JINSI GANI YA KUFIKIA KUWA UMMAH

Muwasilishaji: Sayyid Arif

Imefasiriwa – AsadiqMedia

Aya ya Quraan (3:104) Al-Imran 3:104

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ 

Na uwepo katika na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio waliofanikiwa.

Jamii yoyote ili iwe ni yenye mafanikio (Muflihuni), njia ya kupitia ni kuwa Ummah. Kawaida Uchamungu ni suala la mtu binafsi, na ni moja ya vigezo muhimu vya kujenga Umma, Lakini suala la kufanikiwa kijamii kwa viwango vya Mwenyezimungu ni suala la Umma mzima na sio suala la mtu binafsi.

ummahBaada ya Watu kujenga Umma wao, ndio pekee wataweza kutekeleza Amri ya kulingania kheri kwa kuamrisha mema na kukataza maovu, Hii ni kazi inayofanywa wakati watu wamekuwa ni Ummah. Na haiwezekani kazi hii kufanywa na Mtu mmoja mmoja binafsi bila ya kuwa katika Ummah. Allah amebainisha wazi pindi watu watakapoweza kuwa Umma na wakatekeleza Amri yake kulingania kheri kwa kuamrisha mema na kukataza maovu, hao ndio kwa Viwango vya Mwenyezimungu wanaitwa waliofaulu”

Quraan kama kitabu cha Muongozo kila neno linalotumika limechaguliwa mahususi kubeba maana ya kuongoza jamii, Vivyo hivyo neno “Muflihun” ni neno linalotokana na neno asili “falaha” lenye kutumika kwa Asili kwenye kilimo, likijumuisha shuguli nzima za Uandazi wa shamba kupanda, kumwagilia kuweka madawa na hatimaye kuvuna, Kilimo ni shughuli inayohitaji juhudi na kazi ngumu.

Tukizingatia shughuli ya kilimo kama ilivyo, Mbali ya shughuli ngumu na ya juhudi kubwa ya kuandaa Shamba, kuchagua mbegu bora na kupanda, kuweka Mbolea, kuchunga mazao yasiharibiwe na wanyama pori, na hatimaye kupata Matunda mema kwa maana ya Mavuno ambayo kila mtu hufurahi na kusherehekea.

Vivyo hivyo Watu ambao wataweza kuwa Ummah wakasimamia kazi kuu ya kulingania kheri kwa kuamrisha mema na kukataza maovu watu hao Allah amewaahidi Mazao mazuri (Falaha).

Swali la kujiuliza sasa ni jinsi gani tunaweza kuwa Ummah?

Kuwa ummah ni tendo la kijamii, Jamii ndio inaweza kuwa Umma, Japo kuna nyakati ambazo hata mtu binafsi anaweza kuwa Ummah kama ilivyotajwa katika Quraan…. “Hakika Ibrahim alikuwa Umma mwema, mnyenyekevu kwa MwenyeziMungu, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina” (16:120)

Quraan inathibitisha kuwa Watu walikuwa hapo zamani ni Umma mmoja kabla ya Kukhitalifiana. Allah (sw) anasema katika Quraan tukufu

Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia kutokana na Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu ingeli kwisha katwa baina yao katika hayo wanayo khitalifiana. (10:19).

 Watu wote walikuwa ni umma mmoja. Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale walio khitalifiana. Na wala hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhini yake akawaongoa walio amini kuendea haki katika mambo waliyo khitalifiana. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka

Aya hizi mbili ni uthibitisho kuwa watu wakati fulani walikuwa ni Ummah mmoja na Allah akawapelekea Mitume/Manabii  wabashiri na waonyeji lakini baada ya kukumbwa na majanga. Watu wakagawanyika kijiografia, kikabila, kiirangi, kimila, kiutamaduni nk.

Leo ukitizama pia Jamii zetu, utaona jinsi watu walivyogawanyika Utaona kuna Watu wamegawanyika kwa Dini zao hapa kwetu Tanzania utakuta Waislamu na Wakristo, na hata ndani ya Waislamu utakuta kuna mgawanyiko, wapo Kundi la Masunni, Mashia, Ibadhi nk. Hata ndani ya Mashia au Masunni utakuta kuna Migawanyiko, kuna Mashia Khoja Ithnaashariya, na Mashia Waafrika, Ndani yao pia wamegawanyika zaidi.

Ni wazi basi kazi kubwa waliyotumwa Mitume/Manabii ilikuwa kuvunja Migawanyiko hiyo na kuwafanya watu kuwa Umma mmoja, ili kuweza kulingania kheri kwa kuamrisha mema na kukataza maovu.

Inafaa ieleweke hapa kuwa, Mkishindwa kuwa Ummah mmoja kazi ya kulingania kheri kwa kuamrisha mema na kukataza maovu haitawezekana, hata kama ndani yenu mnadhani inawezekana. Ni kutokana na ukweli kuwa jamii unayoishi maadamu imebakia katika Migawanyiko yao ya Kikabila, Kibiashara, Kivuvi, kiufugaji, kielimu, kikabila, kiutamaduni, ni dhahiri maslahi yao yatakapoguswa jamii hiyo itakuwa ya mwanzo kuendesha mapambano kupiga juhudi na kazi ya kulingania kheri kwa kuamrisha mema na kukataza maovu inayofanywa na mtu mmoja mmoja.

Mfano jamii yenye kuamini kwenye biashara bila mipaka ya Halali na haramu, Anapoibuka mtu binasfsi bila kuwa na Umma katika kulingania kheri kwa kuamrisha mema na kukataza maovu, akasema wazi kuwa Biashara fulani ni haramu, Jamii husika itampinga, itamtenga na hata kutangaza vita vya mapambano ya kufa na kupona kumzuia.

Tahadhari na ieleweke kuna tofauti kati ya kuwa Wamoja na kuwa Ummah, japo kama ilivyokuwa katika Uchamungu wa mtu binafsi, Umoja nao ni nyenzo muhimu sana ya kuwa Umma.

Katika Harakati mnazozifanya ni matendo yenu binafsi ya mtu mmoja mmoja ambayo hutoa taswira kabisa juu ya Muelekeo wenu. Kama matendo yenu binafsi yanalengo la kuwa Ummah basi ifahamike hii ni hatua ya awali ya ujenzi wa umma, Kinyume chake matendo hayo hutafsiriwa ni matendo mema tu ambayo kila mtu bila kujali dini yake pia anaweza kufanya.

Ili kupata picha kamili turudi katika Historia ya Mtume na maisha yake, Mtume alipohamia Madina, kazi ya kwanza aliyoifanya ilikuwa ni kuwaunganisha Makabila makuu mawili ya Madina (Yathrib) Aus na Khazraj. Makabila haya mawili kutoka Yemeni kwa kipindi chote cha Maisha yao walikuwa wakiishi vitani kila mmoja likipigana na jingine. Mtume akayaunganisha Makabila haya Mawili na kuwapa jina jipya “ANSAR” (Waliomnusuru Mtume), Jina hili lilikuwa ni cheo na heshima kwao na liliwaunganisha wote bila kujali tofauti zao za kihali na Mali. Pia mtume kwa kutambua tofauti walizokuwa nazo watu wa Makka na migogoro ya Makabila na koo zao, alifanya vivyo hivyo kwa kuwapa jina la heshima na Cheo kwa kuwaita MUHAJIRUN (Waliohama wakaacha kila kitu chao kumnusuru mtume), Makundi haya mawili Ansar na Muhajirini waliishi kipindi chote cha Mtume kwa kuheshimiana, kushirikiana, kuthaminiana, na kusaidiana wakijuana kila mmoja kwa utukufu wake wa kumsaidia mtume. Mtume hakuunda, chama, Taasisi, Kampuni wala vuguvugu la kisiasa mtume alilenga kuunda Ummah.

Kitendo hiki cha mtume kilifuta Ukabila uliokuwepo, Utaifa na ukanda, ueneo, Utukufu wa kabila, Ukoo, Majivuno, kujitamba kwa nasabu, Tofauti za kipato na mali, Wote wakaungana na kuwa Umma mmoja.

Lakini Masikitiko Makubwa ni baada ya Mtume (saw) kufariki. Jamii zote zikarudi katika Migongano na Malumbano yao. Tukio la kikao cha Sakifa ni uthibitisho tosha juu ya hilo, Walikuwa wakilumbana na kugombana kupitia Ubora wa Makabila, Utukufu wa Koo zao na ukaribu na Mtume, Ueneo na ukanda nk. Kama wanaharakati lazima tutambue hili tendo la kugawanyika ni jambo la kawaida hususani pale watu wanapokumbwa na Majanga na matatizo (Afat).

Nini Maana ya neno Umma,

Umma ni neno la kiarabu linaloumbwa na neno Umam, neno  hili ndilo Asili pia ya neno la kiarabu Umm yaani mama na maana yake ni  kutenda jambo kwa Azma (nia) ya kurudi kwenye Asili.

Mfano Mama ameitwa kwa jina la Umm kwa sababu yeye ndiye asili ya Mtoto.

Hivyo basi ili jamii yoyote ifikie kwenye kuwa ummah lazima ziwepo juhudi za makusudi zenye nia thabiti ya kurejea kwenye Asili yao.

Swali la kujiuliza Allah (sw) anatutaka tuwe Umma Je ni kitu gani hatutaki tusiwe? (kwa maneno mengine Allah anatuzuia kuwa nini?)

Ni wazi mpaka hapa kuwa Uislamu na Mwenyezi Mungu hataki sisi tuwe jumuiya (kaumu). Kama vile Kaumu ya Firaun (26:11:1), Kaumu Nuh (26:105:2), Kaumu Lut (26:160:2), Kawmu Ibrahim (22:43:1).

Kaumu ni watu wanaojikusanya kwa lengo fulani na wakabakia kwenye lengo hilo maisha yao yote. Mfano Kwa nchi ya Tanzania Wamasai ni Kaumu inayojikusanya na kujitambulisha kwa utamaduni wa Ufugaji ng’ombe wengi. Wamekuwa wakifanya sghughuli hii kwa Muda wao wote, Na hata inapotokea eneo walilopo hakuna malisho kwa Ng’ombe wao, jamii hizi huhama maeneo yao na kwenda kuendeleza shughuli zao sehemu zenye Malisho. Zipo jamii za Wakulima, Wafanyabiashara, Wavuvi, Wahunzi, Masonara nk sifa ya muhimu inayowatofautisha hawa na Umma ni kuwa Kawmu Aghalabu hawabadiliki.

Unapoitazama jamii ya kitanzania Watu wamegawanyika katika kaumu tofauti tofauti, Kuna waliojikusanya kutokana na jioghrafia, Maeneo ya Madini, Kilimo, Utamaduni, na Hata kuna waliojikusanya kwenye Imani ya Dini fulani.

Mifano iliyo hai ni jumuiya za Masunni, Jumuiya za Mabohora, Jumuiya za mashia Ithnaasharia, Jumuiya za Mahindosi nk. Hizi ni Kaumu ambazo kwa kipindi chote cha maisha wao wamekuwa wakifanya jambo fulani walilokubaliana bila kubadilika.

Hivyo watu wote waliobakia sehemu moja wakifanya jambo fulani kwa kipindi chote cha maisha yao bila kukubali kupiga hatua mbele ya mabadiliko watu hao tunawaita ni Kaumu.

Kwa kawaida kanuni za Maumbile na sunnah ya Mwenyezimungu ni zenye kuhitajia mabadiliko na kupinga kutulizana sehemu moja kwa jambo moja. Kila utakachokitizama katika Viumbe na maumbile aliyoyaumba Mwenyezimungu utagundua vyote ni vyenye madiliko yenye kuendelea kila wakati. Na kinyume chake eneo au sehemu yoyote isiyokubali mabadiliko mara zote hukumbwa na aina zote za uchafu, Vijidudu hatari, Baktaria, Maradhi, Husuda, majivuno, Uvivu, ususuavu na kila aina ya kasoro na matatizo.

Hata kwenye Mazingira ya kawaida, Maji yaliotuama na maji yanayotembea utaona athari ya mabadiliko, Wakati wote maji yaliyotuama huwa ni Machafu, rahisi kukusanya vijidudu, Hutoa harufu na hatari kwa Afya na mazingira ya Binaadamu, Wakati maji yenye kutembea, huwa na Sifa ya Usafi, rutuba, na sahihi kwa matumizi ya binaadamu.

Hata mimea uwepo wa Maumbile ya Mmea yaani Mizizi, Shina na matawi ni kuwezesha mabadiliko ya kila siku, Endapo Mmea utakosa majani ya kuzalisha  chakula cha Mmea kutoka katika Mwanga wa jua, Mzunguko husimama na mabadiliko pia husimama na mmea hufa. Kila kitu katika dunia huhitajia mabadiliko ya kila wakati ili kubakia hata Mwili wa binaadamu bila mabadiliko ya mzunguko wa Damu mwili hupatwa na mauti (Mfu)

Inafaa kutambua basi watu wanaojikusanya kwa mambo yasiohitajia mabadiliko kama vile Uchumi, Kilimo, Biashara, Ukabila, Tamaduni zao hizi ni jamii mfu na kiala aina ya Maradhi huzikumba jamii hizi ikiwemo, Watu wake kuoneana Choyo, Husuda, Kudharauliana kwa utukufu wa Makabila, Upendeleo, Utwana na Ubwana, nk. Ili jamii hii iwe hai tena na isonge mbele kujiletea mabadiliko ya kweli lazima kubadilika kutoka kuwa Kaumu na kuwa Umma.

Umma ni jamii inayobadilika kwa kijipatia madiliko yake kwa kuzunguka katika Mhimili wa Mwenyezi Mungu.Na  Mhimili huo ni kuwa na Itikadi (Ideology) sahihi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Katika Itikadi hiyo watu wote wanakuwa na Lengo moja walilopewa na Allah  (sw) na wanapolitekeleza lengo hilo hupata cheo cha kuwa Waliofaulu (Muflihun).

Sifa za Waliofaulu (Muflihun) ni zipi?

  1. Kuwa na Itikadi moja
  2. Kuwa na Lengo moja
  3. Kuwa na Njia moja ya kufikia lengo
  4. Kufanya Harakati katika njia hiyo

Mambo yote haya matano Umma unatakiwa kuwa nayo, bila kutofautiana. Mmoja hawezi kusema nakubaliana na Itikadi na lengo lakini nina njia zangu tofauti na wengine, Au nakubali Itikadi lakini ni malengo yangu, hilo haliwezekani.

Swali; Je endapo nitatambua Itikadi yangu, nikatambua Lengo, njia na nikabakia katika harakati ya kufikia lengo, huwenda wakatokea watu wakanishawishi nikatoka katika lengo, na/au Wakati wa harakati za kufikia lengo nikakumbwa na matatizo, nawezaje kubakia na msimamo wangu ule ule?

Inafaa kueleweka wazi kuwa pindi mtu anapotambua Itikadi sahihi anayopaswa kuwa nayo, akaweza kubainisha malengo yanayohusu na akaziainisha njia za kufikia lengo, Maadamu atabakia katika harakati hii, Kanuni za maumbile zitamlazimisha kutafuta Mtu wa kumuongoza kuepuka kuondolewa katika njia na au kuhimili matatizo ya kutetea itikadi aloichagua.

Ni kwa mantiki hii linapokuja suala la Uongozi na Uimamu katika Umma na kufanya suala hilo kuwa ni la kimaumbile zaidi. Hivyo hitajio la Kiongozi/Imamu sio suala la kiimla ambapo watu wanalazimishwa au wanawekewa kiongozi bila matakwa yao. La Hasha, Uongozi/Imamu ni suala linaloendana na Maumbile ya mtu, ni suala analohitajia kumuongoza katika kuifikia Itikadi aliyoichagua.

Mfano Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nchi ina katiba yake, ina mgawanyo wa Mihimili ya Dola na inakazi za kusimamia kila siku kwa ajili ya kuwatumikia Raia wake, Ni kutokana na changamoto ya kazi hizi na ugumu wa usimamizi serikali zikalazimisha lazima wawepo Viongozi watakaopewa majukumu ya usimamizi na kuongoza jamii na ndipo wanapopatika Maraisi, Mawaziri na wakuu wa Idara mbali mbali.

Serikali za kiliberali kwa kuwa Wanaadamu wamejipa Mamlaka ya utungaji sheria kwa ajili ya matumizi yao, Watu hao hao wamejiwekea taratibu za kuwa na Viongozi kwanini? Kwa sababu hii ni kanuni ya kimaumbile.

Vivyo hivyo tofauti na serikali za Kiliberali katika dini ya Uislamu, Mwenye mamlaka ya utungaji wa Sharia zote ni Mwenyezimungu kwa ajili ya manufaa ya wanaadamu. Na ni kwa mamlaka hayo hayo Allah anakuwa na mamlaka ya kuteua nani awe kiongozi wa kusimamia na kuelekeza Sheria zake alizozitunga.

Swali litaulizwa Je ni wakati wote na kwa kila sehemu Mwenyezi Mungu atakuwa akituchagulia Viongozi

Jibu: La hasha, Mwenyezi mungu alichofanya ni kuteua viongozi viigizo wema kwa watu na akawafanya viongozi wa jamii, Mwenyezi Mungu aliwateu maimamu kina Ali Ibn Abii Twalib, Hassan, Husein nk. Kisha baada ya hapo Allah hakuwa na haja ya kuendelea kuteua viongozi, bali aliweka Sifa/Vigezo anuai vya kuzingatiwa kwa kila zama ili kumpata kiongozi.Swali litaulizwa Je ni wakati wote na kwa kila sehemu Mwenyezi Mungu atakuwa akituchagulia Viongozi

Wajibu wetu katika Umma ni kuzingatia vigezo vilivyoweka na kuhakiki sifa za viongozi walioteuliwa na Mwenyezimungu kama kipimo cha kumpata kiongozi wa kutuongoza katika Itikadi tulioibainisha na njia tulikubaliana kwa ajili ya kufikia lengo.

Hili litawezekana tu  kama msingi wa harakati yenu ni kuwa Umma wa kiislamu, Isipokuwa kama malengo ni kujenga Kaumu yenu hili halitawezekana, Kwani kaumu kwa kuwa lengo lake ni kubakia katika jambo waliloliochagua basi watamchagua aliyebobea kwenye hilo, Kama ni kawmu ya Wakulima basi sifa za kiongozi itakuwa mwenye Mazao mengi na Mashamba makubwa, kama ni Kaumu ya wafanyabiashara kiongozi atachaguliwa mwenye biashara kubwa na Mtaji mkubwa, na endapo ni kaumu ya Kimila na utamaduni, kiongozi atatoka kabila kubwa na lenye ushawishi mkubwa katika jamii.

Inafaa tuelewe kuwa tunaweza kama harakati kujenga shule nzuri, kuwa na madarisi, Hospitali na vituo vya Afya, maeneo ya kulea Mayatima, Miradi ya kilimo na Uvuvi, vyombo vya habari nk. Lakini bado tunahitaji kuwa na Kiongozi atakayetutoa kati mazingira haya ya Kaumu na kutufikisha katika Umma ili tuwe ni wenye kufaulu (Muflihuun).

 

Sifa za Umma ni zipi?

  1.  Kuwa Muwahidi na kutokuwa Mshirikina.

Allah anasema katika Quraan tukufu… “Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina. (3:67)

Sifa ya kwanza aliyokuwa nayo Nabii Ibrahimu ni kutokuwa mshirikina, Hakuwa akimshirikisha Allah kwa namna yoyote. Ni kwa sifa hii ya kukataa kuwa mshirikina kwa namna yoyote ile Allah anamuamrisha mtume kuwa mfuasi wa Nabii Ibrahimu pale anaposema… “Sema: Mwenyezi Mungu amesema kweli. Basi fuateni Mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina (3:95)

Tahadhari kubwa lazima tuwe nayo linapotajwa neno Shirk, Kasumba tuliwekewa vichwa ni mwetu ni kuwa Shirk ni tendo la Mtu kuabudu sanamu tu, La hasha ni aina moja tena ya kale iliyozoeleka, Shirk zipo za aina tofauti tofauti;

  • Kuna Shirk kuhusiana na uwepo wa Alla (S.w.T.)
  • Shiri kuhusiana na Sifa za Allah (S.w.T.)
  • Shirk kuhusiana na Matendo
  • Shirk kuhusiana na Utii (Ubudiya)
  • Na Shiriki kuhusiana na Ibada (Rububiya) Katika Kuumba (Takwini) na katika utungaji wa Sheria (Tashrii).

Utakapozitizama aina hizi zote za Shirki na ukatizama harakati zetu utagundua kuwa  mambo yote yanayohusiana na kitendo cha watu kujiwekea kanuni za kufanya haraki ni mali ya wachache ni Shirk, Kitendo cha kuzuia watu wengine wasishiriki katika harakati ni Shirk, kitendo cha mtu kuona Wivu juu ya uwezo wa wengine na akatamani wasiwepo ni sehemu ya shirik, kuhodhi na kujitawalisha juu ya watu ni sehemu ya shirki, Ubinafsi ni sehemu ya shirik, Imani kuwa unajitolea zaidi kuliko wengine ni aina ya shirki, kutothamini kazi za wengine ni sehemu ya shirki, Kujiona wewe ndio msimamizi wa wengine na wengine wanatakiwa kuwa chini yako ni Shirk. Kama tunataka kuwa katika Umma lazima tuzihakiki nafsi zetu na kufuta aina zote za shirki na kubakia ni Muahid kama sifa ya kwanza kuwa katika Ummah.

 

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 17, 2018, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: