Kupatwa kwa Mwezi na Wajibu wa Swala ya Alama (Salat al-Ayat)

Na abuuzahraa.

Baadhi ya Matukio ya asili yana sifa zinazofanana ambazo aghalabu huwa ni kuogofya, na nyakati zingine husababisha Imani za kishirikina kwenye akili za watu wasiojua au wasio namazingatio na hata matambiko ya kimila.

Ni jukumu la dini ya Asili na itokayo kwa Mwenyezi mungu, kusahihisha fikra hizo potofu za kiakili na kuzipeleka akili za watu kuelewa chanzo sahihi kinachosababisha matukio hayo ya kiasili.

Dini ya Uislamu imefaradhishwa Ibada maalumu ya swala kwa ajili ya matukio hayo ya Asili, ili kuelekeza fikra na mawazo ya Wanaadamu kwa Mola muumba wa Ulimwengu, na kuzitambua nguvu zake ndio sababu kuu ya mabadiliko na matukio hayo.

Swala hii inaitwa Swala ya Alama (Salat al-Ayat) kwa sababu huswaliwa nyakati ambazo hutokeo matukio ya asili ambayo ni alama za Kimungu na alama katika dunia.

Tunasoma katika vitabu vya Fiqh na sharia kuwa Sala ya Alama ni Wajibu kunapotokea matukio ya kiasili yafuatayo;

(1) Kupatwa kwa Jua {kusuf};
(2) kupatwa kwa Mwezi{khusuf};
(3) Tetemeko la Ardhi, na
(4) Radi na Mwangaza wake (thunder and lightning,) na upepo mweusi na mwekundu (black and red winds) ambazo huogopesha watu wengi. 

Swala ya Alama funzo la Tawhidi
Baadhi ya watu wenye upungufu wa maarifa wamekuwa wakiyachukulia matukio haya ya kiasili kama alama ya Balaa, Nuksi, au hasira ya Miungu yao. Kwa kukosa ufahamu wa mambo kuhusiana na Asili ya mambo na Sababu ya kutokea matukio hayo, kumewafanya kutomzingatia Mwenyezi mungu na badala yake wamekuwa wakitafuta chanzo cha matukio hayo na kukinasibisha na Nguvu za giza au vitu visivyo na uhai au Maada. Hususani wenye kuabudu Jua na Mwezi wanazo fikra zao za kishirikiana kuhusiana na matukio husika.

Kuiswali swala hii ya Alama imekokotezwa ili kuzielekeza fahamu na akili za wanaadamu kwenye chanzo cha kweli na cha Asili cha uumbaji na mabadiliko ya Asili, ambacho sio kingine isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Bila shaka pia Swala hii hutoa funzo sahihi juu ya upweke (Tawhid) wa Mwenyezi Mungu. 

Imepokewa kuwa ilitokea kupatwa kwa jua wakati Ibrahim, mtoto wa Mtume (saww) alipofariki akiwa mtoto mdogo. Watu wakaanza kusema mtume kupoteza mtoto wa kiume ndio sababu ya tukio la kupatwa kwa jua.
Katika juhudi za kusahihisha fikra hizo potofu na dhana hiyo mbaya, mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akapanda juu ya Mimbar msikitini na baada ya kumhimidi Mwenyezi Mungu akasema: O enyi watu! Jua na Mwezi ni miongoni mwa Alama za Mwenyezi MunguViwili hivyo hutembea katika njia yake nyofu kwa Amri yake, na vyote humyenyekea yeye, Kupatwa jua/Mwezi sio kwa sababu ya kifo au Maisha ya yeyote. Hivyo basi pindi kutakapotokea Kupatwa jua au mwezi basi swali swala (ya Alama). 

Baada ya hotuba hiyo mtume akashuka kwenye Mimbar naye pamoja na Watu waliokuwemo msikitini wakaswali swala kwa ajili ya kupatwa jua.[1][614]

Tunapata mafunzo mawili kwa tabia hii aliyoonyesha mtume (s), Kwanza ni fikra na ufahamu sahihi wa matukio ya Asili na kisha Kuswali swala ya Alama. Humaanisha kuwa  Uelewa sahihi na na fikra sahihi ni muhimu kwanza kabla ya Ibada yenyewe ya swala.

Funzo lingine, kwa kuwa Mtume alikuwa mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wa haki, alizungumza kweli na kuwaita watu waelekee kwa Mola wa kweli. Kinyume chake, Wapotoshaji na waabudu masanamu na washirikina, huenda wakaitumia fursa hiyo kwa maslahi yao binafsi na kuwavutia watu kwao. Wakatafsiri na kufafanua hata matukio ya Asili ya kidunia kwa matanio yao binafsi. 

Imam as-Sadiq (as) anasimulia kuwa baba yake alisema; Matetemeko ya Ardhi, Kupatwa Jua na Mwezi, Upepo mkali wa kutisha, ni miongoni mwa Alama za siku ya Kukufuliwa, kimbilieni kujilinda na matukio hayo misikitini na simameni kuswali.

Hadithi hii pia imekusudiwa kupeleka mazingatio ya watu kutoka kwenye Asili kwenda kwa Mola mwenye kuzisababisha Asili hizo, na hatimaye Asili hii itokayo kwa Mungu hukamilishwa kwa Ibada ya swala ya Alama.

Utaratibu wa kuiswali swala ya alama.

Tutaashiria baadhi tu ya taratibu za kuiswali swala ya Alama na kwa mwenye kuhitaji kwa kina atarejea vitabu vya Fiqh na Sharia.

1. Swala ya Alama ina rakaa mbili (2) (kama swala ya Subhi). Na katika kila rakaa ina rukuu (kuinama) mara nne (4). 

Katika kila rakaa baada ya kusoma suratul Fatiha (Alhamdu) na sura nyingine katika Quraan, atarukuu (na atasema kama asemavyo katika swala zingine) kisha atainuka (itidal) na atasoma tena Sura fatiha (alhamdu) na sura nyingine katika Quraan, na kisha atarukuu tena, na ataendelea kufanya hivyo mara tano. Katika kila rakaa baada ya kusoma sura Fatiha (Alhamdu) mtu anaweza kuigawanya hiyo sura nyingine katika vigawanyo vitano na kusoma sehemu ya kigawanyo husika kabla ya rukuu na aendelee kufanya hivyo mara tano.  

2. Yale yote yaliyowajibu kwa swala ya faradhi kama vile Twahara, kuelekea Kibla, n.k pia ni wajibu kwenye swala hii ya Alama. 
3. Kuswaliwa swala hii ya Alama ni wajibu wa dharura na haipaswi kucheleweshwa. Kwa tukio la kupatwa Jua au Mwezi, inaweza kuswaliwa mwanzo mwa kupatwa Jua/Mwezi . 

Kama mtu ataacha kuiswali swala hii ya alama linapotokea tukio la Asili basi ajue anapata dhambi na itaendelea kuwa ni wajibu kwake kuiswali maadamu atabakia hai kwa maisha yake yote. 

4. Kama tukio la Asili linalowajibisha kuswali swala ya Alama limetokea katika mji fulani, ni wajibu kwa wakaazi wa eneo hilo kuswali swala ya alama na kwa wengine waliopo nje ya mji huo sio lazima. 

5. Haijalishi kupatwa kwenyewe kulikotokea kuwe ni sehemu (nusu) au nzima (kamili) haibadilishi chochote kaa hali zote mbili hizo swala ya Alama ni lazima kuswaliwa. 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 7, 2017, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: