HII NDIO EID KUBWA KABISA YA WAISLAMU

JE UNAITAMBUA EID KUBWA KABISA YA WAISLAMU?

Eid hii ni Eid y Ghadiir.

Eid Elfitri na Eid ya kuchinja ni Eid mbili kubwa na maarufu Zaidi, lakini Eid ya Ghadiir ndio Eid kubwa kuliko hizo mbili. Siku ya Ghadiir ni siku maalumu ambayo mtume wa Waislamu alitangaza waziwazi uteuzi wa mungu juu ya nani atakua mrithi wake, kiongozi, imam na khalifa wake baada yay eye kuondoka duniani. Mtume akamtangaza  Imam Ali bin Abi Talib kuwa kiongozi, khalifa na wasii wake baada yake.
21430462_1275216705921655_2151488920147441183_n

ASILI YA EID YA GHADIIR

Baada ya kumalizika Hijjah ya mwisho ya mtume (hijjah ya kuaga), Mahujaji wakiwa njiani kurudi nyumbani kwao walifika eneo liitwalo Ghadiir-Khum ( Bonde la Ghadiir) na hapo mtume alitekeleza amri ya Allah ya kumtangaza kiongozi na mrithi wa mtume baada ya kuondoka mtume.

TAREHE

Tukio hilo lilitokea tarehe 18 Dhul hijjah mwaka 10 Hijiria.

AMRI ILIYOSHUKA

Hapo Ghadii Khum, Malaika Jibril na amri kwa mtume kutoka kwa mola wake isemayo:

“Ewe Mtume! Fikisha kile ambacho kimeteremshwa kutoka kwa mola wako, na usipofikisha , basi utakua hujafikisha ujumbe, na hakika Allah atakulinda na watu, hakika Allah haongozi watu wasio na imani” Quraan (5:67).

UTEKELEZAJI

Akiwa hapo ghadiuir khum Mtume aliamrisha watu wote waliotangulia mbele warudi nyuma na walio nyuma wasubiriwe.

WALIOKUSANYIKA

Mtume akaamuru jukwaa (Mimbari) iandaliwe kwa majabali na matandiko ya ngamia na maswahaba wakatekeleza na wakakaa kulizunguka jukwaa.

HOTUBA YA MTUME

Siku hii mtume wa Allah alitumia wastani wa saa tano katika eneo hilo, kati ya masaa hayo mtume akiwa juu ya jukwaa alisoma aya Zaidi ya 100 kutoka katika Quraan tukufu, na kwa Zaidi ya mara 73 akiwaonya watu kuhusu matendo yao na mustaqbali wao. Kisha akahutubia hotuba ndefu.

VIZITO VIWILI

Kasha mtume akawajulisha maswahaba zake kuwa punde tu mauti yatamchukua na akasema :

“Ninakuachieni vizito viwili vyeneye thamani kubwa, kama mtashikamana navyo vyote viwili hamtopotea baada yangu. Vizito hivyo ni kitabu cha mwezimungu , Quraan na Watu wa kizazi change (Ahlulbayt) vizito hivi viwili havitatengena mpaka vinijie katika kisima (hodhi ya kawthar)”.

UTEUZI WA MRITHI WAKE

Kisha mtume akawauliza waliokusanyika

“Je mimi si mwenye haki Zaidi kwa waumini kuliko haki walizonazo kwao wenyewe”

WAKAJIBU: “Ndio bila shaka ewe mtume wa Mwenyezimungu”.

Kisha mtume sa.w.w. akaushika mkono wa Imam Ali a.s na kuunyanyua juu kuonyesha kwa watu kisha akasema:

“Yeyote yule ambae mimi nilikuwa MAULA (bwana wake), Basi Ali ni MAULA (bwana wake)”.

DUA KWA MRITHI WAKE

Baada ya kutangaza mrithi wa utawala baada yake akamuombea dua hii

“Ewe mola wangu! Mtawalishe atakayemtawalisha Ali! Na mfanye adui atakayemfanya adui Ali!Ewe mola wangu mpende yule atakayempenda Ali na mchukie yule atakaemchukia Ali”.

MKONO WA KIAPO (BAIYA) NA PONGEZI.

Baada ya dua kumalizika masahaba wote mmoja baada ya mwingine wakapita na kumpa Imam Ali mkono wa kiapo cha utii na pongezi kwa kuteuliwa kiongozi baada ya Mtume.

AYA YA KUKAMILISHWA DINI

Mara tu baada ya Imam Ali kutangazwa kuwa mtawala / mrithi wa mtume , Allah akashusha aya ya Quraan  hapohapo eneo la khadiir Khum isemayo:

“Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimetimiza neema yangu kwenu na nimeridhia Uislamu kuwa dini yenu” Quraan (5:3)

KWA SABABU GANI EID HII NI KUBWA

Eid hii ni kubwa kuliko Eid zote kwa sababu imeambatana na matukio mawili ya msingi ambayo ndio msingi wa kubakisha ndoto za mitume na utawala wa Allah katika mgongo wa ardhi. Matukio hayo ni Kuteuliwa kiongozi baada ya Mtume ili kuhakikisha mafunzoya mtume yanabaki kama iapavyo na tukio la kukamilishwa dini. Eid ya Fitri ni baada ya kukamilisha swaumu na Eid Elhaj ni baada ya tukio la hijjah kubwa, mambo hayo yote ni sehemu ya matawi ya dini na nguzo za dini ila siku ya Ghadiir imekalishwa dini yote inayobeba matawi yote kama swamu na Hijjah kupitia kuteuliwa Imam Ali bin Abi Talib kama kiongozi wa waislamu baada ya mtume.

TUNAWATAKIA EID NJEMA

Imeandaliwa na

AsadiqMedia

Email: asadiqmedia@gmail.com

Facebook: http://www.facebook.com/asadiqmedia

Youtube: http://www.youtube.com/asadiqmedia

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 29, 2018, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: