Blog Archives

Sheikh Hemedi Jalala: Akabidhi Nahjul Balagha kwa Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba

Dodoma, Tanzania

04/09/2014

Wiki hii kiongozi wa harakati ya Kiislamu chini ya Hawza Imam swadiq Samahati Sheikh Hemedi Jalala akiandamana na Naibu wake Sheikh Mohammed Abdu walifanya ziara katika Majenge ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma na Kuonana na Spika wa Bunge maalumu la Katiba Mheshimiwa Samuel Sitta.

Katika hafla hiyo Samahati sheikh Hemedi Jalala alipata fursa ya kutembelea ofisi za Kiongozi huyo mkuu wa bunge na kumkabidhi vitabu 600 zawadi kwa wabunge wa bunge hilo. Aidha Sheikh Jalala alimfahamisha spika wa bunge kuwa maudhumuni makuu ya kugawa Kitabu hicho cha Nahjul balagha kwa wabunge ni kuwawezesha wabunge kufahamu Maagizo na Miongozo ya Imam Ali (as) kama Kiongozi Muadilifu kabisa wa dola ya Kiislamu aliyewahi kutokea baada ya Mtume (saw) na ndani ya kitabu hicho wabunge watapata mbinu kutokana na miongozo ya Imam Ali (as) kutokana na kauli zake tukufu zilizolenga malengo makuu ya Utawala wowote ikiwa ni pamoja  na kulinda maadili ya jamii, Heshima, Utu, Usawa na Haki kwa kila kiumbe. Vitabu vyote hivyo vilipokelewa na Spika kwa niaba ya wabunge wote.

Kitabu cha Nahjul Balagha ni mkusanyiko wa Semi (Maneno) matukufu ya Imam Ali (Kiongozi wa Kwanza baada ya kufariki Mtume (saw) ndani ya kitabu hicho kimekusanya hotuba zake, na Barua zake alizoziandika kwa viongozi mbalimbali wa dola yake na hata kwa viongozi waliokuwa wakipinga dola yake. Ndani ya kitabu hicho kuna moja ya barua Maarufu ambayo inatoa misingi ya uongozi bora na Maadili kwa kila mtawala barua namba 53 ya Imam Ali wakati alipomteua Malik al-Ashtar an-Nakha’i kuwa Gavana wa Misri na Maeneo yanayoizunguka.

DSC00247 - Copy

Sheikh Hemed jalala, akimkabidhi mh spika wa bunge maalum la katiba Mh: Samweli Sita kitabu cha NAHJUL BALAGHA ofisini kwake mjini Dodoma jana. katikati ni mjumbe wa bunge hilo, Mh. Yasmini Aluu.

DSC_0034

Sheikh Hemed jalala, akimkabidhi mh spika wa bunge maalum la katiba Mh: Samweli Sita kitabu cha NAHJUL BALAGHA ofisini kwake mjini Dodoma jana. katikati ni mjumbe wa bunge hilo, Mh. Yasmini Aluu.

DSC_0035

Sheikh Hemed jalala, akimkabidhi mh spika wa bunge maalum la katiba Mh: Samweli Sita kitabu cha NAHJUL BALAGHA ofisini kwake mjini Dodoma jana. katikati ni mjumbe wa bunge hilo, Mh. Yasmini Aluu.

DSC_0046

Spika wa Bunge maalum la katiba Mh Samweli Sita, akiwakaribisha viongozi wa Taasisi ya kiislaam ya Imam swadiq, waliofika kumtembelea ofisini kwake mjini Dodoma na kukabidhi zawadi ya vitabu 600 vya kilele cha ufasaha (Nahjul balagha) kwa ajili ya wabunge. Kulia kwake ni mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Hemedi jalala na mjumbe wa Bunge Maalum Mh Yasmini Aluu

DSC_0061

Samahati Sheikh Hemed Jalala , akifafanua jambo kwa spika wa Bunge maalum la katiba, walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma jana, nakumkabidhi vitabu 600 zawadi kwa wabunge wa bunge hilo. vitabu ni mahsusi kwa ajili ya kulinda maadili katika jamii.

DSC00212 - Copy - Copy

Msafara wa samahati sheikh Hemedi Jalala wakikaribishwa Bungeni jana 03/092014

DSC00240 - Copy

Samahati Sheikh Hemedi Jalala alipokuwa akiitambulisha Nahjul Balagha, Maudhui yake, Umuhimu wake Kwa viongozi na Hasa watawala wa nchi.

DSC00271 - Copy - Copy

Mh Samweli Sita, Akiwatembeza Masheikh katika viwanja vya Bunge

DSC00279 - Copy

Picha ya Pamoja kati ya nMheshimiwa Spika wa Bunge Samweli Sita na Jopo lililoongozana na Sheikh Hemedi jalala mble ya ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

DSC00304 - Copy (2)

DSC00290 - Copy

Elijah J. Magnier

Middle East Politics

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

Pilgrim Center of Hope

Catholic Evangelization Ministry

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: