MAMA KHADIJA: KIIGIZO CHEMA KWA KINA MAMA WOTE DUNIANI

Na fatma Majjid

Kabla ya kuja uislamu Bi Khadija alikuwa ndiye Malikia wa Mji wa Makkah, lakini mara tu nuru ya uislamu ulipoanza kuchomoza, Allah (sw) alipendezwa kumteua na kumfanya Mwanamke malkia wa uislamu pia. Allah (sw) pia alipendezwa kumteua na kumtunuku kuwa Mama wa waumini wote kama alivyosema katika kitabu chake kitukufu:

“Nabii ni bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao” (33:6)

Mama Khadija aliyatoa mapenzi yake ya dhati kwa waumini, mapenzi ambayo hakuna mwingine zaidi ya mama awezaye kuyatoa. Mapenzi haya yanaweza kuthibitika pale wanawe wanapokuwa na njaa, mama huwapa chakula watoto wake kwanza. Na zipo nyakati humlazimu Mama kuwalisha wanawe chakula hata kile chake na yeye kubakia na njaa. Haya yametokea mara nyingi katika historia hususan nyakati za kiangazi, njaa na ukame. Ukweli ni kwamba furaha ya kweli ya Mama ni pale anapowaona wanawe wamekula vizuri na kuridhika, hilo tu linatosha kumbakisha mama yao katika furaha na liwazo la moyo na hilo linatosha kumfanya kusahau hata njaa na kiu yake binafsi. Penzi la Mama halina Masharti ni penzi la hakika na lenye kudumu.

Historia ya uislamu inatufunza kuwa sehemu kubwa ya Waislamu wa Mji wa Makka wakati wa awali walikuwa ni Masikini sana. Hawakuwa na vyanzo vya kipato cha kila siku, hawakuwa na njia za kuendesha maisha yao ya kila siku, kwani njia zote za uchumi zilikuwa zikimilikiwa na muungano (Cartel) wa wafanyabiasha Washirikina.  Wanachama wa Muungano huo wa wafanya biashara walikubaliana kutowalipa waislamu mshahara wala ujira wowote kwa kazi yoyote wanayoifanya kwao na kupitisha marufuku kwa wakaazi wote wa Mji wa Makka ya kununua na au kuuza chochote kwa waislamu.

Walijua kuwa mgomo huo utaathiri kwanza miili yao kwa njaa na hatimaye Imani zao, walijua kuwa njaa na dhiki zitakazo sababishwa na vikwazo hivyo vya uchumi na biashara, hatimaye zitaathiri misimamo yao kwenye dini na hatimaye kupuuza na kutupilia mbali dini na ujumbe aliyokuja nao Muhammad. Lengo kuu la kampeni hii ya vikwazo vya kiuchumi na kususiwa biashara kwa jamii change ya Waislamu wa Makka ilikuwa ni kuleta baa la njaa kwa waislamu na mateso.

Lakini kinyume na matakwa na vitimbi vya Washirikina hao Allah (sw) kwa mapenzi yake akamleta Mama Khadija (s.a) Mwanamama Tajiri na mfanyabiashara mkubwa Arabuni, ambaye alitumia fedha zote za utajiri wake kuwalisha Masikini wote wa kiislamu wa mji wa Makka siku hadi siku hadi kufikia wakati ambapo hapakuwa na Masikini wa kiislamu anayeshinda na njaa na pia aliwapa wote makaazi/nyumba za kuishi.

Aina hii ya msaada haikuwa mpya, kwenye historia ya mwanaadamu bali ni ukubwa wake na kujitolea kwake ndiko kulikofanya msaada huo kuwa wa kipekee; Bibi Khadija aligawa fedha nyingi mno kwa Masikini wa kiislamu na wasio na nyumba katika mji wa Makka na kwa kitendo hicho akavuruga mipango yote miovu iliyokusudiwa na muungano wa wafanyabiashara washirikina kwa kampeni yao ya vikwazo vya uchumi na mgomo wa biashara kwa Umma mchanga wa waislamu.

Msaada aliutoa Bibi Khadija kwa jamii ya waislamu wa mji wa Makka ulikuwa ni Msaada muhimu sana na msingi wa uti wa mgongo wa uhai wa Dini ya Uislamu. Msaada wa Bi Khadija ulitoa uhai mpya kwa jamii changa na masikini ya Kiislamu na kutoa uhakikisho wa maisha marefu kwa umma wa kiislamu japo ummah huo ulikuwa katika mkwamo mkubwa katika historia. Kwa mnasaba huo Bi, Khadija aliibuka kuwa mtengenezaji mkuu wa ummah na historia ya Uislamu.

Ni ukweli usio na shaka kwamba wakeze mtume Muhammad (saw) wote ni Mama wa waumini, lakini hakika baina yao na Khadija kulikuwa na Tofauti kubwa mno nay a kimsingi. Wanawake wote walioolewa Madina walikuwa wakipokea mafao ya kujikimu kutoka Baytul Mal (Hazina kuu ya Umma). Baadhi yao wengine waliomba kupewa upendeleo wa pekee na kupeleka maombi kwa mtume ya kupewa Marupurupu ya ziada. Walikuwa wakisingizia kuwa Mafao ya kujikimu wanayopokea kutoka Baytul Mal hayatoshi kukidhi mahitaji yao ya kila siku na hivyo kushindwa kugharamia chakula chao cha kila siku.

Mama Khadija kwa upande wake hakuwahi hata mara moja kuomba kwa Mumewe fedha ya aina yoyote. Sio tu hakuomba kwa mumewe kuletewa chochote kutoka kwa mumewe, alijitolewa mfuko wake wa Fedha na kupeleka katika Hazina kuu ya fedha (baytul Mal), ulikuwa ni msaada mkubwa sana na fedha nyingi kutolewa bila masharti, msaada ambao ulikuja kuikomboa jamii ya waumini wa kiislamu kuepukana na njaa. Bibi Khadija alikuwa mwenye unyenyekevu mkubwa na wa pekee kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya wafuasi wa Mume wake, Kiasi hakuweza kuzuia hata Senti moja aliyokuwa nayo kujitolewa kuhudumia jamii ya kiislamu.

Dk. Sir Muhammad Iqbal (Alifariki 1938) anasema kwamba kama Muumbaji, mama ana daraja ya pili baada ya Mwenyezi Mungu mwenyewe. Kwani huleta Uhai mpya kwatika huu ulimwengu, hii inamaanisha Mama huumba; na tendo hilo- Tendo la kuzalisha uhai mpya katika maisha katika huu ulimwengu au tendo la kuumba linahitaji kujitoa muhanga (Sacrifice). Katika kuleta Maisha mapya katika ulimwengu, Mama huyaweka maisha yake binafsi katika hatari kubwa. Hivyo hufuzu hadhi na heshima kuu. Kitu kinachomsikuma Mama kuhatarisha maisha yake ni Mapenzi- mapenzi ya dhati kwa watoto wake. Mapenzi ya kweli na dhati aliyokuwa nayo Bi Khadija kwa watoto wake lilikuwa penzi tukufu na lililotakasika. Kwa utakatifu, mapenzi ya mama kwa Mtoto wake yana nafasi ya pili yakitanguliwa na Mapenzi kwa Mungu muumba.

Khadija alikuwa mama bora aliyejivunia watoto watatu- Wakiume wawili na wakike mmoja. Wakiume alikuwa ni Qassimu na Abdullah ambao wote walifariki wakiwa Wachanga. Mtoto wake wa mwisho na wa pekee aliyebakia hai alikuwa ni Fatima.

Yumkini kama Mama Kadija alikuwa ni Mama wa pekee na wa kuigwa, Basi Fatima alikuwa ni Mtoto wa kike wa pekee na wa kiigizo. Fatima, Binti bora wa Muhammad na Khadija, naye pia alikuja kuwa Mama bora na wa kuigwa. Alikuwa ni Mama wa watoto wawili wa kiume Hassan na Hussein na mabinti wawili-Zaynab na Ummu Kulthum.

Khadija na Fatima- Mama na Mwana wawili hao walikuwa ni miongoni mwa wanawake bora Wanne wa dunia hii. Wote waliitumikia kada ya Uzazi kwa Utukufu mkubwa, na kuipa heshima iliyosifika nafasi ya Mama dunia.

Wanawake hawakuheshimika bara Arabu zama zote kabla ya Uislamu. Katika jamii hiyo ya Kiarabu iliyokuwa imetawaliwa na mfumo dume, wanaume waliwafanyia ukatili mkubwa wanawake, na kuwatumikisha kama Wanyama. Ni mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (saw), aliyekuja kukomesha utumwa na unyanyasaji huo na kuwapa wanawake heshima ya juu wanayostahiki, hadhi na utukufu ambayo walipata wanawake haijawahi kutolewa katika taifa lolore wakati wowote. Kuhusu hadhi na nafasi ya Mama Mtume anasema; “Pepo ipo chini ya miguu ya kina Mama”

Hii ikimaanisha kuwa hakuna anayetamani kuingia pepopni wakati hana radhi za mama yake. Mtu kuingia peponi pamoja na mambo mengine hutegemea uwezo wa mmoja wenu kuyashinda na kupata uwokovu (salvation), na Aghalabu hakuna anayemkera na kumuudhi mama yake akapata uwokovu wa kweli hapa duniani

Hii ndio sababu Mtume wa Uislamu ameweka ni sharti la lazima mtu kupata radhi ya Mama yake- Mwanamke ndio sharti la kushinda uwokovu na kuipata pepo tukufu.

Makala hii imeandaliwa kutoka katika rejea ya Kitabu: Khadijatul kubra: Historia ya Maisha yake kilichondikwa na Sayyid Ali Ashgar Razwy na kuchapwa na Tahrike Tarsile Qur’an.

About Asadiq Media

Media for publicise the message of Wilaya under Imam Swadiq

Posted on June 12, 2019, in Habari na Matukio. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: