Blog Archives

MAUAJI YA HUSSEIN,NANI WA KULAUMIWA? KWANINI YAKUMBUKWE?

Waislamu duniani wameendelea kuyakumbuka na kuyaenzi mapinduzi ya Imam Hussein kwa kuweka vikao mbalimbali katika misikiti na sehemu zingine, Maswali yamebaki kwa

sheikh ayub rashid

baadhi ya waislamu na hata wasiokuwa waislam wanajiuliza kwanini Hussein, na je nani wa Kulaumiwa ? na kwanini Mauaji hayo yakumbukwe?

Hujjatul Islamu, Sheikh Ayub Rashid anaandika haya yafutayo kujibu swali hilo hapo juu

Mauji ya Imam Hussein, nani wa kulaumiwa? Na kwa nini yakumbukwe?

Ilikuwa tarehe 7 Muharram 61 AH ipokuja amri ya kuzuia maji yasiwafikie watu ya kambi ya Imam Hussein na wenzake! Wao walikuwa katika ardhi ya Karbala.Walikaa hivyo bila ya maji kwa muda wa siku tatu!

Asubuhi ya tarehe 10 Muharram 61 AH ilikuja amri kupitia kwa mwanajeshi mwenye amri ya yote siku hiyo, huyo hakuwa mwingine bali Umar bin Saad, mtoto wa swahaba Saad bin Abi Waqqas. Huyu aliteuliwa na Ubeidullah bin Ziyaad, kuliwakilisha kundi la Yazid dhidi ya mjukuu wa Mtume (saw).Amri aliyopewa Umar bin Saad ni kumlazimisha Imam Hussein kutoa baia kwa Yazid, na kama akikataa basi auwawe! Yaani Imam Hussein mjukuu wa Mtume amuunge mkono Yazid kama kiongozi wake! Imam Hussein alikataa amri hiyo!

Wakati hayo yote yakiendelea, mwanajeshi mmoja aliyejuliakana kama Hur bin Yazid al Riyaahi alijikuta haamini aliyokuwa akiyasikia yakiamuliwa ya kumuua imam Hussein, mjukuu wa Mtume.Mazungumzo yakaanza ya pande mbili, kambi ya Umar bin Saad na ya Imam Hussein,hiyo ikiwa ni siku ya 10 Muharram, siku ijulikanayo kama Ashura, katika mwaka wa 61 wa Hijiriyyah.

Kambi ya Yazid ikiongozwa na Umar bin Saad ikimtaka Imam Hussein kutoa baia (Kiapo cha utii) kwa Yazid, na Imam Hussein alikataa ombi hilo kata kata! Kwa sababu kubwa kuwa Yazid hakuwa na sifa za kuwa kiongoz wa Waisilamu. Yazid alikuwa mtu fasiq (muovu)!

Ndipo ilipofika baada ya Adhuhuri ikaja amri ya kuanza vita! Mshale wa kwanza ukatupwa kutokea katika kambi ya Kina Yazid dhidi ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saww).

Mapigano

Kabla ya mapigano hayaja anza, yule mwanajeshi, Hur bin Yazid al Riyaahi, alipo ona kuwa wenzake wameazimia kumpiga vita Imam Hussein, na baada ya kuzungumza nao na kuona kuwa maamuzi yao ni ya kweli, aliamua kuikimbia kambi yake na kujiunga na kambi ya Imam Hussein. Rehema ya Allah iwe juu yake.

Mapigano yaka anza ya mtu mmoja mmoja, waka uana wengi wa pande mbili. Jeshi la Yazidi likiua kwa kuwa ni amri ya Yazid dhidi ya waliokosa kutoa baia, na la Imam Hussein likipigana na maadui wa mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) kwa kujihami. Lakini kwa kuwa jeshi la Yazid lilikuwa kubwa mno kulinganisha na jeshi la wafuasi wa Imam Hussein, jeshi la watu 72 Au watu 100 na kidogo. Takriban watu wote wanaume waliokuwa wakimuhami Imam Hussein waliuliwa.

Mwisho wa Imam Hussein

Baada ya kubakia pekee yake, Imam Hussein alipigana kiume kujilinda na kujihami na maadui hao, lakini alizidiwa nguvu na majangili hao wengi.

Mwisho aliangushwa chini kwa kupigwa na mti wa chuma, na pia baada ya kupigwa na jiwe kubwa. Akiwa hapo chini aliomba maji ya kunywa, lakini, mjukuu wa Mtume (saw) hakupewa na badala yake akawa akipigwa mateke na kutukanwa matusi makubwa makubwa.

Mwisho Umar bin Saad akatoa amri; “Mmalizeni”!

Ndipo alipokuja Shimri bin Dhil Jaushan, kama wana historia wengi walivyo eleza. Shimri akiwa ameshika kisu kikubwa! Akashika ndevu za Imam Hussein, akaweka kisu hicho kwenye shingo ya mjukuu wa Mtume! Aka anza kukikata…mpaka akakitenganisha na mwili wake!

Inna lillahi wa inna ilaihi rajiuun!

Kichwa cha Imam Hussein

Maharamia hao, laana ya Mola iwe juu yao! Wakakitundika kichwa cha mjukuu wa Mtume juu ya mkuki! Wakakata na vichwa vya wafuasi wengine wa Imam Hussein, wakavitundika kwenye mikuki! Wakachoma moto kambi ya Imam Hussein, wakawateka wanawake waliokuwemo humo! Akiwemo mjukuu wa Mtume, bibi Zainab binti Ali bin Abi Twalib, Wakawapeleka kwa liwali au gavana Ubeidullah bin Ziyaad, katika mji wa Kufa.

Ubeidullah bin Ziyaad

Gavana huyu wa Yazid aliyekuwa katika mji wa Kufa, katika nchi ya Iraq, alifurahi sana kukiona kichwa cha mjukuu wa Mtume kimekatwa na vichwa vingine vimepangwa pembeni na wanawake wametekwa nyara. Akatoa maneno mengi ya kashfa na matusi!

Mwisho, akaamua kichwa cha Imam Hussein na vingine vilivyokuwa hapo, pamoja na wanawake hao na mwanamume mmoja tu aliyesalimika kuuliwa siku hiyo, wapelekwe Shaam kwa Yazid bin Muawiya. Huyo aliyesalimika alikuwa ni Ali bin Hussein maarufu kama Imam Sajjad.

Safari ya Shaam ika anza kuelekea kwa Yazid, na hii ilikuwa ni safari ya shida na madhila makubwa kwa walioitwa mateka!

Shaam

Msafara huo wa mateka ulipofika Shaam, watu waliamuriwa wajipange kusherehekea kushindwa kwa wapinzani wa Yazid, amir wa waisilamu, kama alivyo itwa!

Pindi Yazidi alipopelekewa kichwa cha Imam Hussein, alichukua fimbo, akapiga piga mdomo wake, huku akisema “hiki ndicho kimdomo alichokuwa akikibusu Muhammad’!

Akasema maneno ya kufru, kuwa yote hayo ni kisasi cha kulipiza mauaji ya mababu zake waliouliwa katika vita vya Badr! Laiti wangelikuwa hai wangelishuhudia mapigo yake!

Inna Lillahi wa inna ilaihi rajiuun!

Kwa nini kumlilia Hussein na sio Hassan?

Baadhi ya watu wameuliza kwa nini kumlilia Hussein na sio kumlilia ndugu yake Hassan au mashahidi wengine waliouliwa kabla yake?

Majibu

Kila mtu mwenye hisia za kibinadamu humlilia Hussein kwa namna alivyouliwa kinyama yeye pamoja na waliokuwa nao. Na kumlilia Hussein alianza babu yake, Mtume Muhammad (saw) kama ilivyokuja katika Hadith ya bibi Ummu Salama, mke wa Mtume (saw).

Na wafuasi wa Ahlulbayt huwalilia wote katika maimamu wao waliouliwa kishahidi na kwa dhulma. Huanza kwa kumlilia Mtume, kisha Ali bin Abi Twalib, kisha Hassan bin Ali na kisha Hussein na wale waliomfuatia miongoni mwa viongozi waliokuja baada yake.

Na hayo unaweza kuyashuhudia katika misikiti ya Mashia na katika kalenda zao ambazo huandika siku za maadhimisho ya kuzaliwa kwa maimamu wao na kuomboleza vifo vyao. Kwa hivyo si kweli kuwa wao humlilia Hussein peke yake!

Kwa nini ikawa msiba wa Imam Hussein umapewa siku nyingi zaidi?

Majibu

Ni kwa sababu ya kuelezea jinsi ya dhulma aliyofanyiwa mjukuu wa Mtume na wale waliodai kuwa wao ni watawala waadilifu wa Kiislamu. Na jinsi watawala hao walivyowalaghai watu na kuwadanganya kwa hila mbali mbali.

Na kuomboleza huku ni kueleza namna Umma ulivyokuwa umelala wakati huo mpaka ukaruhusu mjukuu wa Mtume auwawe kinyama, na kichwa chake kitundikwe katika mkuki na kipitishwe mitaani na watu kushangilia.

Na pia kuelezea namna Yazid, aliyekuwa ‘Amir al Muminin’, alivyokifanyia istihzai kichwa hicho kitukufu! Hayo yote hayatoshi kuomboleza kwa siku moja tu!

Sasa hivi msiba huu unaombolezwa kwa siku unazo ombolezwa ili kuwazindua watu kutoka katika ghafla waliyokuwemo ndani yake! Kwani kuna waisilamu wengi leo hata hawamjui Hussein alikuwa nani? Na Yazid alikuwa nani? Wala hawamjui muovu Ubeidullah bin Ziyad aliyetumwa na Yazid kusimamia mauaji ya mjukuu wa Mtume alikuwa ni mtu wa aina gani na aliamrisha maovu makubwa kiasi gani?

Historia ya kuuliwa Hussein mjukuu wa Mtume ni historia muhimu sana kujulikana leo, ili watu wasije kudanganyika na kuwafuata viongozi kama kina Yazid ambao hawakuwa na sifa ya kuongoza Umma wa Mtume Muhammad, swallallahu alaihi wa aalihi wa sallam.

Naamini hata haya tunayoyaelezea hapa wako watu wengi hawayajui!

Ya Allah tuonyeshe haki kuwa ni haki na uturuzuku kuifuata, na utonyeshe batwil kuwa ni batwil na utuwezeshe kuiepuka.

Imeandikwa na Hujjatul Islam,

Sheikh Ayub Rashid

 

 

Sherehe za Mazazi ya Mtume Muhammad (saww)

SEHEMU YA KWANZA…

DSC03320

Wageni waalikwa katika Hafla ya Mawlid ya Mtume katika Viwanja vya Hawza Imam Swadiq Kigogo, Dar es Salaam

 

DSC03357

DSC03352

 

 

DSC03349

Wanafunzi wa Hawza Imam Swadiq (as) wakiimba Kaswida ya kumsifu Mtume (saww)

DSC03347

DSC03345

DSC03340

Sheik Yusuf, Imam wa Msikiti wa Makuti Manzese, Dar es Salaam akihutubia Mamia ya waliohudhuria katika Sherehe za Mazazi ya Mtume

DSC03312

 

 

 

DSC03341

SAUMU YA ASHURAJE KUFUNGA SIKU YA ASHURA NI SAWA ?

image

Mwandishi:
Ra’isul Mubalighin
Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi R.A.

Mutarjuma:
Amiraly M. H. Datoo

Baadhi ya Hadithi zinapatikana katika vitabu vya Ahl as-Sunnah zinazosema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati wa kuhama kwenda Madina, aliwakuta Mayahudi wakifunga (saumu), mwezi 10 Muharram (Mfunguo nne). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwauliza sababu ya kufanya hivyo, alijibiwa: “Ni siku njema, siku ambayo Mungu aliwaokoa wana wa Israil kutoka kwa adui yao (yaani Firauni); hivyo Mtume Musa alifunga (saumu) siku hiyo.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mimi nastahiki zaidi kwa Musa kuliko ninyi.”

Hivyo Mtume (s.a.w.w.) alifunga siku hiyo na kuwaamrisha Waislamu wafunge siku hiyo. Rejea: Al-Sahih ya al-Bukhari, J. 3; chapa ya Misri, uk. 54. na Mishkatul-Masabih, chapa ya Delhi; 1307 A.H., uk. 172.

Immetolewa maelezo na mfasiri wa Mishkatul-Masbih kwamba: “Ilikuwa katika mwaka wa pili, kwa sababu katika mwaka wa kwanza Mtume aliwasili Madina baada ya Ashura katika mwezi wa Rabiul-Awwal (mfunguo sita).

Ni kiasi gani ilifikiriwa kuwa na umuhimu hivyo? Hiyo inaweza kuamuliwa na Hadithi nyingine iliyosimuliwa katika al-Sahih al-Bukhari: “Mtume (s.a.w.w.) alimwamrisha mtu mmoja kutoka kabila la Aslam: ‘Watangazie watu kwamba yeyote ambaye amekula chochote, basi afunge sehemu ya siku iliyobakia, na yeyote yule ambaye hajala, basi afunge siku hiyo nzima, kwani leo ni siku ya Ashura (mwezi 10 Muharram)’”

Ni katika mwaka huo ambapo saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani iliwajibishwa, na wajibu wa kufunga siku ya Ashura ukaondolewa, kama ambavyo imedaiwa katiaka Hadthi nyingine zilizosimuliwa katika kitabu hicho hicho. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa zilizopo, bado inapewa umuhimu mkubwa kama saumu ya Sunnah!!

Sasa hebu tuziangalie kwa ukaribu sana Hadithi hizi:
Kwanza: Mayahudi walikuwa na kalenda yao na miezi yao. Hakuna mantiki yoyote kwamba walikuwa wakifunga siku ya Ashura mwezi 10 Muharram – mpaka ithibitishwe kwamba tarehe hii siku zote inawiana na siku ya Mayahudi ya kufunga.

Imetajwa katika makala yangu ya, “Matryrdom of Imam Husayn and the Muslim and the Jewish Calendars” (Alserat, vol. VI. No’s 3 & 4; Muharram 1401 Nov. 1980) kwamba mwezi wa kwanza wa Mayahudi (Abib baadae ukaitwa Nisan) ulikuwa ukifungana na mwezi wa Rajabu wa Waarabu. W. O. E. Oesterley na Theodore H. Robinson wameandika kwamba katika Arabia “sherehe muhimu zaidi kuliko zote ni ile ambayo huangukia katika mwezi wa Rajabu (sic), sawa na mwezi wa Kiyahudi Abib, kwani huu ulikuwa wakati ambao Waarabu wanasherehekea majira ya kuchipua baada ya kipupwe.” (Hebrew Religion; S.P.C.K., London; 1955; uk. 128)

Yumkini, katika zama za kale za matawi mawili ya nyumba ya Ibrahim walifuata mfumo huu huu wa kuongheza siku (intercalating), nyongeza ya mwezi mara saba katika mzunguuko wa mika 19. Na katika njia hii mwezi wa saba wa Mayahudi, Tishri I, ulifungana na Muharram. Na Ashura ya Muharram ililingana na mwezi 10 ya Tishri I, siku ya Mayahudi ya upatanisho – siku ya kufunga.

Katika makala hiyo ilielezwa kwamba kalenda hizo mbili zimepoteza uwiano wake wakati katika karne ya 9 hijra Uislamu ulipokataza uongezaji wa siku katika mwaka (intercalation). Lakini katika kuchunguza kwa kina inaonekana kwamba kulingana huko kulipotea zamani zaidi kabla ya kuja kwa Uislamu, kwa sababu Waraabu hawakufuata mpango wowote wa kihesabu katika uongezaji wao wa siku (intercalation).

Hii ndio maana Muharram ya mwaka wa pili Hijra ulianza tarehe 5 Julai, 623 C.E. (Al-Munjid, chapisho la 21), miezi kabla ya Tishri I (ambao kila siku unafungana na Septemba – Oktoba).

Kwa uwazi, Ashura ya Muharram katika mwaka huo (au, ilivyo, wakati wa uhai wote wa Mtume kule Madina) haikuwa na umuhimu wowote ule uwao kwa ajili ya Mayahudi.

Swali ni: Kwa nini walifunga katika siku hiyo?

Pili: Maandiko ya Kiyahudi ya Midrashic huelezea siku ya 10 ya mwezi wa 7 (Yom Hakippurim – Siku ya Upatanisho) kwenye tukio la kurudisha Mbao za Agano kutoka Mlima Sinai, kama Dr. Mishael Maswari-Caspi alivyoandika katika
Pili: Maandiko ya Kiyahudi ya Midrashic huelezea siku ya 10 ya mwezi wa 7 (Yom Hakippurim – Siku ya Upatanisho) kwenye tukio la kurudisha Mbao za Agano kutoka Mlima Sinai, kama Dr. Mishael Maswari-Caspi alivyoandika katika barua yake, iliyonukuliwa katika makala yangu ya nyuma iliyotajwa hapo juu.

Swali ni: Kama Mayahudi walitaka kuweka mawiano ya muda mrefu yaliyopotea ya Tishri na Muharram katika mazingatio, imekuaje kwamba wamesahau kuisimulia Hadithi hii kwa Mtume?

Tatu: Mwezi ambao Mungu aliwakomboa Mayahudi kutoka kwa Firauni ilikuwa ni Abib (yaani, Rajabu), kama Biblia inavyosema kwa uwazi: (Deut. 16: 1)

Swali ni: Inawezekanaje kwa Mayahudi kuhamisha tukio la Abib (kwa asili hufungana na mwezi wa Rajabu) kwenda Muharram, kwa kuiasi Taurati wazi wazi?

Na mwisho, hapa kuna nukta ya kutafakari kwa Waislamu: Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alitumwa pamoja na dini ili azifute dini zote na shari’ah zote zilizokuja nyuma yake. Ni vipi kwamba anaridhia au kujidhili kuiga desturi na mila za Mayahudi?

Ni wazi kutokana na ukweli uliotajwa hapo juu, kwamba Mayahudi walikuwa hawana sababu yoyote ya kufunga katika siku ya Ashura ya Muharram katika wakati huo; na kisa hiki, kilichojengwa juu ya kigezo hicho, ni habari za kubuni tu. Kwa hakika zilibuniwa na msimuliaji (wa Hadithi) ambaye alijua tu kwamba hapo zamani za kale Muharram ilifungana na mwezi wa Tishri I; lakini alikuwa haelewi kabisa dini ya Wayahudi ya wakati ule ule na utamaduni.

Mtu hujiona amelazimika hapa kutaja kwamba Hadithi hii na nyingine kama hii zilibuniwa na kambi ya wafuasi wa Bani Umayyah, baada ya muhanga wa Imamu Huseini (a.s.), kama sehemu ya kampeini yao ya kuigeuza siku ya Ashura, mwezi 10 Muharram kuwa siku ya kusheherekea.

Hadithi hizi ni za aina moja kama zile zinzosema kwamba mwezi 10 Muharram Safina ya Nuh ilisimama juu ya Mlima wa Arafat, moto ulikuwa baridi na salama juu ya Ibrahim, na Isa (Yesu) alipaa kwenda mbinguni.

Katika kundi hilo hilo zimekuja Hadithi zenye kuwahimiza Waisalmu kuifanya Ashura siku ya shangwe ya siku kuu, na mtu kuweka hakiba ya nafaka (chakula) mahususi kwa ajili ya siku hii kwa vile itaongeza riziki ya mtu na kuleta baraka za Allah kwa watu wa kaya (familia).

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

The Pilgrim Log

Helping you live your daily pilgrimage

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: