KUMJUA ADUI (معرفة العدو)

Mwenyezi Mungu (sw) alipomuumba Adam (as) na kukamilika aliwaamuuru Malaika wote wamsujudie Adam, wakamsujudia sijida ya kumtukuza. Miongoni mwa hao malaika alikuwepo kiumbe (sio malaika) jina lake akiitwa Iblis, japo alisifika kwa uchamungu mkubwa akisujudu sana, Kurukuu na kumtaja zaidi Mwenyezi Mungu… Kiumbe huyu (Iblisi) Kwa kiburi na Kujiona alikataa kumsujudia Mwanaadamu na alikana Amri ya Mungu. Akidai yeye ni mbora zaidi ya Adamu.Hatimaye Ibilisi akalaaniwa na kufukuzwa.

kumjua-aduiLakini punde kabla ya kuondoka alimuomba Allah jambo moja akisema “Naomba unibakishe hai mpaka siku ya Mwisho (kiyama)

Allah (swt) alikubali maombi yake, na Iblis akachukua ahadi mbele za Mungu akimuahidi kwa kusema “Nitahakikisha nampoteza huyu Adamu na kizazi chake chote,nitakaa mbele yao, nyuma yao, kushotoni mwao na kuumeni mwao na kuwapoteza wote wasiione njia yako

Allah na yeye akamuhakikishia kuwa utaweza tu kufanya hivyo kwa wale watakao kufuata isipokuwa Waja wangu wema (hutaweza kuwapoteza)
Kisha Allah kwa kutambua hatari ya adui huyu kamueleza Adamu kuwa …Hakika huyu Iblisi ni Adui na wewe mfanye ni Adui.

MAFUNZO
1) Adui wa Adamu na wanawe wote ni Iblisi.
2) Sifa ya Adui na Jeshi lake
Ni wenye Kiburi na yale yenye kuambatana na ugonjwa wa Kiburi (Husda, Kupenda Ukubwa na Madaraka, Matamanio ya Nafsi, Kupenda Dunia, Chuki, Fitina, Uovu na Uasi, Matendo mabaya n.k)
3) Lengo la Adui
Kutimiza ahadi yake alompa mungu ya Kuwapoteza Mwanaadamu (Awe dhalili, Asimjue Mungu, Asahau wajibu wa kuamrisha Mema na kukataza maovu, Awe muasi na hatiye aingie Motoni)
4) Mbinu ya Mapambano

Adui anazuia njia ya haki kwa kuikalia mbele, nyuma, kulia na kushoto) Ikimaanisha sio Mara zote Iblisi yeye kupambana moja kwa moja (Hadharani) bali huwatumia Wasaidizi na Majemedari wake kupambana na Mwanaadamu.

KAMBI ZA MAPAMBANO

Mungu kusema huyu ni adui, mapambano yalianaza siku ile ile..katika mapambano hayo majeruhi na Wahanga ni wengi na itabakia hivyo mpaka siku ya kiyama.
Mambano yatakayobakia milele ni baina ya kambi mbili tu. Kambi ya Mwanadamu kamili na Kambi ya Iblisi

MIFANO YA MAPAMBANO HAYO KATIKA HISTORIA

Nabii Adamu na Mti alokatazwa kuukurubia

Mungu alipomuumna adamu na Mkewe Hawa alimpa kila kitu na kumpa Sharti afanye yote lakini mti fulani asiukurubie.(Huu ndio uliyokuwa uwanja wa mapambano) Nabii Adamu alipokubali ushawishi wa Iblisi na akaukurubia Mti alokatazwa, mapambano hapa hayakuwa ya Mti na Adamu la hasha…Bali yalikuwa ni baina yake na kambi ya Iblis na kambi ya Adamu. Kambi ya iblisi ikashinda na kuweza kumshawishi Nabii Adamu kuacha Maagizo ya Mungu.

Mauaji ya Habil na Qabili.

Kisa maarufu cha watoto wawili wa nabii Adam walipotoa dhabihu yao na mmoja Habili (Aliyekuwa Mwema na Mchamungu) ikapokelewa na Mungu na ya yule Qabil (Muovu, Hasidi Mwenye kibri) ikakataliwa.Muovu huyu akaamua kumuua ndugu yake. Na ikawa ndio Damu ya Shahidi wa kwanza anayeuwawa katika njia ya Mungu.Muhimu kuwelewa kuwa hapa Mapambo hayakuwa ya Habil na Qabili la hasha..Vita ilikuwa baina ya Habili (Mwanaadamu kabili na Mchamungu) na Iblisi hapa akimtumia tu ndugu Muovu Qaabili kama Mwanajeshi wake.

Mapambano baina ya Kambi ya Nabii Ibrahim na Nimrod.

Hayakuwa mapambano kati ya Ibrahim kama mtume na Mfalme Nimrod la hasha…
Yalikuwa ni mapambao baina ya kambi ya muwakilishi wa Mungu na mwanaadamu kamili (Ibrahimu) na Iblisi, katika uwanja huu wa vita Nimrod alikuwa ni kamanda tu wa Jeshi la Iblis.

Mapambano ya Nabii Musa na Firauni.

Ifahamike hayakuwa mapambano baina ya Nabii Mussa na mfalme Farao la hasha huu ni muendelezo tu wa mapambano yale yale ya ahadi ya Iblisi alichukua mbinguni, Mpambano huu ulikua baina ya kambi ya mwanaadamu kamili na mchamungu (Nabii Mussa na wafuasi wake wema) na kambi ya Iblisi. Isipokuwa katika uwanja huu wa Misri Farao ndiye aliyekuwa kamanda na jemedari wa vita akiwakilisha kambi ya Iblisi.

Na wengine walifuatia…Nabii Yusuf na Nduguze, Nabi Shuaibu na Wakazi wa mji wa Madyan, Yunus na mkasa wa kumezwa na Chewa ulotokana na watu wake wa Nainawa… Vyote hivi vilikuwa vita kati ya iblisi na Watu wa mungu
Na hata ilipofika zama za Mapambano baina ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Makuraishi.

Yalikuwa ni Mapambano baina ya kambi ya wacha Mungu, Binaadamu kamili na Iblisi ambaye Iblisi kwa eneo hili la Makka na Madina aliwakilishwa na Koo za kikurayshi kina abuu Jahl na wengine.

Je Mapambano haya yaliishia kwa Mitume tu!

Hapana… kumbuka ni Ahadi ya Ibilisi aliyochukua mpaka siku ya Kiyama
Kuuliwa Imam Ali kwa upanga na Maluuni Shimri lbn dhiljawshan ni mapambano baina ya Imam Ali na wafuasi wake na Iblisi. Kwa eneo hili la kuufa huko Iraq Iblisi alimchagua maluuni Abdurrahman ibn Muljim mmoja wa Majemedari wake amuakilishe kutenda jinai hii.

Ibn Muljim akamvizia Imam wakati akiswali aliposujudu akaunyanyua upanga wa Iblisi na kukipasua kichwa cha Imam na ikawa ndio sababu ya Kifo chake.
Lakini pia Mauaji ya kinyama ya Mjukuu wa Mtume, Imam Hussein (as) miaka michache sana baada ya kuuliwa kaka yake na Baba yake.

Imamu Hussein ambaye mtume anamsifia akisema “Hussein anatokana na mimi na mimi natokana na Hussein, Mwenye kumuudhi Hussein kaniudhi mimi na mwenyekumfurahisha kanifurahisha mimi”

Imamu Hussein aliuwawa na kukatwa kichwa chake na kisha kutundikwa katika mikuki na Wanawake wa nyumba ya Mtume wakavuliwa hijabu na kutembezwa Njiani Uchi… yeye na familia yake nzima huko Karbalaa (Iraq).

Mapambano haya hayakuwa kingine chochote isipokuwa ni mapambano ya Kambi zile zile mbili baina ya Kambi ya Mungu (ambayo hapa karbala iliwakilishwa na mjukuu wa mtume Imam hussein) na kambi ya Iblisi ambayo kamanda wake mkuu alikuwa maluuni Yazidi Mtoto wa maluuni laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na ukoo wao mzima.

Na kuthibitisha azma yao baada ya muaji haya wakaanza kushangilia na kujifakharisha kuwa wamefanikiwa kuzima dini ya Muhammad (s.a.a.w).(huu ni ushahidi kuwa wao shida yao haikuwa Hussein ila ni dini aliyonayo Hussein ambayo ni dini ile walioipinga tangu kwa Adamu na sasa Muhammad).

Wote hawa katika kambi ya Iblisi wamekula kiapo mbele za mungu kuwa watapambana na mwanaadamu mpaka wamtoe katika Njia.

Kila zama na kila sehemu mapambano haya yanaendelea. Yapo Mapambano ya vita vya Silaha..Tizama leo huko Yemeni, Bahrain, Iraq, Somalia Palestina. Mapambo yanaendelea. Watu wanauwawa kama wanyama bali zaidi ya wanyama.

Makundi ya Kikafiri na kigaidi yenye kumuabudu shetani yanachipuka kila uchao. Leo kuna ISIS, ISIL ALNUSRA FRONT, Jana yalikuwepo na hata leo yapo ya ALQAIDA, ALSHABAB, BOKOHARAMU na mengine mengi haya yote ni Kambi za Iblisi

Lakini sio vita vya silaha tu yapo MAPAMBANO YA VITA BARIDI (حرب الناعمة)

Vita vinapiganwa dhidi ya mwanadamu na kizazi cha mwanadamu kupitia mitandao ya Intanet na Apps za simu, Facebook, Twitter, Instagram, Telegram, Badoo n.k Picha za uchi zinasambazwa grupu moja kwenda jingine. Maovu yanasambazwa. Iblisi amekaa katika yetu Wanaaadamu badala ya kuamrisha Mwema na Kukataza maovu wanafanya kinyume chake.

Swali

Lakini Je! Allah (sw) alituacha bila kutupa uwezo wa kumshinda Iblisi… Je sisi hatuna mbinu za kumshinda Iblis.

Ni silaha gani alitumia Adamu, Ibrahimu, Mussa Muhammad na Hata imam Ali na Imam Hussein…. Leo Imam Hussein Analiliwa na dunia Nzima anatukuzwa na kuheshimiwa kila kona ya dunia yule muovu yazidi Hajulikani alipozikwa hakuna anayemkumbuka na analaaniwa na viumbe wote ni Silaha na mbinu gani alitumia imam hussein,
Kama alivyotufungua Allah akatubainishia Adui yetu… vivyo hivyo ametupa Mbinu, Uwezo na Maarifa ya Kumshinda iblis.

Kuwa pamoja nasi katika sehemu ya pili katika kuainisha mbinu za kumshinda Iblisi.
_______________________

DAMU YA HUSSEIN KARBALA NI UKUTA BAINA YA HAKI NA DHULUMA
AsadiqMedia,
Hawza Imam Swadiq (a.s),
Dar es Salaam –Tanzania.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on October 10, 2016, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: