Blog Archives

TUWE VIPI BAADA YA MFUNGO WA RAMADHANI?

Hii ni khutba ya kwanza ya sala ya ijumaa katika mwezi Shawwal, ijumaa ya kwanza baada ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Maulana Sheikh Hemedi Jalala Khatibu wa sala ya ijumaa Msikiti wa Ghadiir Kigogo Post Dar es Salaam Tanzania, amegusia swala la maadili na tabia njema ambazo zilikua ni darasa na malezi ambayo watu wamejifunza na kupambika nayo ndani ya mwezi wa ramadhani na kuelezea ya kuwa kuna wajibu wa kuendeleza tabia hizo baada ya ramadhani.

Sambamba na hayo amezungumza na kukemea vikali maswala ya uvunjifu wa maadili na hasa swala la mahusiano ya jinsia moja (ushoga) amabayo tumeanza kuyaona yanaonyeshwa waziwazi na vyombo vya habari na kuelezea athari zake mbaya kwa taifa na binadamu kwa ujumala. Maulana pia ametoa wito kwa TCRA kuchunguza na kuondoa picha na viashiria vya uvunjifu wa maadili katika mitandao kwani uwezo huo wanao na kusema kuwa yote hayo hayana tija kwa taifa na watu wake na kuwa hakuna dini inaunga mkono mambo hayo.

Ukristo katika Miongozo ya Ayatullah Udhma Khamenei

Mlango wa Kwanza:  Nabii Isa Masihi (AS)

Mtume Mkubwa wa Mwenyezi Mungu

Thamani ya Nabii Isa (AS) kwa mtazamo wa Waislamu, bila ya shaka si ndogo na haishindwi na ile waliyo nayo Wakristo ambao ni wafuasi wa kweli wa mtukufu huyo.

Mtume huyu mkubwa wa Mwenyezi Mungu alikipitisha kipindi chake chote wakati alipokuwepo hapa duniani baina ya watu kwa hima kubwa ili aweze kupambana na dhulma, uchupaji mipaka, ufisadi na watu wanaotumia mabavu. alisimama kidete kukabiliana na dhulma na maovu yaliyokuwa yakifanyiwa mataifa mbalimbali. Tabu alizokumbana nazo Mtume huyu Mkubwa wa Mwenyezi Mungu kuanzia katika kipindi chake cha utotoni hadi kuondoka kwake duniani zote zilikuwa katika njia hiyo hiyo. Itakumbukuwa kuwa Mwenyezi Mungu alimpa Utume Nabii Isa AS tangu akiwa mtoto.

Nabii Isa (Amani Iwe Juu Yake) Mtume Mkubwa wa Mwenyezi Mungu

Waislamu wanamkubali na kumtambua Nabii Isa kuwa ni Mtume Mkubwa wa Mwenyezi Mungu (kama wanavyomkubali Wakristo). Mayahudi hawawezi kusema kwamba, Nabii Mussa (AS) ni mali yetu na hawahusu watu wengine; hapana. Wakristo wote ulimwenguni wanamkubali Nabii Mussa (AS); kama ambavyo Waislamu kote duniani wanamheshimu na kumkubali Nabii huyo wa Mwenyezi Mungu.

Kuhusiana na Nabii Isa pia ni hivyo hivyo; kwa maana kwamba, Nabii Isa Masiya (AS) si wa Wakristo tu, bali Mtume huyo ni wa Waislamu pia. Wananchi Waislamu wa Iran wanampenda na kumtukuza Nabii Isa (AS) na wanamheshimu sana Mtukufu huyo. Wakristo wa Iran – iwe ni Maashuri, iwe ni Wakristo wa maeneo ya kaskazini na Orumieh – wote wanaamini kwamba, asili ya Ukristo inaanzia hapo. Wanasema kuwa, kituo cha Mtukufu Nabii Isa kilikuwa hapa na kwa hakika Ukristo ulienea kuanzia hapa. Pengine kuamini kwao huko ni sawa kwa upande wa historia.

Maryam Ruwaza Njema kwa Wanadamu

Wakati Qur’ani Tukufu inapozungumzia kiigizo kwa ajili ya wanadamu kwa upande wa imani, haidhukuru kiigizo hicho kutoka baina ya wanaume; bali inakitolea mfano kutoka miongoni mwa wanawake; Mwenyezi Mungu Mtukufu anawataja wanawake wawili kama mfano na ruwaza njema kwa wanadamu kwa upande wa imani, lakini hakufanya hivyo miongoni mwa wanawake mahiri. Hii ina maana maana kwamba, katika medani ya ubinadamu na ukamilifu wa kimaanawi, wakati Mwenyezi Mungu anapotaka kubainisha mfano bora, hazungumzii Mitume, shakhsia wakubwa, na shakhsia wa kielimu na wa kidini; bali anatolea mfano wanawake wawili ambapo mmoja kati ya wanawake hao ni mke wa Firauni. Mwanamke mwingine wa pili ni Maryam mama wa Nabii Isa (AS) na binti ya Imran. Maryam ni mwanamke ambaye katika rika lake la ujana alikabiliwa na tuhuma na dhana mbaya ya kutenda dhambi kutoka kwa wakazi wote wa mji na kitongoji chake. Lakini mwanamke huyo mtukufu hakutetereka bali alisimama imara na madhubuti kama mlima na akalishika vilivyo Neno la Allah na Roho (Nabii Isa AS) ambavyo Mwenyezi Mungu alimpulizia mtukufu huyo kwa uwezo na nguvu Zake Allah zisizo na mpaka, na akamlea barabara mwanawe aliyekuwa kama tochi ya kuumulika ulimwengu uliokuwa na giza totoro.

Bibi Maryam Dhihirisho la Usafi

Kuna nukta moja katika kisa cha Bibi Maryam (Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) kwenye Kitabu Kitakatifu cha Qur’ani ambayo imenivutia mno. Waislamu wanamtaja Bibi Maryam katika ibara zao wakisema kuwa Bibi mwema huyo ni dhihirisho la usafi, utakasifu na utoharifu – yaani mwanamke msafi kabisa – katika Qur’ani kuna sehemu kadhaa amezungumziwa Bibi Maryam (SA). Mwenyezi Mungu anasema: ‘‘Na Mariamu binti wa Imrani, aliyelinda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wat’iifu”. At-Tahriim 66:12

Suala la Maryam kulinda ubikira wake, staha, heshima, usafi na utakasifu wake wa mwili, limesisitizwa mno katika Qur’ani. Sasa swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwani mazingira yalikuwa vipi wakati huo? Kwa mtazamo wangu hiki ni kitu muhimu sana. Naam; Binti mdogo alikuja ndani ya maabadi na kuishi hapo hadi ujanani mwake wake. Kulikuwa na sababu na msukumo gani kwamba, Maryam kwa ujudi wake wote asimame kwa nguvu zake zote kukabiliana na nguvu ya hali ya juu kabisa ya Mwanaadamu? Ni wazi kwamba kama haikuwa ya hali ya juu kabisa ya Mwanaadamu, Qur’ani isingelitilia mkazo kiasi chote hiki nguvu hiyo. Sasa jambo kubwa la kujifunza hapa ni huku kujitokeza Bibi Maryam na kusimama kidete kukabiliana na ushawishi wote mbaya uliokuwepo wakati huo kiasi kwamba Qur’ani inamsifu ikisema: “alilinda ubikira wake”. Hili ni jambo lenye umuhimu mkubwa; ni darsa, ibra na funzo kubwa kwa watu wote.

Bibi Maryam (SA) aliweza katika wakati nyeti kupambana na mtihani ule na kuhifadhi usafi wake na utakasifu wake, kiasi kwamba, aliacha taathira kubwa kiasi chote hiki katika historia, kama ambavyo mfano mwingine ni ule wa kijana wa kiume – Nabii Yusuf (AS) – ambapo hilo nalo limeelezwa katika Kitabu Kitakatifu cha Qur’ani.

Sifa Maalumu ya Kisa cha Isa bin Maryam (AS)

Mimi binafsi kila ninaposoma au kusikia Sura Tukufu ya Maryam kuanzia katika kipindi cha ujana mpaka sasa hali yangu huwa hivi hivi yaani huathirika mno; kwani tukio hili ni tukio lisilo la kawaida. Kisa cha kuzaliwa Nabii Isa (AS) katika mazingira kama yale na eneo lile na ile hali na nafasi iliyokuwa ikitawala katika historia na jamii ya wakati ule; wakati yote hayo yanapokusanyika pamoja na mtu anapotilia maanani adhama na utukufu waliokuwa nao watukufu hao, kwa hakika humuwia vigumu kupata maneno sahihi ya kuelezea kisa hicho na hakuna bayani ambayo inaweza kutoa wasifu wa tukio hilo kama inavyostahiki, isipokuwa bayani ya sanaa!

Tukio hili ni miongoni mwa yale matukio ambayo ni ya ajabu mno na machache kuwahi kutokea; nafasi ya Bibi Maryam, nafasi ya Janabi Zakaria, hali ya kijamii ya wakati huo, kuchomoza jua lile lililokuwa liking’ara katika mbingu ya ujudi wa Mwanaadamu, akili ya Mwanaadamu na uhai wake – ambayo ni mafundisho ya Nabii Isa (AS) – na hasa kwa kuzingatia kwamba, mafundisho ya Nabii Isa (AS) hayana tofauti yoyote na mafundisho ya Nabii Mussa (AS); kwa maana kwamba, mafundisho yake yalikuja kukamilisha mafunndisho yaliyotangulia. Mengi ya mafundisho hayo yalikuwa ni ya kukariri yaani ni yale yale ya huko nyuma. Wakati mafundisho hayo yalipokuwa yakitolewa na Nabii Isa AS, wafuasi wa Nabii Mussa (AS), walipinga sana mafundisho hayo na walikuwa wakiyaona kama ni bidaa kutokana na upotofu mkubwa waliokuwa nao; wakati ambapo, mafundisho hayo yalitoka katika chimbuko na chanzo kile kile yaani Wahyi na Ufunuo. Kisa cha Nabii Isa AS kinabainisha kwa uwazi kabisa athari mbaya za upotofu, athari za kutumia vibaya nguvu, ufahamu mbaya na kujiona.

Mshika Bendera ya Hidaya

Ile Kalima ya Mwenyezi Mungu (yaani Nabi Isa Masihi AS) alikuwa mshika bendera ya hidaya ya uongofu katika kipindi cha upotofu, ujahili, dhulma na upuuzaji wa thamani za kibinaadamu na alichukua jukumu la kuwa mwokozi wa wanadamu. Katika kipindi hicho, Nabii Isa alisimama kidete kupambana na udikteta, dhulma na uonevu na alikuwa akifanya hima na jitihada kwa ajili ya kuhakikisha kuwa uadilifu, usawa, rehma na tawhidi vinakuweko katika jamii. Leo hii wanaomwamini Mtume huyo mkubwa wa Mwenyezi Mungu – yaani Wakristo na Waislamu – ili kusimamisha mfumo unaostahiki kuwepo ulimwenguni, ni lazima washikamane na mafundisho ya Mitume sambamba na kueneza mafundisho ya watukufu hao na fadhila na thamani za kibinadamu kwa mujibu wa mafundisho ya walimu hao wa wanadamu.

Mkombozi wa Watu kutoka katika Dhulma

Nabii Isa Masihii (AS) alikuwa na muujiza na alibaathiwa na kupewa Utume kwa ajili ya kumkomboa Mwanaadamu na kumuokoa kutoka katika giza la shirki, kufru, ujahili na dhulma na kumuongoza katika nuru, maarifa, uadilifu na kumwabudu Mwenyezi Mungu Mmoja pasina kumshirikisha na kitu kingine. Katika muda wake wote alioishi na watu, Isa Masiya (AS) alifanya hima ya kupambana na mabaya na kuwaita watu katika mambo mema na hakusita hata kidogo kufanya hima katika uwanja huo. Hili ni somo na darsa ambayo Wakristo na Waislamu ambao waanaamini Utume wa Nabii Isa (AS) wanapaswa kujifunza.

Leo hii Mwanaadamu anahitajia zaidi mafundisho hayo kuliko wakati mwengine wowote ule. Uislamu ambao ni kamilisho la mafundisho ya Isa Masihi AS, umeweka mbele katika daawa yake masuala ya kheri, marekebisho na ukamilifu pamoja na ifanisi wa Mwanaadamu humu duniani na kesho Akhera. Mwanaadamu aliyepotea kwa kuwa na nguvu zisizo na mpaka za maumbile na ambaye amepata nguvu hizo kwa baraka za elimu aliyopewa na Mwenyezi Mungu, anafanya kinyume kabisa na malengo aliyoumbiwa na kupewa nguvu hizo. Leo hii majukumu ya wafuasi wa dini za Mwenyezi Mungu ni mazito zaidi. Madola ya kibeberu na yenye satua ulimwenguni kimsingi yamekuwa yakibana anga ya mataifa na watu madhulumu na hayaachi kufanya dhulma yoyote dhidi ya mataifa hayo kwa madai ya kulinda dini ya Kikristo.

Mlinganiaji wa Bahati Njema

Nabii huyo mukhtari wa Mwenyezi Mungu, alikuwa akiwaita na kuwalingania watu kwenye mema na kheri zao na alikuwa akiwatahadharisha watu juu ya matamanio ya nafsi na kujitumbukiza katika mambo machafu na sifa mbaya za kiroho, dhulma na mambo mabaya na machafu. Madola ya kifisadi ya kibeberu na watumiaji mabavu walikuwa wakimuudhi, kumtuhumu na kumvunjia heshima Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu na hata kufikia hatua ya kutaka kumuua na baada ya Mwenyezi Mungu kumpa hifadhi, Hawariyyun (wanafunzi) na wafuasi wake kwa miaka kadhaa waliteseka na kutaabishwa na watu waliokuwa wakipinga mafundisho ya Nabii Isa (AS) ambayo yalikuwa dhidi ya ufisadi, dhulma, shirki, kufuata hawaa na matamanio ya nafsi, kupenda vita na kuwahadaa watu maadui ambao walitaka kuyafutilia mbali mafundisho ya mtukufu huyo.

Wale ambao walikuwa ni mafasidi, madhalimu, washirikina, wafuasi wa matamanio ya nafsi, wapenda vita na wahadaaji wa watu walikuwa hawako tayari kuivumilia dini ya Mwenyezi Mungu wala Mtume wa Allah (Masihi Isa AS) na mafundisho yake.

Kuzaliwa Mtukufu Isa Masiya (AS)

Mamia ya miaka ya kukifanyika sherehe za kukumbuka kuzaliwa Isa Masihi (AS) imepita. Kwa nini kuzaliwa kwake kuna umuhimu na thamani kubwa?

Ni kutokana na kuwa, hicho kilikuwa ni kipindi muhimu, nyeti na chenye kuainisha, nukta ya kurejea na nukta ya kona na kupinda katika historia. Yaani historia ilikuwa ikienda katika mstari wake; lakini katika lahadha hii ikapinda na kuelekea upande mwingine. Hii ni nukta ya kukata kona na nukta ya kuelekea upande mwingine. Sisi kila mwaka huwatumia salamu za mkono wa baraka na kheri ndugu zetu Wakristo hapa nchini na Wakristo wengine ulimwenguni kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa Nabii Isa (AS); hata hivyo kutokana na kuwa kwa mujibu wa nadharia ya Wakristo wengi wanaoishi hapa nchini tarehe ya kuzaliwa Nabii Isa AS si tarehe 25 Desemba kama wanavyoamini Wakristo wengine ulimwenguni, bali ni katika kumi la kwanza la mwezi Januari – ambapo Waarmenia ni miongoni mwa waliomo katika kundi hili – sisi huwa hatufuati tarehe hiyo ya 25 Desemba na ndio maana hatutumi salamu za pongezi siku hiyo, bali husubiri mpaka ufike mwezi Januari hapo ndipo tunapotuma salamu zetu za pongezi, kheri na baraka ili tuendane na nadharia ya ndugu zetu wa hapa nchini.

Inshallah, kumbukumbu ya kuzaliwa Nabii Isa (AS) inabidi iwe ni siku ya baraka kwa Wakristo na Waislamu wote ulimwenguni. Ala Kulli Haal, katika siku kumi hizi ni siku za kukumbuka ya kuzaliwa Nabii Isa Masiya Inshallah Waislamu na Wakristo wote watajifunza muamala na mwenendo wa Mtukufu huyo na kumfahamu vyema Isa Masiya (AS) na hivyo kumfuata Nabii huyo mteule wa Allah….. Itaendelea….

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: