mitukufu ya kiislamu, Katika siku ya leo tunavuka mwaka na kuanza mwaka mpya kwa mujibu wa kalenda ya kiislamu.tumemaliza mwaka 1437H na tumeanza mwaka 1438H, Alhamdulilah mungu muweza ashukuriwe.

14536831_1315854905106316_1697953953_oTunatoa mkono wetu wa kheri na salamu za hongera kwa waumini wote duniani kufuatia mwaka mpya wa kiislamu, lakini pia tunatoa pole kwa waumini na binadamu wote kufuatia kumbukumbu ya huzuni kubwa ambayo iliikumba nyumba ya mtume wa uislamu, tukio la kusikitisha lililosababisha mauaji makubwa yaliyotekelezwa na mfalme dhalimu wa zama hizo dhidi ya ubindamu, Yazidi mwana wa Muawiya. Mauaji hayo ya kikatili yalifanywa katika mji wa Karbalaa nchini Iraq mwaka 61H, katika uwanja huo wa dhulma dhidi ya haki na ubinadamu hadi mtoto mchanga wa miezi sita hakusalimika, wanawake wanaonyonyesha waliteswa kwa kiu na panga za maadui zikashuka juu ya zile sauti za ukombozi, sauti zilizoinuliwa kudai uhuru wa ubinadamu, kudai haki na utumwa kwa binadamu ambae mola wake amemuumba huru tangu atoke katika tumbo la mama yake.

Katika mwezi huu tunakumbuka tukio la kuuwawa kikatili mjukuu wa mtume, tunahuzunika ili kujipa uwezo madhubuti kwa kulifanya tukio lile la kusikitisha liweze kuishi ndani mwetu, mwisho liweze kuibua chachu ya kupambambana na kila kilichokinyume na heshima ya mwanadamu kama vile Imam Hussein alivyopambana katika ule uwanja wa karbalaa, tuweze kuvuja jasho letu kwaajili ya kuitengeneza jamii na kuhakikisha14522016_1315854945106312_699026066_o

Dunia ya leo inawakumbuka watu wengi waliopita na viongozi wa zama zao kutokana na kazi zilizotukuka na huduma bora walizowahi kuwafanyia watu wao, mfano nchi yetu ya Tanzania inamkumbuka mwalimu Nyerere kwa kazi kubwa ya kupigania umoja wa kitaifa, kupinga ukabila na ubaguzi, watu wa jamii hii wanaomkumbuka Mwalim Nyerere wanapaswa kumkumbuka Zaidi Imam Hussein kwa sababu yeye hakupigania ubinadamu wa eneo lake pekee bali alipigania ubinadamu wa dunia nzima, alipigania uhuru wa watu wote waliokuwa wanavishwa utumwa wa minyororo ya kiitikadi iliyopelekea watu kutoheshimu utu na hata haki ndogo za binadamu. Ndio maana ukisoma unampata imam Hussein anasema :

Ikiwa ninyi hamna dini na hamuogopi siku ya malipo basi kuweni huru katika dunia yenu.

Tukio la Ashuraa na muhanga wa Imam Hussein ni tukio linalohusiana na swala la ubinadamu, tunapomkumbuka Imam Hussein na kumlilia, hatumkumbuki kama mtu aliyekufa au kuuwawa, laa hasha, Tunamkumbuka mtu ambae alikua anajambo kubwa analipigania, mtu ambae alilifia jambo kubwa la kuunusuru ubinadamu. Katika mafunzo tunayopata katika tukio la imam Hussein ni kama yafuatayo:

1. KUPINGA UUAJI WA WATU
Imam Hussein alitoka kuitengeneza jamii iliyokua imepoteza ustaarabu wake, jamii ambayo ilikua tayari inazidi kupoteza hata uelewa mdogo wa thamani ya mtu na mwanadamu, Imam alitoka ili kupinga umwagaji damu na kuuwawa watu pasi ya hati.

Katika maneno yake aliyokua akisema wakati akimpinga Yazidi dhalimu wa zama hizo alisema :

Hakika sisi ni watu wa nyumba ya utume, chimbuko la ujumbe (wa mungu), watu wa nyumba ambayo malaika wa mungu walikua wakipishana (kushusha ujumbe), chemchemu ya elimu na Yazidi ni mtu muovu, mlevi, mwenye kuuwa nafsi zisizo na hatia na mtu kama mimi (mwenye nafasi hii) hampi kiapo cha utii mtu kama Yazidi”.

Imam Hussein alikubali kufa kwaajili ya heshima ya utu, alikubali kuuwawa kwaajili ya kuunusuru ubinadamu, alikubali kufa na wanawe kuchinjwa kwa sababu ya kuutetea utu.
Leo Hii dunia inahitaji kuitikia wito wa Imam Hussein ili kuinusuru dunia iliyotapakaa damu kila kona, Katika Mashariki ya kati tunashuhudia watoto wanavyochinjwa na maelfu kukimbia makazi yao kwa sababu ya uharibifu, watu hawajasalimika hata katika nyumba za ibada kwani zingine zinakua makaburi ya waumini wake kwa milipuko ya mabomu na mirindimo ya risasi inayofanywa na maadui wa ubinadamu, Leo hii afrika yetu ya amani inashuhudia makundi ya kigaidi yanayojinasibisha na uislamu, makundi haya yanaua na kuteka hata wanawake, hakika hawa ndio wale akina Yazidi wa zama hizi ambao lau Imam Hussein angekuwepo angetoka kupambana nao ili kuunusuru ubinadamu.

2. KUPINGA UDHALILI
Imam Husein (a.s) katika kufunza thamani ya utu na heshima yake, aliamua kujitoa muhanga na kuelekea katika uwanja wa mapambano ili damu yake iweze kuandika historia ya ushindi, historia ya darasa juu ya kupinga udhalili na kukataa uovu. Darsa hilo liwe dira kwa kila kizazi kitakachokuja, wajue ya kwamba wanatakiwa kuipigania heshima yao, heshima ya mataifa yao, heshima ya kila mnyonge na kumnusuru anaedhulumiwa au kukandamizwa. Katika maneno yake maarufu Imam Hussein anasema:
“Hakika muovu mtoto wa muovu ametuweka baina ya machaguo mawili, baina ya kifo na udhalili na udhalili kwetu haukubaliki”.

3. KUDAI HAKI, MAADILI NA UHURU WA WATU.
Imam alikataa ukimya ndani ya ukandamizaji, akawafunza watu kunyamazia ukandamizaji ni aina ya kuukubali, hivyo ukimya katika unyonyaji, duluma na ukandamizaji ni aina nyingine ya ukandamizi, Imam akasema kuwaambia watu wa zama zake na hakika maneno yake haya ni kwa kila mtu
“Hivi hamuoni haki haifanyiwi kazi, na batili maovu hayakatazwi. Muumini anahaki ya kutamani kufa. Hakika mimi sioni kifo ila ni utukufu kwangu na kuishi na watu waovu isipokua upotevu”

Hivyo swala la Imam Hussein si swala la waislamu pekee, wala si swala la mashia au kundi la watu fulani bali ni swal la binadamu wote kwani Imam Hussein alitoka kupambana na kila uovu, Hakuna dini inayokubali udhalilishaji, unyonyaji wala dhuluma. Ndio maana mpigania uhuru wa taifa la Afrika ya kusini hayati Nelson Mandela aliwahi kusema:

Nimekaa zaidi ya miaka ishirini (20) gerezani,siku moja usiku nialimua kusalimu amri na kusaini nyaraka za makubaliano na serikali kwa kukubali kila sharti lao. Lakini ghafla nilikiri kuhusu imam Hussein na harakati za Karbalaa na Imam Hussein akanipa nguvu ya kusimamia haki ya uhuru na ukombozi”.

Tunatoa wito kwa watu wote Tanzania bila kujali tofauti za dini zao wala makabila yao juu ya kuhakikisha maswala ya kuboresha hali za jamii yanapewa kipaombele, kukataa kudhulumu, kuamrisha mema pamoja na kukemea maovu iwe ndio jadi yetu sisi watanzania, matendo ya kijambazi, ubakaji, uuaji wa walemavu wa ngozi na kila aina ya uharibifu tuukemee katika nchi yetu na kamwe tusiukabali. Tukifanya hivyo tuatakua tumefanikiwa kuitikia wito ule kibinadamu kutoka kwa Imam Hussein alipoomba watu wamnusuru na kumsaidia.

Sheikh Muhammad Abdi, Naibu wa Maulana Sheikh Hemedi Jalala.
Hawza Imam Swadiq (a.s),
S.L.P 67002,Dar es Salaam- Tanzania.
B.pepe: asadiqmedia@gmail.com
Tovuti: imamswadiq.com/

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on October 3, 2016, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: