Siku hadi Siku za Ibada ya Hijja

lvl220121009053224

Siku ya Kwanza: Siku ya 8 ya Dhul-Hijjah

Siku ya nane ya Dhul-Hijjah (Yawm Tarwiyah), Hujaji anavaa Ihraam yake baada ya swala ya Dhuhr & Asr na kutoka Makkah kwenda Mina. Anatumia muda wote wa mchana na usiku akiwa huko Mina Kwa ibada na swala, akijitayarisha kwenda Arafa.

Siku ya pili: Siku ya 9 ya Dhul-Hijjah

Siku ya tisa ya Dhul-Hijjah (Yawm Arafa), baada ya sala ya al-Fajr huko Mina, Hujaji anasubiri hadi muda kidogo baada ya jua kuchomoza, kisha anatoka nje ya mji wa Mina kwenda kwenye viwanja vya Arafa ambapo anapaswa kuingia hapo Arafa mchana. Akiwa Arafa ataswali Sala ya Dhuhr na Asr pamoja kwa Adhana moja na Iqama mbili wakati wa mwanzo wa muda wa Zuhr (Kwa maneno mengine ataunganisha Swala ya Dhuhri na Alasiri).

Hujaji anapaswa kusubiri huko Arafa mpaka muda mfupi baada ya kuzama kwa jua (takriban dakika 10 baada ya kuzama kwa jua), halafu atatoka kuelekea Mash’ar au Muzdalifa (eneo kati ya Arafaat na Mina). Ataahirisha swala ya maghribi na Isha huko Arafaat ili kwenda kuziswali kwa pamoja huko Mash’ar kwa Adhana moja na Iqama mbili, (Ataunganisha Maghrib na Isha) kisha atautumia muda wote usiku katika sala na usingizi. Aidha Hujaji akiwa hapo Muzdalifa anapaswa kuchukua/Kuokota vijiwe vingi zaidi ya idadi ya vijiwe (21) vinavyohitajika ili baadaye siku inayofuata akavitupe kupiga shetani Jamaraats huko Mina.

Siku ya Tatu: Siku ya 10 ya Dhul-Hijjah

Siku hii inajulikana kama Eidul Adha / Yawm Nahr. Hujaji anapaswa kuswali swala ya al-Fajr hapo Muzdalifa, kisha kuondoka Muzdalifa kwenda Mina muda mfupi baada ya jua kuchomoza. Na kisha  kuelekea kupiga mawe ilipo Jamrah Al-Aqabah (Shetani mkubwa), kisha Jamrah Al-Ula (Shetani wa mwanzo) na mwisho Jamara Al-Wusta (Shetani wa kati). Anapopiga kila jiwe kwenye Jamaraat hizi anapaswa kusema Allahu Akbar.

Baada ya kukamilisha ibada ya kupiga mawe, Hujaji anapaswa kwenda mahali ambako wanyama huhifadhiwa na kuchinja mnyama (Qurbani / Kutoa sadaka). Kisha aelekee kwenye kukata kucha (Taqseer) au kunyoa nywele za kichwani (Halaq). Baada ya hapo, ataanza safari ya kuelekea mji wa Makka kwa ajili ya Matendo ya ibada ya Makka (Amaal Makkah), ambayo yanajumuisha Tawaaf ya Hijja / Tawaafu Ziyara, Swala ya Sunnah ya Tawaf (Salaat Al-Tawaaf) na Sayee. (Kutembea matiti baina ya vilima viwili Safa na marwa) Kisha hujaji atakamilisha kwa Tawaaf-Un-Nisa na Swala yake na baada ya hapo atavua Ihraam yake.

Siku ya nne: Siku ya 11 ya Dhul-Hijjah

Siku hii Hujaji atafanya tendo la Ramy Jamaraats huko Mina. Vijiwe vinavyopiga Shetani vinapaswa kutupwa kwenye Jamaraat kwa mfuatano na nidhamu iliowekwa, yaani, kuanzia shetani lile la mwanzo unapotoka upande wa Mina kwenda Makkah liitwalo Al-Jamrah Al-Ula, kisha linalofuatia liitwalo Al-Jamrah Al-Wusta na mwisho lililopo karibu na Makkah liitwalo Al-Jamrah Al-Aqabah. Na Hujaji anapaswa kuupitisha usiku huo mjini Mina. Si lazima kuwa huko usiku wote.

Siku ya Tano: Siku ya 12 ya Dhul-Hijjah

Hujaji atafanya matendo kama alivyofanya siku ya 11 ya Dhul-Hijjah.

Siku ya Sita: Siku ya 13 ya Dhul-Hijjah.

Vijiwe vinavyopiga Shetani vinapaswa kutupwa kwenye Jamaraat mfuatano uliowekwa, yaani, kuanzia shetani lile la mwanzo unapotoka kwa Mina kwenda Makkah liitwalo Al-Jamrah Al-Ula, kisha linalofuatia liitwalo Al-Jamrah Al-Wusta na mwisho lililopo karibu na Makkah liitwalo Al-Jamrah Al-Aqabah. Na Hujaji sasa anaweza kuondoka kuelekea Makka mara moja kwa ajili ya Tawafu ya kuaga (Tawafuu-ul-Widaa) na Swala yake ya Sunna.

 

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 25, 2017, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: