Kwa nini aliitwa Fatima (as)

 

kwanini aliitwa Fatima
Kupewa jina kwa watoto mchanga waliozaliwa huchukuliwa kuwa ni msingi muhimu katika kanuni za dini. Kwani ni Mwenyezi Mungu pekee yake aliyempa jina Adam na Hawaa siku ya mwanzo tu alipowaumba, kisha akamfundisha Adamu majina yote.

Binaadamu pia wameendeleza utamaduni huu na kuutekeleza tangu hapo mwanzo. Kutoa jina kwa watoto ni kanuni ya watu wenye maendeleo.

Majina ya watu hutofautiana kutokana na nyakati na zama bali na lugha tofauti. Aidha pia lazima kuwepo uhusiano kati ya jina na maana yake; lakini hili mara nyingi haliakisi ukweli. Hivyo majina mengine yanaweza kupatikana kutoka vyanzo vingine visivyokuwa vya kilugha.

Hata hivyo, watetezi wa dini ya Mwenyezi Mungu juendelea kutoa umuhimu wa pekee kwenye suala la jina. Utamaduni huu una maana kubwa,  kwani binaadamu huitwa kwa jina lake, hivyo basi jina zuri au jina baya huaacha athari yake kwa mwenye nalo. Hakika kuna umuhimu mkubwa katika kuchagua jina zuri; ni muhimu hapa tukaashiria kuwa hata Mke wa Imran alipojifungua mtoto wake wa kike alisema;

“na nitampa jina la Mariam (Maria)”.

Zaidi ya hapo, Mwenyezi Mungu pekee yake ndiye aliyewachagulia majina Nabii Yahya (a) kabla hata mimba yake haijatungwa. Mwenyezi Mungu mtukufu anasema kuwa Zakaria, Baba yake Yahya alisema;

… “Basi nipe mrithi kutoka kwako. Atakaye nirithi mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Ewe Mola wangu Mlezi! Na umjaalie awe mwenye kuridhisha”

(Dua yake ikapokelewa na kujibiwa)

(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake..﴿ (19: 5-7)

Ni wazi pia katika kauli ya Mwenyezi mungu maneno “Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake;” inaashiria kuwa Mwenyezi Mungu (mtukufu) ndiye aliyekuwa akichukua nafazi ya wazazi na kutwaa majina ya waja wake wema, kama vile Mitume na maimamu.

Na hapa tutazame  kundi la hadithi zilizopokelewa zinazojadili na kuelezea kuhusu Fatima Zahraa, na sababu ya kupewa jina hilo; na hivyo tueleze kuwa kupewa jina hilo ilitokana na  umuhimu wa pekee na wala sio bahati nasibu, wala sio kwa kupendelewa jina hilo bali, kuna mahusiano makubwa kati ya jina na mwenyewe mwenye jina.
Imam Sadiq (A.S.) anasema:  Jina la Fatima lina majina mengine Tisa (9) mbele ya Mwenyezi Mungu (Mtukufu), Majina hayo ni Fatima, Siddiqah (Mkweli), Al-Mubarakah (Mwenye kubarikiwa), At-Tahirah (Aliyetakaswa), Az-Zakiyah (Msafi), Ar-Radhiatul Mardhiah (Mwenye shukran, mwenye kuridhia), Al-Muhaddathah (mtu asiyekuwa Mtume ambaye Malaika huongea nae), and Az-Zahra (the Maridadi).”

  1. Imesimuliwa kutoka katika Bihar, Juz. 10, 1 kuwa Imam Abu Ja’far Al-Baqir (as) amesema: “Wakati Fatma alipozaliwa Mwenyezi Mungu (Mtukufu) alimteremsha Malaika kulitaja jina la Fatima kwa ulimi wa Mtume Muhammad. Mwenyezi Mungu akasema; “Hakika mimi nimekupa maarifa wewe, na kukulinda kutokana na hedhi.”
    Kisha Abu Ja’far (as) akaongeza: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu mtukufu Allaha alimpa elimu yeye (Fatima) na akamkinga na Hedhi kwa agano hilo.”
  2. Imam Ar-Ridha’ na  Imam Jawad (as) Wanasema: “Tulimsikia Maamun akisimulia kutoka kwa Rashid kutoka kwa Mahdi kutoka kwa Mansur kutoka kwa Baba yake kutoka kwa babu yake kuwa Ibn Abbas alimwambia Muawiya kwa: ‘Unafahamu kwanini Fatima alipewa hilo jina?’ Akajibu: Sifahamu.’ Ibn Abbas akasema: ‘Kwasababu yeye na wafuasi wake wamekingwa na Moto wa Jahannam, nimemsikia mtume wa Mwenyezi Mungu akisema hivyo.’
  3. Imam Ar-Ridha’, akinukuu kutoka kwa Baba zake amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: ‘O Fatima unajua kwanini ulipewa jina hili la Fatima?’ ‘Ali (as) akauliza: ’Kwanini alipewa jina hilo la Fatima? Akajibu mtume: Kwasababu yeye (Fatima Zahraa) na wafuasi wake (Mashia) wamekingwa na Moto wa Jahannam”
  4. Imam Sadiq (as) amesema: “Unafahamu tafsiri ya (jina) Fatima? Nikasema: Nifahamishe ewe bwana wangu. Akasema: `Amekingwa na Maovu.’ Kisha akaongeza zaidi: Laiti Amirul Muumin asingelimuoa yeye, hakuna mwanaume katika dunia tangu Adam angekuwa stahiki kwake mpaka siku ya kufufuliwa”

Riwaya hizi pia zimesimuliwa na kundi la Wanazuoni wa Kisunni, miongoni mwao ni Ibn Shirooyah Ad-Dailami ambaye anasema: “Um Salamah alisema: ‘Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Laiti Allah asingelimuumba Ali (as) hakungekuwepo wa kumfaa Fatima

Zaidi Ad-Dailami, Khawarazmi katika Al-Manaqib, Munawi katika Kunz al-Haqaeq, na Qandouzi katika Yanabea al-Mawaddah wamesimulia hadithi hii kwa nukuu ya Um Salamah na Al-Abbas, Mjomba wake mtume.

  1. Kharghoushi na Ibn Batta wamesimulia katika vitabu vyao Sharaf An-Nabi na Ibaneh kwamba Imam Sadiq (as) alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwambia ‘Ali (as) `Unafahamu sababu kwanini Fatima alipewa jina hilo?‘Ali (as) akauliza: Kwanini alipewa jina hilo. Mtume akajibu: Kwasababu yeye [Fatima Zahra],  na wafuasi wake (Mashia) wamekingwa  na moto.”
  2. Imam Ar-Ridha’ (as) amesema; kuwa baba yake alimnukuu Amirul-Mu’mineen (as) akisema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema Fatima alipewa hilo jina kwasababu Allah amemkinga yeye na kizazi chake na Moto; wa;e ambao watafika mwa Mwenyezi Mungu wakiwa na Imani ya Tawhid na wenye kuamini ninayoyafundisha

Rejea:

Fatima [‘a] The Gracious. By Abu Muhammad Ordoni. Sura ya 7. Chapa ya: Ansariyan,Qum, The Islamic Republic of Iran.

Bihar: v.10.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on March 22, 2017, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: