Category Archives: Media na Rekodi

Sauto, rekodi na Picha mbalimbali za Harakati

MAHUSIANO BAINA YA DINI KATIKA KUDUMISHA AMANI

MAHOJIANO NA CITIZEN TV  KUHUSU MAHUSIANO BAINA YA WAISLAMU NA DINI 12631490_814920438617953_1352665887689457416_nNYINGINE KATIKA KUDUMISHA AMANI.

Adhuhuri ya  03/02/2016 Maulana Samahat Sheikh Hemed Jalala alitembelewa ofini kwake jijini Dar es Salaam na mwanahabari Samwel Mwalogo wa CITZENTV ya Kenya na kufanya mahojiano kuhusiana na swala la mahusiao ya waislamu na na dini zingine khususan wakiristo katika kuijenga amani ya nchi.

Maulana Samahat Sheikh Hemed katika kuelezea mahusiano hayo ambayo alisema ni msingi mkuu wa kudumisha amani alianza na aya ya Quraan inayosema :

“Hakika tumekuumbeni miongoni mwa wanaume na wanawake, na tukawafanyeni kuwa mataifa na makabila mbalimbali…..” Quraan.

Maulana Samahat Sheikh Hemed Jalala alielezea na kusema:

“Amani inapatikana katika msingi wa kuzikubali tofauti zetu, kukubali tofauti za makabila na mataifa na huku tukiunganishwa na msingi wa asili moja, asili moja ya kwamba tunatokana na baba mmoja. Hivyo pamoja na tofauti za kidini,kikabila na mataifa pia bado sisi ni ndugu. Imam Ali ambae ni mmoja wa viongozi wa waislamu akimuusia mwanafunzi na swahaba wake Maalik Al-ashtar alimwambia :”WATU NI WA AINA MBILI, IMMA NDUGU YAKO KATIKA DINI AU MWENZAKO KATIKA MAUMBILE”. Hivyo tunaweza kuwa ndugu kwa kuwa tunatoka katika dini moja, Tunaweza kuwa ndugu kwa kuwa sisi ni Waislamu au tunaweza kuwa ndugu kwa kuwa sisi ni Wakiristo au mbali ya hivyo vyote sisi ni ndugu kwa kuwa tunaasli moja, sisi sote ni binadamu tunatokana na baba mmoja ambae ni Adamu a.s”.

Maulana Sheikh Hemed Jalala aliendelea kuelezea mahusiano kama msingi wa kuiboresha amani ya nchi na khususan Tanzania yetu na akasema:

“Dini zote zenye vitatabu kutoka mbinguni kama Injil na Quraan zinausia swala zima la maelewano na kukaa pamoja, hakuna dini wala mtume aliyewahi kutumwa na Allah kwa ajili ya kuja kuwavuruga watu ili wasikae mahala pamoja, na ukisoma vitabu hivi vitakatifu utagundua vyote vinalingania Umoja na Amani kwa ujumla, ndipo utapata mtume wa Uislamu alikaa na Wakiristo na Mayahudi, aliishi nao na alifanya nao vikao katika miji ya madina na Makka na kufikia kuwekeana mikataba ya Amani baina ya mtume Muhammad s.a.w.w na wasiokua waislamu miongoni mwa mayahudi na wakiristo juu ya kulindana na kuienzi amani ,moja ya masharti yaliyoandikwa katika mkataba huo ni IKIWA YAHUDI AU MKIRISTO ATASHAMBULIWA BASI WAISLAMU WATAWAJIBIKA KUMHAMIna kwa upande wa Waislamu vivyo hivyo wakishambuliwa Wakiristo na Mayahudi watawajibika kuwahami ”.

Maulana Sheikh Hemed Jalala aliendelea na akaongeza kusema:

“Hapa katika makubaliano haya Mtume wa Uislamu anatufundisha jambo kubwa kuhusiana na Amani na swala zima la kuvumiliana kiitikadi, kuishi pamoja na kuienzi amani bila kujali tofauti za dini zetu, yote hii ni kwa kuwa amani ni tunu ambayo ikipotezwa kurudishwa kwake inagharimu mno na pengine isiwezekane, Hivyo ninasema kwa msingi huu wa amani juu ya mahusiano, basi MAHUSIANO BAINA YA WAISLAMU NA WAKIRISTO NI WAJIBU, kwani uislamu ni dini ya amani na ndio maana Quraan tukufu inasema juu ya kuienzi amani na kupinga umwagaji wa damu“ATAKAEUWA MTU BILA KUWA MTU HUYO AMEUA BASI NI KAMA AMEUA WATU WOTE””.

Maualana Sheikh Hemed Jalala aliendelea kusema :

“Patakapopatikana kundi lolote linalovunja amani huku likijinasibisha na Uislamu, jua hilo kundi sii kundi la kiislamu kwani hakuna uislamu usiokuwa wa amani, na vile vile wanaojinasibisha na ufuasi wa mitume wengine kama Nabii Issa na wengine kasha wakamwaga damu na kuvunja misingi ya amani basi hao si wafuasi wa dini yeyote ya mbinguni.”

Tumeshuhudia yanayoendelea duniani, miongoni mwao ni umwagaji wa damu kwa jina la dini na matendo ya kigaidi, yote hayo hayawezi kunasibishwa na dini kwani hakuna Mungu anaetuma au kuamrisha vita na umwagaji damu kwa dhuluma.

Mwisho Maulana Sheikh Hemed Jalala alisema:

Amani mnayoiona hapa nchini ni kwa sababu ya viongozi wa dini katika mimbari na madhabahu zao kuzungumzia na kuomba amani, waumini wanapata maelekezo mazuri kutoka kwa viongozi wa dini juu ya kuilinda amani na jinsi ya kuenzi kupitia mahusiano mazuri katika jamii.

Imehaririwa na kitengo cha Habari,

Asadiq Media, Hawza Al-Imam Swadiq a.s, Dar es Salaam Tanzania.

EMAIL: asadiqmedia@gmail.com

YOUTUBE: https://youtube.com/asadiqmedia.

TEMBELEA UKURASA RASMI: https://www.facebook.com/SheikhHemediJalala/

 

Ziara ya Tabligh: Komkonga Handeni Tanga

Picha za msafara wa Tabligh katika kijiji cha komkonga -Handeni -Tanga, ziara iliwakutanisha Masheikh na Mubalighina kutoka Hawza imam swadiq na mamia ya wakaazi wa wilaya ya Handeni siku ya Jumanne na Jumatano ya Tarehe (24, na 25 mwezi wa Sita, 2014). Lengo la ziara ni kuamsha umma wa kiislamu na kuwakumbusha majukumu yao hususani udugu baina yao ushirikiano na kujenga uwezo wa kiuchumi kwa ajili ya kuendesha maesha na dini yetu. Aidha Samahat sheeikh jalala Aliwaasa wakaazi wa Handeni juu ya ubaguzi wa kimadhehebu na kuwataka wote kuwa kitu kimoja dhidi ya Adui anayefaidika kwa utengano wao.

DSC00075 Read the rest of this entry

Sheikh Hemedi Jalala: Ziarani kitabligh Mkoani Tabora

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Tanzania chini ya Mwamvuli wa Hawza Imam Swadiq Samahat Sheikh Hemedi Jalala Mwisho mwa Wiki hii aliongoza Jopo la Wanaharakati na Wahubiri kutoka hawza Imam Swadiq (as) kuzuru Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kukutana na waumini wa kiislamu katika mkoa huo. Huu ni muendelezo wa Kampeni ya Uamsho wa Jamii, Kampeni inayolenga mikoa yote ndani ya nchi ya Tanzania kuamsha waumini kushikamana katika kamba moja (Laa Illaha Illah llah Muhammad Rasulullah) na kupiga vita Utengano wowote wa Kidini unaochochewa na baadhi ya Makundi ndani nchi.
Samahati sheikh Jalala aliwataka wananchi na hususan waislamu wa mkoa wa Tabora kurudi katika Mafundisho ya Uislamu wa Asili unaolazimisha na kuwataka waislamu kuwa kama mwili mmoja na kutupilia mbali tofauti zao za kimitizamo kuwatenganisha.

DSC00043

Samahati Sheikh Jalalala na Jopo la Masheikh waliongozana nae Mkoani Tabora

DSC00061

Samahati Sheikh Hemedi Jalala Akiwa Jukwaani akihutubia wananchi wa mkoa wa Tabora

DSC00076

Sehemu ya Wakaazi wa Mkoa wa Tabora waliokusanyika kwa Mamia kumsikiliza Samahati Sheikh Hemedi Jalala

DSC00096

Picha za Wakaazi wa Tabora wakifuatilia hutuba ya Sheikh Hemedi Jalala mkoani Tabora.

DSC00102

Sura mbalimbali za Raia wa mkoa wa Tabora wakifuatilia Mhadhara wa Samahat Sheikh Hemedi Jalala

DSC00105

DSC00117

Baadhi ya Sehemu ya Picha ikionyesha Kinamama wakifuatilia hotuba ya wahadhiri walioandaman na Samahat Sheikh Hemed Jalala

DSC00103

 

DSC00131

Sehemu ya waalikwa katika Muhadhara wa Kitabligh Moani Tabora

 

DSC00125

DSC00190

Sehemu ya Kina Mama wakifuatilia Mhadhara wa Kiongozi wao Samahati Sheikh Hemedi Jalala.

DSC00204


ScreenShot

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: