Rambirambi kwa kifo cha Fatima

Rambirambi kwa kifo cha Fatima

Mtukufu Mtume alisema:

“Yeyote anayemuudhi (kimwili au kwa maneno) Fatima, ameniudhi mimi; na yeyote anayeniudhi mimi amemuudhi Mwenyezi Mungu na yeyote anayemuudhi Allah ametenda kufuru. O Fatima kukasirika kwako, ni ghadhabu za Allah Pia! Na kama wewe ni mwenye furaha, Allah pia hufurahi sana. ”

Fatima, binti pekee wa Mtume mtukufu wa Uislamu, alizaliwa katika mji wa Makkah tarehe 20 ya mwezi wa Jumadi al-Thani Mwaka 18 Kabla ya Hijira. Mwanamama mwenye heshima, mtukufu na mzuri Mama Khadijah na mumewe Mtume wa Allah (saw) walielekeza mapenzi yao yote, kumhudumia kipenzi chao na mtoto wao wa pekee Fatima, ambapo kwa upande wake Fatima alikuwa akiwapenda sana wazazi wake. Malkia huyu wa Nyumba ya Mtume alikuwa na akili sana, aliyetimia kila njanja na mwenye furahawakati wote. Mahubiri yake, mashairi na maneno yamebakia, ni hazina ya kumbukumbu ya nguvu ya tabia yake na heshima ya akili yake. Fadhila zake zilimpatia cheo cha “Mama mwenye nuru”.

Fatma alikuwa binti mrefu, mwembamba na amejaaliwa uzuri wa pekee, ambao ulisababisha apewe jina la “Al-Zahra” (Mwanamke mwenye nuru). Aliitwa al-Zahra ‘kwa sababu mwanga wake ulikuwa ukiangaza miongoni mwa wale walioko Mbinguni.

Baada ya kuwasili mji wa Madina, aliolewa na Ali, mwaka wa kwanza wa Hijira, na akajifungua watoto wawili wakiume na mabinti wawili. Watoto wake, Hasan, Hussein, Zeinab na Ummu Kulthum walijulikana kwa Uchamungu wao, wema na ukarimu wao. Nguvu zao za tabia na vitendo vyema vilibadili mwenendo wa historia.

Mtume Mtukufu alikuwa akisema, “Fatima ni amani ya moyo wangu”.

Kila siku asubuhi akiwa njiani kuelekea Msikitini, mtume alikuwa akipita nyumbani kwa Fatima na akimtolea salamu: “Amani iwe juu yenu enyi watu wa nyumba unabi na chanzo cha Utume”.

Fatima alikuwa Mwanamke maarufu na alitambulika kama “Kiongozi wa wanawake wote wa ulimwengu”. Mtume alikuwa kiigizo kamili kwa ajili ya wanaume, lakini hakuweza kuwa hivyo kwa wanawake. Kwani aya zote za Qur’an Tukufu zilizoshuka kwa wanawake, Fatima ni ndiye aliyekuwa kiigizo kamili, ambae alizifasiri aya hizo katika matendo. Katika maisha yake, alibakia kuwa mwanamke kamili, Binti, mke na mama kwa wakati mmoja.

Fatima alikuwa Binti mwenye ukarimu wa pekee sana; na hakuna hata mtu mmoja aliyefika katika mlango wake, na akatoka mikono mitupu. Kamwe hakuwahi kumuuliza Ali kwa kitu chochote katika maisha yake yote. Kama mama, yeye aliwatunza na kuwakuza watoto wa watukufu na wa pekee ambao baadae walizinyanyua alama utukufu wao juu ya uso wa dunia, ambapo hakuna zama zitaweza kufuta athari zao.

Kifo cha Mtume, kilimuathiri sana Fatima na kumsikitisha sana na alikumbwa na ukiwa mkubwa na kubakia akilia muda wake wote. Fatima alikufa katika umri wa ujana wake akiwa na umri wa miaka kumi na nane (18), na alizikwa kwa Siri sehemu isiyojulikana isipokuwa na Watu wachache walioshiriki Mazishi yake.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on March 2, 2017, in Habari na Matukio, Matukio and tagged , , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: