Blog Archives

TUWE VIPI BAADA YA MFUNGO WA RAMADHANI?

Hii ni khutba ya kwanza ya sala ya ijumaa katika mwezi Shawwal, ijumaa ya kwanza baada ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Maulana Sheikh Hemedi Jalala Khatibu wa sala ya ijumaa Msikiti wa Ghadiir Kigogo Post Dar es Salaam Tanzania, amegusia swala la maadili na tabia njema ambazo zilikua ni darasa na malezi ambayo watu wamejifunza na kupambika nayo ndani ya mwezi wa ramadhani na kuelezea ya kuwa kuna wajibu wa kuendeleza tabia hizo baada ya ramadhani.

Sambamba na hayo amezungumza na kukemea vikali maswala ya uvunjifu wa maadili na hasa swala la mahusiano ya jinsia moja (ushoga) amabayo tumeanza kuyaona yanaonyeshwa waziwazi na vyombo vya habari na kuelezea athari zake mbaya kwa taifa na binadamu kwa ujumala. Maulana pia ametoa wito kwa TCRA kuchunguza na kuondoa picha na viashiria vya uvunjifu wa maadili katika mitandao kwani uwezo huo wanao na kusema kuwa yote hayo hayana tija kwa taifa na watu wake na kuwa hakuna dini inaunga mkono mambo hayo.

Semina ya Viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristu kupinga Ugaidi Barani Afrika.

Msikiti wa Ghadir Kigogo Polisi post, Jana 29/05/2015

DSC01243

Uongozi wa Hawza Imam Swadiq Chini ya Kiongozi wake Mawlana Sheikh Hemedi Jalala uliandaa Semina ya Kupinga Ugaidi Barani Afrika, Semina hiyo iliwakusanya viongozi mblimbali wa Dini akiwemo Pasta Erasto Likongo Mwenyekiti wa Pentecoste Pastors Fellowship, Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania na Raisi wa Baraza la Makanisa barani Afrika. Pia alikuwepo Amiri Mstaafu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Juma Mbukuzi pamoja na Masheikh wengine wa Madhehebu mbalimbali na Viongozi mbalimbali wa Kikristo Tanzania bila kusahau Viongozi wa Serikali.

DSC01355

Pastor Evarest Mmoja wa Wageni waalikwa katika semina

DSC01383DSC01371Akihutubia Wageni waalikwa Sheikh Hemedi Jalala, alikumbusha kuwa Mwewnyezi Mungu awali alipowaumba wanaadamu wakiwa ni kitu kimoja hawakuwa na migongano na hili analithibitisha katika Quraan aliposema hakika huu Umma wenu ni ummah moja,

DSC01366

Kisha baada ya zama kupita tofauti baina ya wanaadamu zilianza kukuwa, hata uwepo wa Mitume kuletwa kuja kufundisha Amani na Utulivu, Matabaka na Migongano kwenye jamii ya Mwanaadamu ilizidi kuongezeka  mpaka leo tulipo duniani kizazi cha Mwanaadamu kinakabiliwa na tishio kubwa la kuangamia kwa Matendo yaliokiuka mipika, Matendo ya kigaidi. Akianisha sababu kuu za Ugaidi Sheikh Jalala amesema “Ugaidi unaweza kuwa unatokana na Sababu kuu tatu, Mmoja ni kusafishwa ubongo (brainwashing) anaoufanyiwa mwanaadamu na kuwekewa fikra kuwa Imani yake, Dini yake, Madhehebu yake, Mila yake ndio sahihi na za watu wengi hazifai na hawana haki ya kuishi, Huu ni ugaidi wa Kifikra uliovishwa Gauni la Kidini lakini chanzo ni Fikra mbovu na chafu, Akataja sababu ya Pili kuwa Mara nyingine wanaweza kutumiwa watu kukosesha Amani ndani ya jamii, kwa sababu ya Fedha, na Mara nyingine umetumika ugaidi kama sababu ya kudai haki. Mwisho Sheikh Jalala alikokoteza kuwa aina hii ya kwanza ya Ugaidi kama zao la Fikra mbovu ndio sababu kuu ya Ugaidi dunia. Aidha Sheikh Jalala aliwataka Viongozi wote wa Dini Kushikamana Pamoja kupiga Ugaidi unaoendelea sehemu tofauti tofauti Duniani na hususan barani Afrika na kueleza yaliyotokea huko Kenya na yanayoendelea Somali, Libya, Misri na nchi zingine barani Afrika ni matendo ya Kigaidi na kamwe hayana mahusiano yoyote na Dini yoyote kati ya dini kuu Tatu duniani, Ukristo, Uyahudi na Uislamu.

DSC01315DSC01265

Kwa upande wake Pastor Erasto Mokiwa wa Kanisa la Pentekoste, alishukuru sana na kufurahishwa sana lakini alikiri kuwa mualiko wenyewe ulimshitua sana kuhudhuria semina Msikitini kwani Wakristo wanafikra kuwa  waislamu ni watu wanaotumia dini kuuwa na kuteka watu. Aidha amekiri kuwa wakristo wamejengewa hofu kuwa maeneo ya dini ya Kiislamu na vyuo vya dini ni maeneo ambayo ni kambi ambazo vijana wanafundishwa Ugaidi, Mafunzo  ya Kijeshi. Aidha alimtaka Sheikh Jalala kuandaa semina nyingine kubwa kwa viongozi wa dini wa kikristo ili kuondoa hofu hiyo kwa Maaskofu na Wachungaji..

DSC01307

Mwisho alikiri kuwa amefarijika sana na maneno ya Sheikh Jalala na kumtaka maneno hayo yarudiwe katika mkutano mwingine ili kuwatete wakristo Tanzania. Aidha amesema Sheikh Jalala amefanya vizuri sana kuwaalika na kuandaa mkutano huo katika eneo la chuo chake kwani ni uthibitisho kuwa tofauti na dhana iliyopo sio vyuo vyote vya dini ni kambi za kufundisha Ugaidi. Mwisho aliwaomba waislamu kujitokeza kuwaondoa khofu wakristo na kuwatetea kwani hata wakristo nao huwatetea na kutoa mfano wa dhulma unaofanywa na Benk ya NMB Morogoro kuwadhulumu familia ya Kiislamu kiwanja kilichojengwa benki hiyo.

Kwa upande wake askofu mokiwa walisema, Wakati mwingine Ugaidi ni Mradi unaofanywa na nchi kubwa duniani na akaonyesha wasiwasi wake kwa Mashirika makubwa ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa kuwa ndio wenye kuanzisha Machafuko na ugaidi ili kuweza kuziwezesha nchi kubwa duniani kufanya biashara ya Silaha. Akizungumzia Magaidi amekiri kuwa ugaidi upo ndani ya Dini zote na kutoa mifano kuwa kama ilivyokuwa vita vya miaka mingi kati ya Ireland ya Kaskazi (Waprotestant) na Uingereza (Waanglikan) ndivyo hivyo leo huko Yemen Mawahabi wanaongoza dola ya Saudia Arabia na Houth Mashia wanaoishikilia yemen. Mwisho amewataka viongozi wa kidini kupambana na ugaidi na akainisha njia tatu:

DSC01327

  1. Kila kiongozi wa Dini na kila mwanadini aonekane hadharani ni Mtu wa Amani na Usalama kwa Mienendo yake kwa Mujibu wa Mafundisho ya dini yake.
  2. Kuwepo vikao vya pamoja baina ya viongozi wa Dini kukaa kwa Amani mara kwa mara kujadili hatari zinazoikabili jamii na Dini kwa ujumla.
  3. Viongozi wa dini tofauti tofauti na Madhehebu yao walindane wao kwa wao, Utu wao, Heshima zao na Damu zao na Waishi kwa Amani bila kuchokozana.
  4. Viongozi wa Kikristo na kiislamu wawe na Mtandao wa Mawasiliano na makubaliano ya pamoja kuhakikisha hakuna kiongozi anatakayeruhusu nyumba yake ya Ibada kutumika kama kichaka cha Magaidi.

Baada ya kukamilisha shughuli nzima Mawnala Sheikh Hemedi Jalala aliwaalika wageni wake katika Tafrija fupi ya chai ya Jini na kubadilishana mawazo .

DSC01391 DSC01394 DSC01390

Sherehe za Mazazi ya Mtume Muhammad (saww)

SEHEMU YA KWANZA…

DSC03320

Wageni waalikwa katika Hafla ya Mawlid ya Mtume katika Viwanja vya Hawza Imam Swadiq Kigogo, Dar es Salaam

 

DSC03357

DSC03352

 

 

DSC03349

Wanafunzi wa Hawza Imam Swadiq (as) wakiimba Kaswida ya kumsifu Mtume (saww)

DSC03347

DSC03345

DSC03340

Sheik Yusuf, Imam wa Msikiti wa Makuti Manzese, Dar es Salaam akihutubia Mamia ya waliohudhuria katika Sherehe za Mazazi ya Mtume

DSC03312

 

 

 

DSC03341

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: