KHUTBA YA SALA YA EID ADH-HA 2018

Sala ya eid ya kuchinja imesaliwa katika viwanja vya Pipo Dar es Salaam Tanzania ikiongozwa na Sheikh Mkuu wa Jumuia ya Mashia nchini Samahat Sheikh Abdallah Seif. Khatibu wa Sala ya Eid Maulana Sheikh Hemedi Jalala ameleeza kuwa Eid kubwa ni Eid ya kijamii na kuhurumiana.

photo_2018-08-22_13-33-14

Ifuatayo ni sehemu ya khutba yake:

Enyi vipenzi nawasalimia kwa salamu ya Allah yenye baraka, Mola mtukufu anasema katika kitabu chake kitukufu ” Sali kwa ajili ya Mola wako na uchinje” .

Sala hii inayobeba jina la Eid ya kuchinja historia yake na tarekh yake inarudi kwenye jambo la huruma, mapenzi na upendo. Nabii Ibrahim ambae ndie baba wa dini zote aliona usingizini ya kuwa anamchinja mwanae, na kwa kuwa ndoto za mitume ni ufunuo Ibrahim alimchukua mwanawe ili kwenda kutekeleza ndoto ile, Allah akamtuma Jibril ampelekee kondoo kasha Ibrahim akaambiwa na Allah kuwa ewe Ibrahim umeifanyia kazi ndoto, na hivyo ndivyo tunavyowalipa wenye kutenda mema.

Hii inatuonesha kuwa Eid hii ni Eid ya mapenzi na huruma kwa kubadilishwa Nabii Ismail ili abakie na asichinjwe kwa msingi huu ukiisoma Eid hii utaiona ni Eid ya huruma inayolenga kumbakisha mtu kama alivyobakishwa Nabii Ismail na badala yake akaletwa kondoo, Eid hii ni Eid ya kupendana watu, kupendana watu wote walio hai nsio maana Ismail akabakizwa na kondoo achinjwa badala yake, kitendo hiki cha kuenzi tukio lile linatufunza pia kuwa huruma hii iwe kwa waliotangulia mbele ya haki, wale ambao walifanya mazuri kwetu ambayo tunayaenzi, wale waliotulea na kutusaidia mpaka tukafika hapa tulipofika, Hii ni moja ya namna ya kusherehekea Eid hii.

Kwa hivyo ujumbe wetu katika Eid hii ni ujumbe wa kuwaonea huruma wale waliotangulia mbele ya haki, tulikua na wazazi na wapenzi wetu ambao wametangulia mbele ya haki katika Eid hii tuwakumbuke wenzetu.

Tunahimiza Sunnah ambayo inakwenda sambamba na Eid hii, ni muhimu kuizungumza Sunnah hii kwa sababu imeuwawa, Mtume Muhammad s.a.w.w anasema:

 “wenye kuihuisha Sunna iliyouwawa basi anaujira wa mashihidi 100”

Katika jambo la kusikitisha sunnah hii ya kuwakumbuka waliotangulia na hususan kuzuru makaburi yao imeteketezwa na waislamu wameliwacha jambo hili, ukimsoma Bibi Fatima a.s alikua akiwatembelea marehemu na mtume Muhamamd s.a.w.w anasema :

“Nilikua nimewakatazeni kuzuru makuburi lakini sasa yazuruni makaburi kwani yanawakumbusheni Akhera.”

Muumini mjanja ni yule ambae hata akiwa na hali nzuri huwa anakwenda kuzuru makaburi kwani kunamfanya mtu aamke kama alikua amejisahau, kunamfanya mtu aione dunia kuwa  ni mapito na kwamba itampita kama ilivyowapita hawa walio katika mashimo leo, kuzuru makaburi kunaongeza chachu ya kuipenda akhera na ni kuwatendea wema ndugu zetu, Je ikiwa umekwenda kuwatembelea wazazi wawili ambao Allah ameelekeza kuwatembea mema ni jambo zuri kiasi gani?

Tutambue ya kwamba tunapokwenda makaburini mwao wanafarijika na wanajisikia raha, Mtume anasema: “Hakuna mtu yeyote anaelizuru kaburi la ndugu yake illa marehemu huyo analiwazika.”

Katika moja ya faida ya kuzuru makaburi pamoja na kuwa ni kuwafanyia wema lakini ni kuwashukuru na kwa sababu hii mola hukupa baraka,  Mtume anasema:

“Hakuna mtu anaetembelea kaburi la ndugu yake aliyekua anamjua ila Allah humrudishia roho yake ili aijibi aalamu yake.”

Ndugu zangu kuzuru makaburi ni sunnah nzito na muhimu, Mtume Muhammad siku ya Alhamis alikua anaonekana akienda Baqii au makaburi ya uhudi na huku akisema Allah ameniamrisha niwaombee rehema na msamaha watu wa Wahudi.

Imam Ali nae alikua akizuru makaburi na akifika hapo anayaambia makaburi hayo “Zile nyumba mlizokua mnakaa zinakaliwa na wengine na wake zenu wameolewa na watu wengine, hizi ndio habari zetu vipi ninyi mnahabari gani”

Maulana aliendelea kuhimiza kuwa Eid lazima iwe ya kijamii.

Khutba nzima inapatikana kwenye chanel yetu ya www.youtube.com/asadiqmedia

Sehemu ya Khutba hii imehaririwa na :

AsadiqMedia, Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano

Ofisi ya Maulana Sheikh Jalala.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 22, 2018, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: