SHEIKH JALALA, ASKOFU BANZA WAFANYA UZINDUZI -MUHARRAM 2017

Mapema leo Maulana Sheikh hemedi Jalala kiongozi mkuu wa huduma za kidini na

maulana press-01kijamii zinazotelwa chini ya usimamizi wa Imam Swadiq a.s akiwa na Askofu Reverence Banza wa Tanzania Austrich Ministry pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo Mh

 

. Nguogani ametambulisha miradi ya kijamii inayolengwa kufanywa katika siku hizi za kumbukumbu ya Imam Hussein.

Maulana Sheikh Hemedi Jalala ametambulisha utoaji wa damu salama na kuhimiza watu kujitokeza kuunga mkono zoezi hilo kwaajili ya kusaidia wagonjwa wetu na kila wenye uhitaji wa damu katika hospitali zetu nchini, Tukio hilo linafanywa na waumini pamoja na wadau mbalimbali ili kuenzi damu za mashahidi zilizomwagwa katika ardhi ya Karbalaa wakiwa wanatetea haki na ubinadamu, Sambamba na zoezi hilo kuna ugawaji wa maji katika maeneo mbalimbali, kutembelea vituo vya mayatima, kupanda miti na kutembelea magereza za watoto ili kukaa nao na kuwanasihi juu ya maadili mema.

Maulana Sheikh Hemedi jalala katika uzinduzi na utambulisho huo alisema: “Ndugu zangu na watanzania wenzangu amani ya Mungu iwe juu yenu! napenda nianze mazungumzo yangu kwa maneno matakatifu ya mtume Muhammad s.a.w.w yanayosema  “Wanaohurumiana huwa Mungu anawahurumia, wahurumieni wote

IMG_3123

walioko duniani wanatawahurumieni wote walioko mbinguni”.Haya ni maelekezo ya di ni ya uislamu, ni maelekezo ambayo siku hii ya leo sisi kama waislamu na hususan wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbayt au Mashia duiniani huwa tunakumbuka mauaji ya imam Hussein (ambae) ni mjukuu wa mtume Muhammad  s.a.w.w , Imam Hussein moja ya sababu yake ya msingi ya kukubali yeye afe ni ili watu wapendane na wahurumiane,alikua kwenye kipindi ambacho mapenzi na mahabba yalikua yamekosekana katika jamii“.

Maulana Sheikh Jalala aliendelea kusema “ufunguzi mnaouona, tendo la kugawa maji na programu nyingi zinazofanyika zote ni katika kurudisha huruma na upendo kwa jamii ya wanaadamu“.

Banza-01Kwa upande wake Askofu Reverend Banza Suleiman mwenyekiti na askofu wa kanisa la Tanzania Austrich Ministry  amesema kuwa amefurahishwa na kazi zinazofanywa na taasisi hii ya kidini na ameamua kuungana nayo kwa sababu ni kazi za kibinadamu ambazo taasisi yake pia inazifanya na kuongeza kuwa hata serikali inaunga mkono na kuhimiza mashirika ya kidini kujitolea katika kuihudumia jamii.

IMG_3100

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali serikali y akata ya kigogo nayo haikusahauliwa, Mwenyekiti wa kata ya Kigogo Mbuyuni amesema kuwa wananchi wa kigogo wanabahati kubwa sana kwa taasisi hii kuwa katika kata hii, ameeleza kuwa huduma nyingi zinazotolewa na taasisi hii ya kishia inatoa huduma nyingi za afya ambazo sisi kama serikali tunatoa pongezi kubwa kwao, Mwnyekiti huyo ameeleza kuwa Mashia huwa wanafanya kazi nyingi katika maadhimisho yao kwa kupanda miti na usafi pamoja na misaada ya kijamii.

Samahat Sheikh Muhammad Abdi naibu wa Maulana Sheikh Hemedi Jalala, Samahat Sheikh Ghawth Nyambwa na Sheikh Qasimu waliwaongoza waumini katika tukio la kujitolea damu katika zoezi hilobaada ya sala ya Ijumaa ya leo.

 

Msiba na kumbukumbu za Imam Hussein si kisa cha huzuni pekee bali ni funzo juu ya ubinadamu na kuihudumia jamii, Imam Hussein alikwenda karbalaa kufa ili abaki milele.

AsadiqMedia, Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano,

Ofisi ya Maulana Sheikh Jalala,

Hawza Imam Swadiq a.s

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on September 29, 2017, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: