Category Archives: Habari

Dk. Abouzar Ebrahimi Torkaman: Sheikh Hemedi Jalala kinara wa Mahusiano mema baina ya Dini zote Tanzania.

22_286966

Imeripotiwa katika tovuti ya Shirika hilo kuwa Mkuu wa Shirika la Utamaduni wa kiislamu na Mahusiano la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika muendelezo wa safari yake hapa nchini Tanzania alitembelea Msikiti wa Ghadir na chuo cha Seminari cha Imam Sadiq jijini Dar es Salaam na yeye akiwa miongoni mwa wanafunzi wa sayansi za kidini alisema: “umoja wa ulimwengu wa Kiislamu ni jamu muhimu lisiloepukika”.

Katika tovuti hiyo iliripotiwa kuwa, Kiongozi mkuu wa seminari hiyo na Imam wa Msikiti wa Ghadiri  Sheikh Hemedi Jalala, alipata fursa ya kuwasilisha ripoti ya kina ya kazi na Mafanikio yalioyopigwa na changamoto zake juu ya mipango na shughuli za kidini na akasema: “Sisi tunayo fahari kuwa yote tunayoyafanya ni kwa baraka na miongozo ya Kiongozi wetu wa Kiroho Ayatollah Ali Khamenei na utukufu wa Mfumo wa Wilayatul faqih.

Alisisitiza kusema: “Kwa Imani hii tuliyonayo tunapanga mambo yetu na programu zetu na tutaendelea kufanya hivyo na tumefanya mengi katika uga wa kuelimisha na kuamsha wanaseminari katika njia hii tukufu ya elimu ya dini” iliripoti tovuti hiyo.

Katika nyongeza, Sheikh Hemedi Jalala ameripotiwa kuwa alidokeza kuhusiana, uwepo wa Waislamu wenye Madhehebu tofauti tofauti hapa nchini Tanzania na kusema “Kutokana na Imani hizo tofauti miongoni mwa Waislamu, sisi daima tupo makini na suala la umoja baina yao na bado tunazidisha kuanzisha programu za mahusiano mema na mazuri baina ya Madhehebu na Dini nyingine hapa nchini Tanzania.

Dk Ebrahimi Torkaman alionyesha kuridhika na kueleza kuwa yeye kama mmoja wa Wanafunzi wa Seminari (Hawza) alikiri kuwa Shughuli za Chuo hicho zinaonyesha ukomavu wa akili wa viongozi wake na alidokeza hali mbaya ya Uislamu na Waislamu kwa sasa. Alisema: “Mafunzo ya Uislamu Asili na maadili ya kidini yanayolingania amani kwa njia ya busara yanahitajika kuzidi kutiliwa mkazo katika shughuli hizi na muhimu sana katika hali ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu”.

Mkuu wa Shirika hilo la Utamaduni wa Kiislamu na Mahusiano aliendelea: “Umoja wa ulimwengu wa Kiislamu ni dharura muhimu isiyoepukika na kile unachokifanya (Sheikh Jalala) kwa ajili ya ushirikiano na uratibu Mahusiano miongoni mwa Waislamu na dini zingine katika taifa la Tanzania ni jambo muhimu sana kwani sote tunapaswa kujitahidi kuhifadhi na kuimarisha umma wa Kiislamu ili atakapopenda Mwenyezi Mungu tushuhudie kupotea na kuangamia kabisa kwa Makundi ya misimamo mikali yenye kukufurisha na kutekeleza jinai za kigaidi duniani, ambayo mengi yametengenezwa kwa maslahi ya kumlinda Adui wa Uislamu.”

Akiendelea kupongeza hatua chanya zinazochukuliwa na mlezi huyo wa chuo cha Seminari cha Swadiq na Imam wa Msikiti wa Ghadiri, Dk Ebrahimi Torkaman Aliongeza: “mafundisho ya ujuzi wa Maarifa ya lugha lazima pia yatiliwe mkazo na yaende sambamba na lugha ya sayansi, Pamoja Juhudi zote katika  kituo hiki kitukufu cha kidini lazima kuongeza mafunzo yatakayoongeza uwezo wa kuzalisha Wataalamu waliobobea, kiroho na wenye ushawishi mkubwa kwa jamii “.

Kwa mujibu wa ripoti hii, iliyowekwa katika tovuti ya Shirika hilo Mkuu huyo wa Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu alikuwa katika safari ya nchi za Afrika kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma, kielimu na kitamaduni na Mahusiano kati ya taifa la Iran na baadhi nchi za Afrika. Kabla ya ziara katika chuo cha Imam Swadiq pia ugeni huu ulitembelea Zanzibar na baada ya ziara ya Tanzania mkuu huu ataelekea nchini Afrika Kusini katika hatua ya mwisho ya safari yake.

Imetafsiriwa kutoka:  http://en.icro.ir/

#HABARI_MARUDIO: Ajali ya kutisha: Wahanga Ndugu Haruna Elbinawi, na wengine, Mal. Haruna Shelleng na Mal. Mika’ilu Wamepata kifo cha Shahada

Habari hii ni marejeo ya habari iliyotangazwa na Khalid Idris siku ya Jumamosi, 31 July 2016

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, ndugu zetu wamepatwa na ajali mbaya jioni hii wakielekea Kaduna kutoka Abuja baada hitimisho la Mkutano siku Quds yaKimataifa.

13640745_683851788420218_3806049553037195642_o.jpg  13680208_683851825086881_9195218240067953065_o.jpg 13661943_683851845086879_284758022605516258_o.jpg

Waathirika wa ajali hiyo ni pamoja na Daktari Shuaibu Musa, Harun Al Nabawi, Mchora vibonzo wa Gazeti la Almizan Hakim Raajii Malam Mika’il Abdullahi Kaduna, Malam Haruna Shelleng, na Malam Ibrahim Potiskum.

Haruna Shelleng na Malam Mika’il walifariki kutokana na ajali, wakati wengine walipelekwa hospitali katika hali mbaya.

13659152_1230087697024478_5675163566269282594_n

Mallam Haruna Yusuf Shelleng wakati wa Uhai wake.

Mallam Haruna Yusuf Shelleng

Baada likatolewa Tangazo:
Sheikh Abdulhameed Bello Alitangaza kifo cha Mallam Haruna Yusuf Shelleng na Mallam Mika’il Abdullahi ambao walihusika katika ajali hiyo mbaya ya gari wakitoka Abuja kuelekea Kaduna wakipita njia ya mwendo kasi siku ya Jumapili Julai 31, 2016 baada ya kuhudhuria Mkutano wa Semina ya siku ya Quds ya Kimataifa huko Abuja.

Mallam Haruna Yusuf Shelleng

Wengine ambao wanaendelea na matibabu hospitali wakiwa katika hali tofauti tofauti ni pamoja na Dr. Shu’aibu Musa, Mallam Ibrahim Muhammad Potsikum na Mallam Haruna El-Binawi Sala ya mazishi ya marehemu wawili (2) ilifanyika Barabara ya Gombe, Kaduna nyumbani kwa Mallam Mika’il na na baadaye miili yao ikahamishiwa katika Makaburi ya Mashahid ‘Darur Rahman’, yaliyopo Dembo Kijiji Zaria kwa maziko. Watu hao watano (5) ni wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Mwaka siku ya Quds ya Kimataifa nchini Nigeria.

Mazishi ya ndugu yetu Mallam Haruna Yusuf Shelleng

   

Uongozi wa Hawza Imam Swadiq na Masjid Ghadir chini ya Mlezi wake Mawlana Sheikh Hemedi Jalala unatoa mkono wa Rambi rambi kwa Mujahidina wote waliopoteza maisha yao katika Ajali hiyo mbaya na kuwapa pole familia za Wafiwa na Uongozi mzima wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria chini ya Kiongozi wake Sheikh Ibrahim Zakzaky. Vile vile Unawaombea dua majeruhi wote wapate Shifaa ya Haraka kwa majeraha yao na  Allah awape Afya na nguvu ili kuendeleza utumishi ulotukuka kwa Imam wetu wa Zama.

INNALILLAHI WA INNA’ILAHIR RAJI’UN

Chanzo: http://imnig.org/

MAHUSIANO BAINA YA DINI KATIKA KUDUMISHA AMANI

MAHOJIANO NA CITIZEN TV  KUHUSU MAHUSIANO BAINA YA WAISLAMU NA DINI 12631490_814920438617953_1352665887689457416_nNYINGINE KATIKA KUDUMISHA AMANI.

Adhuhuri ya  03/02/2016 Maulana Samahat Sheikh Hemed Jalala alitembelewa ofini kwake jijini Dar es Salaam na mwanahabari Samwel Mwalogo wa CITZENTV ya Kenya na kufanya mahojiano kuhusiana na swala la mahusiao ya waislamu na na dini zingine khususan wakiristo katika kuijenga amani ya nchi.

Maulana Samahat Sheikh Hemed katika kuelezea mahusiano hayo ambayo alisema ni msingi mkuu wa kudumisha amani alianza na aya ya Quraan inayosema :

“Hakika tumekuumbeni miongoni mwa wanaume na wanawake, na tukawafanyeni kuwa mataifa na makabila mbalimbali…..” Quraan.

Maulana Samahat Sheikh Hemed Jalala alielezea na kusema:

“Amani inapatikana katika msingi wa kuzikubali tofauti zetu, kukubali tofauti za makabila na mataifa na huku tukiunganishwa na msingi wa asili moja, asili moja ya kwamba tunatokana na baba mmoja. Hivyo pamoja na tofauti za kidini,kikabila na mataifa pia bado sisi ni ndugu. Imam Ali ambae ni mmoja wa viongozi wa waislamu akimuusia mwanafunzi na swahaba wake Maalik Al-ashtar alimwambia :”WATU NI WA AINA MBILI, IMMA NDUGU YAKO KATIKA DINI AU MWENZAKO KATIKA MAUMBILE”. Hivyo tunaweza kuwa ndugu kwa kuwa tunatoka katika dini moja, Tunaweza kuwa ndugu kwa kuwa sisi ni Waislamu au tunaweza kuwa ndugu kwa kuwa sisi ni Wakiristo au mbali ya hivyo vyote sisi ni ndugu kwa kuwa tunaasli moja, sisi sote ni binadamu tunatokana na baba mmoja ambae ni Adamu a.s”.

Maulana Sheikh Hemed Jalala aliendelea kuelezea mahusiano kama msingi wa kuiboresha amani ya nchi na khususan Tanzania yetu na akasema:

“Dini zote zenye vitatabu kutoka mbinguni kama Injil na Quraan zinausia swala zima la maelewano na kukaa pamoja, hakuna dini wala mtume aliyewahi kutumwa na Allah kwa ajili ya kuja kuwavuruga watu ili wasikae mahala pamoja, na ukisoma vitabu hivi vitakatifu utagundua vyote vinalingania Umoja na Amani kwa ujumla, ndipo utapata mtume wa Uislamu alikaa na Wakiristo na Mayahudi, aliishi nao na alifanya nao vikao katika miji ya madina na Makka na kufikia kuwekeana mikataba ya Amani baina ya mtume Muhammad s.a.w.w na wasiokua waislamu miongoni mwa mayahudi na wakiristo juu ya kulindana na kuienzi amani ,moja ya masharti yaliyoandikwa katika mkataba huo ni IKIWA YAHUDI AU MKIRISTO ATASHAMBULIWA BASI WAISLAMU WATAWAJIBIKA KUMHAMIna kwa upande wa Waislamu vivyo hivyo wakishambuliwa Wakiristo na Mayahudi watawajibika kuwahami ”.

Maulana Sheikh Hemed Jalala aliendelea na akaongeza kusema:

“Hapa katika makubaliano haya Mtume wa Uislamu anatufundisha jambo kubwa kuhusiana na Amani na swala zima la kuvumiliana kiitikadi, kuishi pamoja na kuienzi amani bila kujali tofauti za dini zetu, yote hii ni kwa kuwa amani ni tunu ambayo ikipotezwa kurudishwa kwake inagharimu mno na pengine isiwezekane, Hivyo ninasema kwa msingi huu wa amani juu ya mahusiano, basi MAHUSIANO BAINA YA WAISLAMU NA WAKIRISTO NI WAJIBU, kwani uislamu ni dini ya amani na ndio maana Quraan tukufu inasema juu ya kuienzi amani na kupinga umwagaji wa damu“ATAKAEUWA MTU BILA KUWA MTU HUYO AMEUA BASI NI KAMA AMEUA WATU WOTE””.

Maualana Sheikh Hemed Jalala aliendelea kusema :

“Patakapopatikana kundi lolote linalovunja amani huku likijinasibisha na Uislamu, jua hilo kundi sii kundi la kiislamu kwani hakuna uislamu usiokuwa wa amani, na vile vile wanaojinasibisha na ufuasi wa mitume wengine kama Nabii Issa na wengine kasha wakamwaga damu na kuvunja misingi ya amani basi hao si wafuasi wa dini yeyote ya mbinguni.”

Tumeshuhudia yanayoendelea duniani, miongoni mwao ni umwagaji wa damu kwa jina la dini na matendo ya kigaidi, yote hayo hayawezi kunasibishwa na dini kwani hakuna Mungu anaetuma au kuamrisha vita na umwagaji damu kwa dhuluma.

Mwisho Maulana Sheikh Hemed Jalala alisema:

Amani mnayoiona hapa nchini ni kwa sababu ya viongozi wa dini katika mimbari na madhabahu zao kuzungumzia na kuomba amani, waumini wanapata maelekezo mazuri kutoka kwa viongozi wa dini juu ya kuilinda amani na jinsi ya kuenzi kupitia mahusiano mazuri katika jamii.

Imehaririwa na kitengo cha Habari,

Asadiq Media, Hawza Al-Imam Swadiq a.s, Dar es Salaam Tanzania.

EMAIL: asadiqmedia@gmail.com

YOUTUBE: https://youtube.com/asadiqmedia.

TEMBELEA UKURASA RASMI: https://www.facebook.com/SheikhHemediJalala/

 

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: