Category Archives: Uncategorized
UMUHIMU WA NDOA KATIKA JAMII
Katika khutba ya ijumaa iliyotolewa leo, katika masjid Ghadiir kigogo Post- Dar es alaam, Shk Said Otmani alizungumzia umuhimu wa ndoa katika jamii, alisema : ndoa ni ibada na ni ndio Taasisi muhimu katika jamii, hivyo inabidi kuenziwa na kuheshimiwa, kutoka katika ndoa, kukinga uharibifu na kutotokea kwa k watoto wa wasio halali
Akayataja malengo ya ndoa . kua ni 1: kupata utulivu. Kama alivyosema mwenyezi Mungu katika surat Nuur nakatika alama za kuwepo mwenyezi Mungu, nikukuumbieni kutokana na nafsi zenupea mbili. (mwanmke na mwanmume) ili mpate utulivu. 2: lengo la pili. Ni vazi . kama alivyosema mwenyezi mungu, katika surat baqarat: (2: 187): wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Aktaja faida za vazi kua vazi linamsitiri mtu, linampendezesha mtu, na ni kinga kwa mtu kwa joto na baridi.
“ Kama vile mtu anatumia muda kutafuta vazi zuri vile vile kwa watakao kuoa watumie muda mmingi kutafuta mtu atkae kua mwenza katika Taasisi hiyo muhimu, ili isije kuharibika na kuvunjika mapema” akawataka watu waifate hadithi ya mtume (s.a.w.w.) aliyosema, atakapowajilia mtu mnayependezwa nae kwa dini yake na tabia yake , basi muozesheni, msipofanya hivyo, kutatokea fitna na uharibifu mkubwa katika jamii. : dini iwe ni kipaumbele chakwanza na uzuri uwe ni sifa ya mwisho, kwani mtu akimuoa mwanamkw kwa sababu ya uzuri, ipo siku utaondoka uzuri huo, kwa uzee, au kwa ajali, na itakua sababu ya kuachana, lakini kama atamuo kwa sababu ya dini, dini atabaki nayo milele kama ataienzi.
Lengo latatu ni kwa kupatikana kizazi cha halali, ndoa inasababisha wapatikane watoto wa halali, isio ka ndoa watapatikana watoto wa mitaani na panya road, nawatoto ombaomba.
Mwisho Sheikh Said aliwaasa vijana kufanya haraka kuoa, wasihofie ufaqiri,kwani hiyo ni dhana mbaya kwa mwenyezi Mungu(s.w.) kwani mwenyezi Mungu (s.w) amewapa uhakika mafaqiri kwa kuwaongezea Riziki pindi watakapo oa, pale aliposema katika surat Nuur aya (24 ya 32): mkiwa ni mafaqir mwenyezi mungu atakunjulieni kipato.” Nani mwenye maneno ya kweli kuliko mwenyezi mungu? Kwa hiyo vijana waache woge