Matendo ya Ibada Siku ya Eid Al-Ghadir

lvl220150930020714

Matendo ya Ibada ya kufanywa Siku ya Eid Al-Ghadir
Kwa mujibu wa Hadith iliyopokewa na Imam Ali Ibn Musa Ridha (as) anasema:

“Kuna malipo makubwa mno kwa muumini kuwepo katika mji mtukufu wa Najaf siku ya leo kwa ajili ya kumzuru Imam Ali ibn Tali (as). Toa sadaka siku ya leo kwa kadiri uwezavyo, Kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa watu masikini, kwasababu “siku ya Ghadir” ni mahususi kwa ajili ya kusaidia wasiojiweza”

MATENDO YA IBADA SIKU YA LEO

1.    Kuoga kabla ya Swala ya Dhuhur, Vaa nguo safi na nzuri na jipambe kwa manukato.

2.    Funga swaumu ya Sunna

3.    Soma Ziara Maalumu ya kumzuru Imam Ali ibn Abii Twali (as)

i)    Ziyara Ameenallah

ii)  Ziyara Mut’laqah

4.    Soma dua Nudbah

5.    Unaweza kushereka kwa namna yoyote isiyopingana na sharia za kiislamu lakini kubwa wakumbuke watu wa nyumba ya Mtume (Ahlulbayt) kwa kusoma sana ‘Swalawaat’ mara nyingi iwezekanavyo. Sema Allahumma Swali alaa Muhammad wa Aali Muhammad  (Ewe mola wangu wa haki rehemu juu ya Muhammadi na Ahli zake)

6.    Swali rakaa mbili za sunnah kabla ya Swala ya Dhuhri Katika kila rakaa baada ya suratul Hamdi soma kama ifuatavyo;

(i)           Suratul Ikhlas (Quraan 112:1-4) mara 10

(ii)          Ayatul Kursi (Quraan 2:255-257)  mara 10

(iii)        Suratul Qadr (Quraan 97:1-5) mara 10.

(iv)        Baada ya salamu nenda katika Sijida na sema mara 100; Alhamdullilah, Shukran Lillah

7.    Kisha kaa kitako na soma dua :

‘Allamumma Inni Asaloka Be Anna Lakal Hamda Wahdaka” Mara 100

8.    Wakati utakapokutana na Ndugu yako muislamu sema kumsalimia: Sifa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye alitubariki sisi kuwa miongoni mwa – wale ambao wanamshikamana na kushikilia “Wilaya” (upendo, urafiki na mamlaka) ya Ameerul Muminiin na mamimamu wote, amani iwe juu yao wote.

Sifa ni kwa Mwenyezi Mungu ambaye alitutukuza na siku hii, na kutujumuisha sisi miongoni mwa wale waliopewa kila kitu kilichoahidiwa, na wamefungwa pamoja na vifungo vya mkataba wa kuwa na Imani thabiti katika mamlaka ya sheria za kidini zilizoanzisha haki; na hakutuabisha sisi kuwa miongoni mwa wale wanaojua jema lakini wakapinga ukweli na na kuifanya  Siku ya Hukumu kama hadithi ya uwongo.

9.    Soma dua hii Mara 100: Sifa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amefanya dini yake na kukamilisha neema yake kwa kuanzishwa kwa mamlaka ya utawala wa Ali ibn Abi Talib, amani iwe juu yake.

10. Omba Msamaha kwa Mwenyezi mungu (Istighfaar). Kwani Madhambi husamehewe  na waumini hupata uokovu na moto siku hii kama vile ilivyo katika Masiku ya Mwezi wa ramadhani na usiku wa Laylatul Qadr.

11. Kuwasaidi wenye shida miongoni mwa Waumini. Malipo ya mwenye kutoa Msaada siku hii ni mara 1000 zaidi ya siku zingine. Kutenda wema kwa waumini wenzio inajumusha kujitolea kwa hali, nguvu na Mali na kuwafanya wawe na furaha (Mfano; kuwasamehe waliokukosea zamani, kutokuhesabu makosa yao, kuwatembelea, kuwapa zawadi nk)

12. Soma dua ya Siku ya Eid al Ghadir

Yule ambaye atatekeleza Matendo haya ya Ibada siku hii ya Ghadir atapata malipo sawa na yule aliyekuwepo siku ile pale Ghadir Khum, akalisikia Tamko la Mtume akalikubali ni kweli na kulifuata.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on August 30, 2018, in Habari na Matukio, Makala and tagged , , , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: