Lini alizaliwa Fatima Zahra?
Posted by Asadiq Media
Lini alizaliwa Fatima Zahra? |
Mkanganyiko wa wazi juu ya tarehe ya kuzaliwa Fatima ni jambo la kustajaabisha sana. Miongoni mwa kauli ni baadhi ya wanazuoni wanasema alizaliwa miaka mitano (5) baada ya kuanza kushuka Wahy, wakati wengine wanasema kuwa alizaliwa miaka Miwili au Mitatu kabla ya hapo, na bado wapo wale wanaosema alizaliwa miaka mitano (5) kabla ya kuanza kushuka Wahyi. Ni vema ifahamike hapa kuwa kauli ya kwanza imesimuliwa kutoka kwa Maimamu wa Ahlulbayt (a), kundi la wanazuoni wa kisunni pia wanaunga mkono mtizamo huu. Kwa upande wa pili ni wanazuoni wa kisunni na wapokezi wao wa hadithi pekee yao ndio wenye kuleta kauli hiyo ya pili. Zifuatazo ni hadithi zilizopokewa kuelezeaHistoria fupi ya Maisha ya Bi Fatma tarehe aliyozaliwa Fatima Zahra:
Maelezo hayo hapo juu ni baadhi ya sehemu za riwaya zilizopokewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlulbayt (a) na wanawazuoni wakongwe wa Kishia (Mwenyezi Mungu azihifadhi roho zao) zikianisha wazi kuwa kuzaliwa Fatima Zahraa kulitokea baada ya Kuanza kushuka Wahyi. Kinyume na riwaya hizi, Wanazuoni wa Kisuni wamesimulia yafuatayo;’
Huwenda utafiti zaidi ukifanywa utathibitisha kuwa Masunni pia wanao mtazamo huu huu karibu katika vitabu vyao vyote. Baada ya kuchunguza riwaya hizo hapo juu na tukiwa na mtizamo kuwa ni kweli kuwa Sio safari ya Miraj wala Kuanza kwa wahyi kulitokea kabla ya Utume, itabainika wazi basi kuwa uzao wa Bi Fatima Zahraa ulitokea baada ya kupewa utume. Hivyo basi ni wazi riwaya, zinazodai kuwa alizaliwa Miaka Mitano kabla ya kuanza wahyi wa kwanza ni riwaya dhaifu na zenye mapungufu.
(Mwengi tutayaweka wazi kwenye nukta hii pindi tutakapokuwa tukielezea ndoa ya Bi Fatima.) Hata hivyo, Tabari katika kitabu chake cha Dhakhaer al-Uqbi, Asfuri Shafe’i katika kitabu cha Nuzhat al-Majalis na Qanduzi katika kitabu cha Yanabea al-Mawaddah wamesimulia kuwa Bi Khadija (A.S.) anasema: “…Kisha, pindi (Fatima) uzao wake ulipokaribia, niliwaita wakunga wa kikurayshi kuja kunisaidia na walikataa kwasababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Wakati wa kumzaa, wanawake wane (4) ambao uzuri wao na kung’aa kwao hauelezeki waliingia katika nyumba’ “Mimi ni mama yako Hawaa” Wapili akasema: “Mimi ni Ummi Kulthum, Dada yake mtume Mussa” Watatu akasema: Pindi Khadija alipokaribia sana kujifungua, Aliwaomba wanawake wa Kikurayshi waje kumsaidia wakati wa kujifungu mwanawe. Walikataa na kusema: “Hatutakuja kukusaidia; kwasababu wewe umeolewa na Muhammad’ Mmoja wao akasema: “Mimi ni mama yako Hawaa” Wapili akasema: `Mimi ni Asiya Bint Muzahim.’ Watatu akasema: Wanne akasema: Mimi ni Mariam Mtoto wa Imran (Mama yake Nabii issa). Tumekuja kukusaidia ujifungue kisha ndipo Fatima akazaliwa. Wakati Fatima alipozaliwa na kugusa Ardhi, alikuwa katika umbile la kusujudu, na kidole akiwa amekinyanyua juu” Zaidi ya hapo, Riwaya iliyosimuliwa kwa kina imeyajwa na Mufaddal Ibn Amr kwa mapokezi ya Imam Swadiq (a) katika Juzuu ya 1 ya kitabu cha Bihar cha Al-Majlisi Riwaya hii pia imetajwa na Ibn Kathir katika Al-Bidayah wan-Nihayah. |
About Asadiq Media
Media for publicise the message of Wilaya under Imam SwadiqPosted on March 21, 2017, in Habari na Matukio and tagged Dar es Salaam, Fatima Zahraa, Hawaa, Khadija, Kumbukumbu ya kuzaliwa Fatma zahraa, Tanzania, Ummi kulthum, Wilada Zahraa. Bookmark the permalink. Leave a comment.
Leave a comment
Comments 0