Aya za Quraan kuhusiana na Tukio la Ghadir Khum

Aya za Quraan kuhusiana na Tukio la Ghadir Khum
20180828091146
Aya ya kwanza: Mwenyezi Mungu anasema;

Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri. (5:67)﴿

Ayah hii ya Quraan imeshushwa kuonyesha Utawala wa Imam Ali. Suala hili pia limetajwa katika vitabu vya ndugu zetu masunni. Muandishi wa kitabu Al-Ghadir amenukuu hili katika kitabu chake Juzuu 1 Uk. 214-223 katika vitabu  thelathini.

Aya ya pili: Mwenyezi Mungu anasema

Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. (5:3)﴿

Al-Amini katika kitabu chake Al-Ghadir Juz 1 Uk. 230 amenukuu hadithi inayothibitisha uteuzi huu kimungu wa Imam Ali kutoka vitabu Sitini (60) vya Masunni

Aya ya Tatu:

Mwenyezi Mungu anasema Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea. Kwa makafiri – ambayo hapana awezaye kuizuia, Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. (70:1-3)

Ayah hii ilishuka pale mmoja wa watu alipomsikia mtume akisema, “Kwa yeyote ambaye nilikuwa kiongozi wake, Ali pia ni kiongozi wake”, mtu huyo akasema, Eeh Mwenyezi Mungu kama hili alisemalo Muhammad ni kweli, tudondoshee Mawe kutoka mbinguni Punde kidogo baada ya matamshi yake Allah akashusha mawe na kumpiga katika kichwa chake na kumuua. Kisha Allah akashusha ayah hii kwa Mtume Muhammad (saw). Muandishi Al-Amini amenukuu katika kitabu chake Al-Ghadir, Juzuu 1 Uk. 239-246 kutoka katika vitabu Sitini (60) vya kisunni.
Maswahaba kumpa mkono wa pongezi Imam Ali.

At-Tabari anasema: “Kisha watu wakaanza kusema, Ndiyo tumesikia na tunatii amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa Mioyo yetu. Wa Mwanzo kutoa mkono wa pongezi kwa Mtume na Imam Ali alikuwa ni Abu Bakr, kisha Omar, Othman, Twalha, Zubeir, Muhajirina wengine, Ansar na kisha wote waliokuwepo. Waliendelea kutoa mkono wa pongezi mpaka wakati mtume alipoongoza swala ya Jamaa ya Adhuhuri na Alasiri kwa kujumuisha. Kisha waliendelea kutoa mkono wa Pongezi mpaka ilipofika wakati wa Swala ya Magharibi na mtume akaongoza swala kwa jamaa kwa kuunganisha Magharibi na Isha. Waliendelea na zoezi hili la kutoa pongezi na kumpa mkono wa utii kwa muda wa siku tatu.”
Muandishi wa Kitabu cha Al-Ghadir amenukuu katika juzuu 1 Uk. 272 habari hii ya Omar bin Khattab kumpongeza Imam Ali kutoka Vitabu sitini (60) vya Masunni.

* Chanzo: imamreza.net

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: