Historia fupi ya Maisha ya Bi Fatma

Kuzaliwa kwake

Fatima mtoto pekee wa Mtume wa Uislamu Muhammad (saw), alizaliwa Makkah tarehe 20 Jumada-than mwaka 8 kabla ya Hijira. Mama mtukufu Khadija na Mtume wa Mwenyezi Mungu walielekeza mapenzi yao ya dhati na kujitolea na ulinzi kwa kipenzi chao na Mwanao wa pekee Fatima, ambaye Mtoto huyo nae alikuwa na mapenzi ya pekee kwa wazazi wao.

Wasifu wake

Mwana huyu Malkia wa nyumba ya Mtume, alikuwa na akili kubwa sana aliyekamilika na mcheshi, Khutba, Semi zake na Mashairi yake yanabakia ni hazina na uthibitisho wa uwezo wake, tabia zake njema na utukufu wake na akili yake. Ni uchamungu wake uliompatia jina Al-zahraa (Ikimaanisha Binti Mwenye nuru). Fatima alikuwa binti Mrefu, Mwembamba na alikuwa na Urembo wa hali ya juu, ndio sababu akaitwa al-Zahraa (Binti Mwenye nuru). Aliitwa al-Zahra kwa sababu pia nuru yake ilikuwa ikiangaza hata kwa waliopo peponi.

Ndoa

Baada ya kuwasili Madina, alifunga ndoa na Ali, mwaka wa kwanza baada ya Hijra, Fatima alijaaliwa kupata watoto watatu wa kiume na wawili wakike. Watoto wake ni Hasan, Hussein, Zeinab na Umm Kulthum wote walijulikana kwa uchamungu wao, wema na upole. Tabia na mwenendo wa maadili yao ulibadili mwenendo wa historia.

Mtume mtukufu amesema “Fatima ni sehemu ya moyo wangu”. Alikuwa akitoka kwenda kumpokea binti yake kila alipokuwa akitoka katika nyumba ya mumewe. Kila alfajiri alipokuwa akielekea msikitini alikuwa akipita nyumbani kwa Fatima na kusema ”as-Salamu “alaykum ya ahli bayti n-nubuwwah wa ma dani r-risalah” (Amani ya ya mwenyezi Mungu iwe juu yenu watu wa nyumba ya Utume na chanzo cha Utume)

image-slider-eid-zehra2Mwanamke Bora kuliko wote

Fatima ni mwanamke maarufu na akitambulika kama “Sayyidatu nisa’i l-alamin” (Mwanamke bora wa duniani wakati wote) Mtume Muhammad ni mfano wa kuigwa kwa wanaume,  lakini Fatima ni mfano sahihi na kiigizo chema kwa wanawake. Kwani kwa Aya azote zilizoshuka za Quraan kwa wanawake, Fatima ndiye aliyekuwa kiigizo ambaye alizifasiri aya hizo na kuziweka katika matendo. Wakati wa maisha yake alikuwa ni mwanamke aliyekamilika, alikuwa binti, akawa mke na kisha akawa mama kwa wakati mmoja. Akiwa mtoto aliwapenda sana wazazi wake na akaweza kulishinda penzi lao kiasi kwamba ilifika wakati mtume akawa akimsimamia anapomkaribia. Kama mke alikuwa ni mwenye kujitolea. Hakuwahi kumlalamikia Ali kwa jambo lolote katika maisha yake. Na akiwa mama aliwalinda na kuwalea watoto bora kabisa ambao waliacha alama za utukufu wao katika sura ya dunia, ambapo hakuna zama zitaacha kuwakumbuka.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on March 20, 2017, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: