Category Archives: Hotuba na Mawaidha

Ujumbe, Maarifa, Elimu kuhusiana na Dini na Maisha

KWA NINI UISLAMU UNAHARAMISHA RIBA NA KUHIMIZA SADAKA.

Mwandishi: Dr. Zafar Bangash.
(Crescent International, June 2016)

Katika Qur`ani Tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuelezea Uislamu kama ni dini (din). Hakuna mahali popote ambapo neno madhehebu (madhhab)limetumika kwa ajili ya hilo. Kuna tofauti? Dini (Din) maana yake ni njia kamili ya maisha ikiwa na mpangilio wake wa kanuni na maadili ambayo humwezesha mtu kuishi maisha yake hatika duniani hii. Kufuatana na mtazamo wa Kiislamu, dini inawakilisha maisha ambayo msingi wake umewekwa kwenye maadili na kanuni za Kiislamu; pia panaweza kuwepo dini nyinginezo ambazo misingi yake imewekwa juu ya kufuru. Madhehebu, kwa upande mwingine ni neno takriban linaloweza kutafsiriwa kama dini.

riba

kwanini uislamu unaharamisha riba na kuhimiza sadaka

Neno religion mbalo linatafsirika kama dini lina maana finyu sana ambayo mara nyingi huhusisha vitendo vya ibada tu. Hivyo, Ukristo, Uyuda na mifumo mingine mingi ya imani inaweza kuwekwa kwenye kundi la “dini” kwa sababu mifumo hii kimsingi inajihusisha na vitendo vya ibada bila kutoa mwongozo mahususi juu ya ni jinsi gani maisha kwa ujumla yanaweza kuamriwa au kutawaliwa. Hii ni dhahiri na wazi zaidi katika nchi zenye Wakristo wengi ambazo zimechagua kutenganisha baina ya kanisa na serikali. Uislamu haukubaliani na utenganishi wa namna hiyo na kwa hiyo, mfumo huo hauwezii kuitwa dini “religion” pamoja na kwamba Waislamu wengi hufanya kosa hili bila kujua.

Katika Uislamu, mtu binafsi, ambaye anaitwa binadamu (insan) katika Qur`ani Tukufu, yupo chini ya uangalizi wa wema na upendo wa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu amemuumba binadamu sio tu katika umbo bora la maumbile (95:4) lakini pia aliweka mwongozo katika namna ya ufunuo (wahyi) kwamba aliahidi wakati ule hasa alipompeleka Adam na mkewe (a.s.) hapa duniani, “…….na kama ukiwafikia uongozi wangu basi watakaoufuata mwongozo wangu, haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.” (2:38).

Qur`ani Tukufu yote kama ilivyoelezwa kwa mifano na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika maisha yake yote yaliyobarikiwa inatoa mwongozo kwa ajili yetu sisi katika safari yetu yenye ukaidi kupitia katika dunia hii. Katika Siku ya Hukumu ambapo kila mtu itambidi ajibu kuhusu vitendo vyake mwenyewe, maisha ya hapa duniani lazima yaendeshwe kama mjumuiko. Wanadamu ni viumbe wa kijamii wenye kushirikiana; huwa wanawahitaji binadamu wengine wa kuishi na kuamiliana nao. Hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametoa mwongozo kwa ajili ya tabia katika ngazi ya mtu binafsi, familia, jumuiya, na serikali. Kuna sheria zinazohusu halali (yanayoruhusiwa) na haramu (yanayokatazwawa) katika mwenendo wa mtu binafsi na maingiliano ya kijamii na katika kuendesha shughuli.

Wakati ambapo Waislamu wametengeneza sehemu kubwa ya maandiko ambayo yameegemezwa kwenye Qur`ani Tukufu, Sunnah na Sirah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuhusu mambo yao ya kijamii, kitamaduni, na kisiasa, lakini katika nyanja ya uchumi, maandishi yaliyopo ni machache sana. Mbali na madai mepesi kama vile, “riba ni haramu” yaani kulinganisha faida na riba, na kujaribu kuleta sheria ya makubaliano ya rehani (mara nyingi kwa kutumia njia zenye kutia wasiwasi), hususani kwa Waislamu waishio nchi za Magharibi, kuna mapungufu katika uelewa wa wazi kuhusu ni jinsi gani mifumo ya uchumi na benki ya Kimagharibi inavyofanya kazi.

Na tuanze na kuangalia Qur`ani Tukufu inasema nini kuhusu riba. Katika Sura ya Baqarah , Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuonya:

“Ambao wanakula riba, hawainuki, ila kama ainukavyo aliyezugwa na shetani kwa wazimu. Hayo ni kwa sababu wanasema kuwa biashara ni kama riba. Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara na ameharamisha riba. Na aliyefikiwa na na mawaidha kutoka kwa Mola wake, akakoma, basi yake ni yaliyokwishapita na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wanaorejea, basi hao ndio watu wa motoni; wao ni wenye kukaa humo milele. Mwenyezi Mungu huipunguza riba na huizidisha sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila kafiri afanyae dhambi.” (2:275-276).

Uharamisho wa Qur`ani Tukufu juu ya riba uko wazi. Katika aya zinazofuata (2:278-279) Mwenyezi Mungu Mtukufu anatangaza kwamba wale wanaojiingiza katika kula riba ni “…basi jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake…..” Pia zipo hadithi nyingi zinazohusu uharamisho wa riba na miongoni mwa hadithi hizo moja inatosha kwa lengo letu. Katika Sahih Muslim, Abu Dawud, na al-Tirmidhi, Jabir ibn Abdullah anasimulia hadithi ifuatayo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):

“Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (s.a.w.w.) amewalaani wanaopokea riba, wanaofanya biashara ya riba, (wakopeshaji na wakopaji kwa riba), wale wanaoshuhudia mapatano ya riba, na wale wanaosajili biashara za riba. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema, ‘Wote hao ni washiriki.”’

Kwanza tuelewe riba ina maana gani. Katika maana ya kilugha, riba maana yake ni nyongeza au ongezeko la kitu juu na zaidi ya kiwango au idadi yake ya mwanzo. Kwa kawaida hutumika kwa fedha inayokopeshwa kwa mtu fulani na kiasi fulani cha ziada kilipwe juu na zaidi ya kiasi halisi kilichokopeshwa. Dhuluma iliyopo katika mpango kama huu iko wazi; mkopaji ni muhitaji na wakati ambapo kiasi halisi cha mwanzo cha mkopeshaji kinahakikishwa pamoja na kiasi cha nyongeza, haizingatii hali au uwezo wa mkopaji. Hakuna hatari wala shaka kwa mkopeshaji; lakini tatizo lipo kwa mkopaji tu. Qur`ani Tukufu inazungumzia jambo hili kwamba kiasili ni udhalimu.

Lazima pia tuzingatie akilini kwamba aya inayoharamisha riba inafuata mara tu baada ya fungu la aya zinazohimiza kutoa sadaka kwa hiari kuwapa wenye kuhitaji na masikini bila ya kutaka chochote kutoka kwa mpokeaji. Sadaka ni zaidi ya zaka, ambayo ni wajibu kwa wale wenye uwezo.

Riba imekuwepo takribani tangu dahari lakini imekuwa na madhara zaidi tangu ujio wa ustaarabu wa Kimagaharibi kufuatana na mfumo wake wa kibenki na jinsi fedha inavyotengenezwa. Ni utando mpana sana wa buibui ambamo kila mtu amekuwa mfungwa. Mfumo huu umeandaa mazingira ya kuchukua fedha kutoka kwa watu masikini na kuzidi kuwatajirisha ambao tayari ni matajiri. Sio jambo la kushangaza, taarifa ya shirika la misaada la Uingerza-Oxfam ya Januari mwaka 2016 kwa mara nyingine likithibitisha jambo hili. Uchunguzi wake huo ulitolewa usiku wa Kongamano la Uchumi la Dunia, huko Davos nchini Uswisi lililofanyika kuanzia tarehe 20-26, Januari, 2016, iligundua kwamba familia 62 zilizo tajiri kupindukia hapa duniani zinahodhi utajiri mwingi ambao unawatosha nusu ya idadi ya watu masikini sana duniani, ni kwamba utajiri huo ni sawa na utajiri wa watu bilioni 3.5.

Fedha ni kitu gani, na nani anayetengeneza fedha na huzitengeneza namna gani? Katika msingi wake mkuu hasa fedha ni chombo cha mabadilishano; hakina thamani ya asili na lengo lake ni kurahisisha biashara ya bidhaa mbalimbali. Kama tungekuwa tunaishi katika dunia rahisi yenye waoka mikate na wafuga kuku tu, labda tusingehitaji fedha. Muoka mikate angeweza kufanya makubaliano ya kubadilishana na mfuga kuku ili apate idadi fulani ya mayai kwa boflo la mkate. Vivyo hivyo, muoka mikate angetoa idadi fulani ya mikate kwa mfuga kuku ili apate kuku moja. Lakini wapi! Dunia imekuwa na utata sana kuliko hivyo. Tunahitaji kula mbogamboga na matunda, nguo za kuvaa, nyumba za kuishi na magari ya kuendesha. Kwa kuongezea hayo ni mahitaji ya kompyuta, simu za mkononi na vitu vingine vingi sana na taswira inakuwa na utata zaidi kueleweka. Hivyo, muoka mikate asingeweza kufika mbali sana kama ingembidi kuchukua lori lililojaa mikate na kwenda dukani kununua kompyuta ndogo ya kupakata!
Tunahitaji fedha kurahisisha biashara kama hizo. Zamani, watu walitengeneza sarafu za dhahabu na fedha kwa ajili ya biashara za kila siku. Baadaye, fedha ya karatasi ilianzishwa, inayoitwa waraka wa ahadi au hawala. Wakati sarafu za dhahabu na fedha zilikuwa na thamani ya madini, fedha ya karatasi haina chochote, lakini mfumo wa kibenki wa kisasa ambao umeegemezwa kwenye riba umeanzisha thamani ya fedha ya karatasi pia!

Ni vipi na ni nani anayechapisha fedha? Mwanzoni fedha ya karatasi iliegemezwa kwenye hifadhi ya dhahabu. Kwa kuwa dola ya Kimarekani imekuwa hifadhi ya fedha ya kidunia kuanzia Vita Kuu vya Pili vya Dunia na kuendelea, bei ya dhahabu ilikadiriwa kuwa dola za Kimarekani 35 kwa wakia moja. Mwaka wa 1971, serikali ya Marekani kwa kujiamulia yenyewe iliondosha muunganiko wa dola kwenye dhahabu. Kwa hakika, bei ya dhahabu imepanda haraka sana. Leo hii bei ya dhahabu ni takribani dola 1,200 kwa wakia moja.

Kinyume na jinsi watu wengi wanavyoamini, serikali hazitengenezi fedha; benki ndizo zinazotengeneza fedha, hususani Benki ya Marekani iitwayo “Federal Reserve Bank.” Benki hii haipo katika umiliki au udhibiti wa serikali; benki hii inamilikiwa kibinafsi yenye bodi yake yenyewe ya wakurugenzi. Kwa bahati mbaya hata Wamarekani walio wengi hawaujui mpango huu. Kwa kuwa dola ya Kimarekani ndio hifadhi ya fedha ya dunia (64% ya akiba ya fedha za kigeni za dunia zimeshikiliwa katika dola za Kimarekani), maamuzi yanayofanywa na Federal Reserve Bank ya Marekani, huathiri dunia nzima.

Hii ni sehemu moja ya tatizo. Sehemu nyingine ya tatizo, ambalo ni baya zaidi ni utengenezaji wa fedha. Hapa ndipo mkono wa kishetani unapofanya kazi, kama Qur`ani Tukufu inavyoueleza “Ambao wanakula riba, hawainuki, ila kama ainukavyo aliyezugwa na shetani kwa wazimu….”(2:275). Inaweza kuelezewa vizuri zaidi kwa kufikiria mfano.

Chukulia kwamba mtu binafsi angeweka akiba ya dola 100,000 za Kimarekani katika benki. Kwa msingi wa akiba hii, benki inaweza kukopesha dola laki tisa (900,000). Hii sio fedha halisi; inaweza kuelezewa kama “fedha ya manufaa” – (Virtual money) Benki inaifahamisha serikali ichape dola laki tisa (900,000). Fedha hizi zinazoitwa “waraka wa ahadi” ni ahadi na hazina thamani kwa sababu hizo sio fedha halisi lakini benki hukopesha fedha hizi nyingi kwa watu na pia kwa makampuni.

Jambo hili hufanyika kwa dhana kwamba 10% tu ya fedha iliyowekwa akiba katika benki ndiyo itakayochukuliwa. Katika mfumo na msamiati wa kibenki, hii inarejelewa kama akiba ya hesabu ya sehemu. Hivyo fedha inayoitwa “waraka wa ahadi” inayokopeshwa na benki huwa fedha halisi wakati wakopaji wanapolipa fedha hiyo kwa kuipata kupitia kazi ngumu.

Wakati Benki inapopokea $900,000 zikiwa fedha halisi ambazo ilizikopesha mapema mwanzoni kama hawala, sasa inaweza kukopesha $ milioni 8.10 (kwa mara nyinginetena kama hawala) kwa sababu kwa mujibu wa akiba ya hesabu ya sehemu inayotakiwa, benki inapaswa kuweka 10% ya kiasi cha fedha inayokopeshwa kwenye akiba. Baada ya muda mrefu, jinsi mzunguko wa kukopesha na kuweka akiba unavyoendelea, jumla ya kiasi kinachokopeshwa huanza kukua na inaweza kuwakilishwa kwa mlolongo usiokoma wa punguzo la polepole (kwa 10%). Kwa kila amana iliyowekwa, mara 9 ya kiasi cha mwanzo hutolewa kama mkopo hivyo kutengeneza piramidi kubwa ya utajiri unaoongezeka kwenye benki na wenye hisa wake kupitia kazi ngumu ya watu wa kawaida.

Huu ndio utapeli unaofanyakazi leo na umeigeuza takriban dunia yote kuwa watumwa isipokuwa kundi dogo la watu wachache sana walioko huko juu. Hivi ni jambo la kushangaza kwamba kupitia lundo lote la maelezo magumu na yenye utata, watu wanafanywa wakubaliane na udanganyifu huu ili kwamba hao watu wachache waweze kutajirika haraka kwa kunyanyua kidole tu kumfanya mkopaji asaini kwenye msitari wa chini wa mkataba wa mkopo bandia.

Katika miaka ambamo mfumo wa akiba ya hesabu ya sehemu umetumika, sasa umekuwa ndio mfumo wenyewe wa kibenki na mambo ya fedha usiopingika duniani kote. Njia pekee ya Waislamu na watu wengine dhaifu (mustadhafa) ya kujikomboa kutoka kwenye mtindo huu wa kishetani ya deni ni wao kurejesha tena mamalaka ya utendaji ya Kiislamu yenye mwelekeo wa haki na kujenga mfumo wa uchumi unaoendana na kanuni pana za Qur`ani Tukufu juu ya haki za kijamii na mgawanyo wa utajiri.

Zafar Bangash.
(Crescent International, June 2016)

IFAHAMU TAWHIDI YA KIISLAMU


Katika mambo yanayotatiza waislamu na kupelekea kuitana makafiri au washirikina na watu wa bidaa ni mafhumu isiyo sawa kuhusu Maana ya Tawhidi na maana ya shirk. Katika darasa hii Maulana Sheikh Hemedi Jalala ameelezea maana ya Tawhidi na kujaribu kuainisha makundi ya Tawhidi.

Wosia wa Bibi Fatimah Zahra kwa Imamu Ali (A.S)

Wosia wa Bibi Fatimah Zahra kwa Imamu Ali (A.S)

Imamu Ali (A.Ş.) alishangazwa kuona kwamba mke wake mpendwa alimuacha kitandani na kuanza kufanya kazi za nyumbani; alimuuliza kuhusu hilo na yeye alijibu:

“Hii ni siku ya mwisho ya maisha yangu. Nataka kuosha nywele za watoto wangu na nguo zao, kwa sababu hivi karibuni watakuwa mayatima, bila mama !!”

Kisha Imamu Ali (A.Ş.) aliuliza kuhusu chanzo cha wa habari hii (siku ya kuondoka kwake). Na yeye (A.S.) alimwambia kwamba alimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu katika ndoto yake naye mtume ndiye alimweleza kuwa usiku wa leo anakwenda kukutana naye. kisha Bi Fatima akamtaka Imamu Ali (A.Ş.) kutekeleza usia wake.

Imam Ali akasema: “Nielekeze kufanya kitu chochote unachotamani, binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” kisha Ali (A.S.) aliwaamuru watu wote kutoka nje ya nyumba naye akaketi karibu naye.

Fatima alianza kwa kusema:

msiba wa bibi fatima

“Binamu, wewe huna desturi ya kuwa muongo, wala Muasi, au mimi hakuna siku niliwahi kuacha kukutii tangu niwe mshiraka wako katika Maisha?”

Ali akasema:

“Mwenyezi Mungu apishe mbali !! Wewe unajulikana zaidi na Mwenyezi Mungu, Ni mchamungu zaidi, na mwenye kujitolea, na heshima zaidi na umezidi katika kumuogopa Mwenyezi Mungu kuliko (kunipa sababu). Hakika ni uchungu na maumivu yaliyoje kwangu mimi kutengana na wewe na kukupoteza wewe;. lakini (kifo) ni marejeo yasiyoepukika. Wallahi unayafanya mapya majonzi yangu kwa kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu; hakika kifo chako na kuondoka kwako utakuwa ni msiba mkubwa, lakini ‘kwa Mwenyezi Mungu sisi sote ni wake, na kwake tutarejea.’ “

Ni uchungu, maumivu na huzuni namna gani. Hakika huu ni utakuwa ni msiba ambao hakuna kuniliwaza, na yatakuwa ni maafa ambayo hakuna fidia. “

Basi wote wawili walilia sana na Imamu Ali (A.Ş.) akakikumbatia kichwa cha Bi fatima na kusema:

Nielekeze cha kufanya kitu chochote unachotamani; hakika utanipata mimi ni mwenye kujitolea nami nitatekeleza kila kitu utakachoniamuru kufanya. Nami pia nitayaweka mambo yako juu ya dhima yangu..”

Yeye Fatima (A.S.) akasema:

“Namuomba Mwenyezi Mungu akulipe mema Binamu, kwanza naomba baada ya kifo changu umuoe, mpwa wangu Umamah; Hakika yeye atakuwa kwa watoto wangu kama mimi nilivyokuwa. Mbali ya hivyo, watu hawawezi kuishi bila mwanamke..”

Fatima (A.Ş.) kisha aliongeza:

“Ninakuomba kutoruhusu mtu yeyote ambaye alinitendea uovu kushuhudia mazishi yangu, kwa hakika hao ni maadui zangu, na adui wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Pia usiwape wao nafasi ya kuniswali, wala wafuasi wao. Uzike mwili wangu usiku wakati macho ya watu yamelala. “

Akisherehesha hotuba Imamu Ali baada ya mazishi ya Fatima, Mshereheshaji katika Nahjul Balagha toleo la Kiingereza iliyochapishwa na Mchapaji Ansariyan, Uk.347 – aliandika:

“Aliyofanyiwa binti ya Mtume baada ya kifo chake yamekuwa ni machungu sana na huzuni. Japo Sayyedah Fatima (as) hakuishi katika dunia hii zaidi ya miezi michache baada ya kifo cha Mtume (SAW), lakini hata kwa kipindi hiki kifupi kimejaa hadithi ya muda mrefu ya huzuni na majonzi (juu yake). katika muunganiko  huo, tukio la kwanza lililoshangaza macho ya watu ni maandalizi ya mpango wa ibada ya mazishi ya Mtume yakiwa bado hayajakamilika pale ushindani na upinzani wa madaraka ulipoanza katika ukumbi wa Saqifa Bani Sa’ida. Watu wakauacha mwili wa Mtume (bila kuuzika), tendo hilo lazima lilimjeruhi na kumuumiza Bi Fatima na kumsababibishia majonzi makubwa moyoni kuona kwamba wale waliodai kumpenda na kushikamana (na Mtume) wakati wa uhai wake, wameshughulishwa na kugombea Madaraka na utawala na kusahau kumliwaza binti pekee wa mtume, Hawakujua hata ni wakati gani Mwili wa Mtume (saw) ulioshwa na wakati gani ulizikwa; na njia pekee waliyomliwaza nayo Biti huyu pekee wa Mtume ni kuizingira nyumba yake na  vifaa vya kuchoma nyumba kwa kutaka kulazimisha kupewa Mkono wa utii (Baiya) kwa nguvu na kwa kuonyesha ukatili, na uovu mkubwa. Ulafi huo wote wa madaraka ulikuwa ni kwa lengo la kuipindua nafasi tukufu na ya kifahari ya nyumba hii ya mtume kwamba huenda isibakie nyumba tukufu wakati wote.

Kwa lengo hilo hilo na kwa mtazamo huo huo, ili kuponda nafasi yake ya kiuchumi, madai yake (Bi fatma) kwa (Urith wake) wa Fadak yalitupiliwa mbali na kukataliwa kwa kisingizio kuwa ni madai ya uongo, athari ambayo ilimfanya Bi Fatima (as) kuacha Usia wa kifo chake kuwa asiruhusiwe yeyote miongoni mwao kuhudhuria Mazishi yake. “

Fatima Binti wa Muhammad alikuwa tayari kukutana na Bwana wake. Alioga, kisha akajilaza katika tandiko lake… kisha akamuelekeza Asmaa bint Umais kusubiri muda na kisha amuite jina lake; kama hatomjibu, hii ina maana yeye (A.Ş.) kashaondoka kuelekea kwa Bwana wake.

Asma alisubiri kitambo kidogo, kisha akaliita jina la Fatima … lakini hapakuwa na jibu;

Asma alirudia wito:

“Ee binti wa mteule Muhammad!

Ee binti wa mtu mwenye heshima ambapo wanawake hawajazaa mfano wake!

Ee binti wa mbora ya wale ambao walitembea juu ya changarawe!

Ee binti yake yule ambaye alikuwa kati ya ‘umbali miwili

 {Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi “(Qur’an aya, (53: 9)}

… Hakukua na jibu … ukimya ulitawala nyumba nzima … Asmaa kisha akamsogelea Fatima na kumkuta kesha fariki.

Katika hatua hiyo, Hassan na Hussein wakaingia na kumuuliza:

“Yuko wapi mama yetu?”

Hata hivyo Asma hakutamka neno!

Hassan na Hussein waliuendea mwili wa mama yao na kukuta ameshakufa; ndipo Hussein alipomgeukia Hassan na kusema:

”Allah atupe faraja kwa kuondokewa na Mama yetu”

wakati huo Imam Ali alikuwa Msikitini. Hassan na Hussein wakaelekea Msikitini na kutangaza habari ya Msiba kwa baba yao. Mara aliposikia maneno yao, alianguka na Kuzimia. Alipopata fahamu alisema:

Ni nani atakayenifariji sasa hivi, Binti wa Muhammad? Ulikuwa ukiniliwaza, ni nani basi atakayeichukua nafasi yako?

Wanawake wa ukoo wa Hashim wakakusanyika kupata habari za msiba mkubwa…ndio ni msiba mwingine umewakumba kwa mara nyingine wakati damu ingali ikichuruzika kwa majeraha ya kuondokewa na Mtume…

Mji wa Madina ukitetema…

Kila mtu alikuja kumfariji Ali (a.s) na wanawe wawili… Wakisema Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, watoto wa Zahra…

Ilikuwa ni jana tu mlikumbwa na msiba mkubwa wa Baba yenu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Msiba huu mpya hauna nafuu kuliko wa Mwanzo! Lakini tunawausia kusubiri kwani haya ni Matakwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na muweza wa kila kitu.

Rejea Kitabu Fatima (S.A) The Gracious kilichoandikwa na Abu Muhammad Ordoni


AsadiqMedia,

Kitengo cha Habari Hawza Imam Swadiq (a.s).

B.pepe:asadiqmedia@gmail.com.
Tovuti:imamswadiq.com/

 

 

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

The Pilgrim Log

Helping you live your daily pilgrimage

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: