HUU NI MWEZI MTUKUFU WA RAJAB

Rajabu ni mwezi wa Saba (7) katika kalenda ya Kiislamu. Mwezi mtukufu wa Rajabu ni moja ya miezi mine (4) mitukufu. Mwezi huu na mwezi unaofuata wa Shaban na mwezi mtukufu wa Ramadhani ndio Miezi mikuu na mitukufu kwa mwaka mzima.

Ipo hadith isemayo kuwa Mwezi wa Rajabu ni Mwezi wa Mwenyezi Mungu na Shabani ni Mwezi wa Mtume mtukufu (saw) na mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Ummah wa Kiislamu.

Pia mwezi huu unatangulia mwezi wa Ramadhani, Kwasababu Ramadhani hufuatia baada ya kuingia Mwezi wa Shaban, hivyo basi pindi mwezi muandamo wa Rajab (Mwezi wa Saba wa Kalenda ya kiislamu) utakapoandama, mtume wa Allah (sw) alikuwa aghalabu akisoma dua hii:

“Oh Mwenyezi Mungu! tupe baraka katika miezi ya Rajab na Shaaban na utufikishe katika mwezi wa Ramadhani.”

Imam Musa Al- Kadhim, Imamu wa Saba (7) anasema: “Rajabu ni mwezi mtukufu, ambao Allah huongeza mara dufu thawabu kwa Mwema  na kufuta madhambi”

Matendo matukufu ya Ibada ndani ya Mwezi wa Rajabu:

1.   Kufunga

Imekokotezwa sana kufunga katika mwezi huu wa Rajab angalau mara moja kwa uchache. Riwaya iliyopokelewa kutoka kwa mtume (saw) Yeyote atakayefunga siku moja katika mwezi wa Rajabu, Moto wa Jahannamu utawekwa mbali nay eye umbali wa masafa ya safari  ya Mwaka mmoja, na ambaye atakayefunga siku tatu (3) katika mwezi wa rajabu, pepo ni stahiki yake”

Imam Ali (as) alikuwa mara zote akifunga mwezi wote wa Rajabu, na wafuasi wake wengi pia walikuwa wakifanya hivyo.

2.   Kuomba Msamaha (Istighfaar)

Mtume Mtukufu (saw) alikuwa akisema; “Rajabu ni mwezi wa kuomba toba, hivyo ombeni toba kwa Mola wenu, Hakika yeye ni mwenye kusamehe mwingi wa kurehemu. aidha imekokotezwa sana kusema ‘Astaghfirullah’ mara nyingi” ndani ya mwezi wa Rajabu.

3. Kutoa Sadaka (Sadaqa)
Yapo malipo makubwa kwa mwenye kutoa Sadaka ndani ya mwezi huu wa Rajabu. Wale ambao hawawezi kufunga wanaweza kutoa Sadaka kwa kuwapa masikini kila siku.

4. Rudia mara kwa Mara kusema  ‘Laa ilaaha illa-Allah’  mara 1,000.

5. Rudia mara kwa mara kusema ‘Astaghfirullaaha dhul jalale wal Ikraam min jamii’ dhunubi  wal aathaam mara 1000. Ili kuweza kuingia katika Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa nidhamu kubwa mtu anapaswa kuanza maandalizi katika mwezi wa Rajabu na Shaban.

Imesemwa  Rajab ni mwezi wa kupanda mbegu njema kwa kufanya matendo mema, Shaabani ni mwezi wa kuzimwagilia  mbegu hizo na Ramadhani ni mwezi wa kuvuna.

Imam Jafar Al-Sadiq (as) aghalabu ndani ya mwezi wa Rajabu alikuwa akisoma dua hii kila siku baada ya swala ya Asubuhi na Magraribi; Oh yule ambaye kwake ninaomba na kutarajia malipo ya matendo mema (niyatendayo); na kwake ambaye ninaomba Amani kwa hasira zake kwa kila ovu nilitendalo!

Ewe ambaye hutoa malipo makubwa kwa (Mema) machache! O yule ambaye huweka katika mkono wa muombaji kile alichoomba, Eeh yule ambaye hukidhi haja , kw ahata asiyeomba humkidhia haja yake bila kuiomba, japo humkumbuki (mola wake) anajisikia huruma, na kuchukua huruma juu yao. Nakuomba unipe zawadi njema kwa kila lengo langu katika ulimwengu huu na kesho Akhera, niwezeshe nijitenge na Maovu katika matendo yangu katika ulimwengu huu  na kesho Akhera, kwani hakika ukitoacho hakipotei bure wala mbegu yake haozi, Kutoka katika hazina ya miliki yako nizidishie Zaidi na Zaidi Ewe mkarimu mwenye kurehemu.

Tunamuomba Mwenyezi mungu mtukufu, Awabariki katika mwezi huu mtukufu na kila mwezi na awawezeshe  kuzidi kutenda mema kwa ajili ya kesho Akhera.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on March 29, 2017, in Matukio and tagged , , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: