Blog Archives

KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI: SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MSIBA WA WANAFUNZI ARUSHA

Maulana Sheikh Hemedi Jalala kiongozi mkuu Hawza Imam swadiq ametoa salamu za kufuatia msiba wa wanafunzi 30 uliotokea huko Arusha na kusema :

“Hakika Sisi sote ni wa Mungu na mwisho sote tutarudi kwake, Tumepokea kwa masikitiko makubwa na kwa huzuni ya hali ya juu isiyokua na kifani ajali ya basi la shule ya lucky visent ya mjini Arusha, iliyotokea katika eneo la mlima rotia karatu na kusababisha vifo vya wanafunzi wasio pungua 30 pamoja na walimu.

Mauna Sheikh Hemedi Jalala ametoa salamu za pole kufuatia msiba wa wanafunzi wa Lucky Viscent

Sisi kama watumishi wa Imam Swadiq ambao makao yetu makuu yapo hapa Kigogo Dar es Salaam, kama Waislamu na wafuasi wa madhehebu ya Shia (Ithna Asharriya) Tanzania tunaungana na watanzania wenzetu wote, Waislamu, wakristo na wasiokua waislamu na wakristo wanaoishi Tanzania kutoa mkono wa pole kwa wazazi wa wanafunzi wote, uongozi mzima wa shule ya Lucky Vicent na kwa wanafunzi wenzao ambao bado wapo shuleni hapo. Vilevile tunatoa mkono wa pole kwa Taifa letu takatifu kwa ujumla na kwa Mh Raisi wa taifa letu, napenda kusema hili limetugusa kama waumini na kama watanzania.
Tunaposoma Quraan amabayo ndio Kitabu chetu inatuambia ya kuwa waumini wote ni ndugu, hivyo lililotokea limewakumba waumini wenzetu. Ni wajibu wetu kama watanzania pasina kubaguana kidini wala kimadhehebu kupendana, kuhurumiana wakati wote, iwe ni wakati wa raha au wa majanga kama hili ambalo limetukumbu katika kipindi hiki. Mtume Muhammad (s.a.w.w) anasema hakika waumini wanasifa ya kuhurumiana kama vile unavyoona mwili mmoja, kiungo kimoja kinapougua viungo vingine navyo vinakesha.

Mungu awape wafiwa Subira na uvumilivu na wote waliotangulia Mungu aziweke roho zao mahala pema na sisi tuliobaki Tanzania atupe upendo, mshikamno, umoja, kuvumiliana, kuenzi Amani na utulivu tuliokua nao. Mungu ibariki Tanzania, watu wake wote na viongozi wote. Aami Aamin”

MAULANA SHEIKH JALALA ATEMBELEA SHULE ILIYOKUMBWA NA AJALI YA MOTO

MAULANA SHEIKH HEMEDI JALALA ATEMBELEA “DAR ES SALAAM ISLAMIC SECONDARY SCHOOL” AMBAYO ILIKUMBWA NA AJALI YA MOTO ILI KUTOA SALAMU ZA POLE.
Maulana Samahat Sheikh Hemedi Jalala akiongozana na jopo la walimu na masheikh kutoka chuo cha theolojia ya dini ya kiislamu, Hawza Imam Swadiq (a.s) ametembelea na kutoa salamu za pole kwa uongozi wa shule ya kiislamu ya DAR ES SALAAM ISLAMIC SECONDARY SCHOOL ambayo hivi karibuni ilikumbwa na ajali mbaya ya moto iliyoteketeza madarasa, mabweni, mali na samani za shule hiyo, hali ambayo imepelekea kusimamishwa masomo ya mamia ya wanafunzi wa shule hiyo.
Maulana Sheikh Hemedi Jalala alipowasili Masjid Taqwa alipokelewa na uongozi na kukaribishwa na Sheikh Ponda Issa Ponda ambae ni kiongozi na mwenyekiti wa Islamic Development Foundation (IDF), Taasisi inayoendesha na kusimimia shule hizo.
Maulana Samahat Sheikh Hemedi Jalala akiongea na mwenyekiti wa IDF ofisini kwake mapema leo, amesema:DSC_0424

“Tukio hili limetugusa, uwepo wetu hapa ni dalili ya hilo. Tumepata taarifa kupitia vyombo vya habari juu ya tukio lililotokea tukaona ni lazima tufike kutoa pole na kuwaunga mkono ndugu zetu kwani itikadi yetu na Imani yetu ni kwamba yule ambae hatilii umuhimu maswala ya waislamu basi si miongoni mwa waislam”

Maulana pamoja na jopo lake walikabidhi mchango wao ili kusaidia kurekebisha shule hiyo kwa malengo ya kusaidia wanafunzi kuendelea na masomo mapema iwezekenavyo.

photo_2016-05-21_14-58-43
Maulana Sheikh Jalala akiwa na wenyeji alitembelea eneo lililoathirika na ajali na kujionea uharibifu mkubwa uliosababishwa na moto huo, uongozi wa shule kupitia katibu wake umeashiria upungufu wa vitabu, magodoro ya kulalia na vifaa vingine vinavyohusiana na uendeshaji wa shule na kutoa wito kwa wahisani kuchangia thamani au vifaa husika ili kurudisha shule katika hali yake.

AsadiqMedia.
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Hawza Imam Swadiq (a.s).
B.p: asadiqmedia@gmail.com
Tovuti: imamswadiq.com/

MAULANA SHEIKH HEMED JALALA AFANYA MKUTANO NA WANAHABARI

 

KUMBUKUMBU YA MWAKA MPYA WA KIISLAM

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufikia mwaka 1437, baadhi yetu tukiwa wazima, pia Mwenyezi Mungu awape afya wale wenye maradhi na awatie nguvu wale wanyonge.

Usiku wa leo ni tarehe 1 muharram 1437, sawa na tarehe 15 Oktoba 2015. Lakini siku ya leo, watanzania wanaadhimisha siku aliyofariki baba wa taifa hili Mwl. J.K Nyerere (14/Oktoba). Tunatoa mkono wa pole kwa familia ya Mwl. Nyerere, kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watanzania wote. Baba wa taifa anakumbukwa kwa mambo mengi katika historia ya nchi yetu.

  1. Kama waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika
  2. Kama rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  3. Kama miongoni mwa viongozi walioongoza mapambano ya kumuondoa mkoloni Tanzania na afrika kwa ujumla.

Tunafanya haya kwakurejea maneno ya Imam Ali (a.s) katika nahjul balagha, maneno yaliyonukuliwa na aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Koffi Annan (1997-2006) kuwa “ watu ni aina mbili, aidha  ni ndugu yako katika dini au ni ndugu yako katika damu (nasabu). Kwahiyo tunakila sababu ya kutoa mkono wa pole kwa watanzania.

Pili, leo katika historia baada ya maghrib, waislam kwa kuzingatia kalenda ya mwezi (lunar calender) tunaukaribisha mwaka mpya wa kiislam (1437 .H).

Maulana Sheikh Hemed jalala akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwaka mpya na Ashuraa

Maulana Sheikh Hemed jalala akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwaka mpya na Ashuraa

Katika kuukaribisha, hatuna budi kufahamu pia kuwa mwaka uliopita (1436 H) ulimwengu wa kiislam ulikumbana na changamoto nyingi. Kuna haja ya kujifunza kutokana na changamoto hizo. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na maafa ya mahujaji ambapo maelfu ya mahujaji wamepoteza uhai wao, hatutosita kuzitaka mamlaka husika kuwajibika kwa hilo.

Pili, vita nchini Syria na Yemen ambazo msingi wake mkuu ni kukithiri kwa ubepari /ubeberu ulimwenguni na kuibuka kwa makundi ya kukufurishana (takfiir groups).

Tatu, kumomonyoka kwa maadili miongoni mwa wanajamii hasa baada ya kutangazwa kwa uhalali wa ndoa za jinsia moja kwa nchi za magharibi, hivyo kuathirika kimaadili na kiuchumi kwa nchi nyingi tegemezi.

Tatu, kushuka kwa bei ya nishati ya mafuta duniani ambayo kwa kiasi kikubwa nchi nyingi zilizoathirika ni za ukanda wa ASIA ambazo zinaidadi kubwa ya waislam.Nne, ni kukithiri kwa mauaji ya watu wenye albinism, hali iliyopelekea wajihisi kuwa ni raia wa daraja la tatu nchini Tanzania.

Tano, kuchomwa kwa baadhi ya nyumba za ibada na kudhuriwa kwa baadhi ya viongozi wa dini nchini Tanzania.

Mwisho, leo (usiku, 15/10/2015 sawa na 1 Muharram 1437) katika ulimwengu wa kiislam, waislam na wapenda haki wote duniani tunakumbuka matukio ya kuuwawa kikatili mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), DSC06032Imam HUSSEIN (a.s). Kwa ufupi, Imam Hussein  ni kiongozi aliyeonesha dira ya namna ya kupambana  na DHULMA ulimwenguni kama Mahatma Gandhi (Baba wa Taifa la India) na Rabindranath Tagore (Indian Nobel Prize in Literature 1913), Thomas Carlyle (Scottish historian and essayist) , Charles Dickens (English novelist) Edward G. Brown (Professor at the University of Cambridge walivyomulezea Imam Hussein katika maandishi mbalimbali wakihusianisha mafanikio ya harakati nyingi za kudai haki na Imam Hussein (A.S).

Kwa huzuni kabisa, tunatoa mkono wa pole kwa Mtume (s.a.w.w) na familia yake (Ahlulbayt), pia kwa waislam wote ulimwenguni na wapenda haki pasina kujali imani zao.

Imam Hussein ni kielelezo cha utu, uadilifu, na amani. Pia ni ishara ya ukombozi wa viumbe na ni kielelezo cha kupinga dhulma ulimwenguni.

Kaulimbiu ya mwaka huu:

IMAM HUSSEIN (A.S) NI DARASA JUU YA UHURU WA BINAADAMU NA UPINGAJI WA DHULMA.

IMETOLEWA NA SHEIKH HEMED JALALA

 KWA MAELEZO:

Kitengo cha habari na mawasiliano

Assadiq Media

Email: asadiqmedia@gmail.com

https://imamswadiq.com

elbinawi

To interact with humanity & share ideas...

felicity114

felicity is the purpose of everybody

Ladakh Express

Ladakh's 1st political and cultural online journal.

Islamic Library

Shia Islamic PDFs - Now in Collaboration with ShiaTranslate.org!

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

mmubaraka1

A fine WordPress.com site

The Pilgrim Log

Helping you live your daily pilgrimage

World Shia Forum

Identity, Equality, Unity

Source of Inspiration

All is One, co-creating with the Creator

Bill Langill's Blog

Love is the Answer

Interrupting the Silence

An Episcopal Priest's Sermons, Prayers, and Reflections on Life, Becoming Human, and Discovering Our Divinity

Morgan L. Busse

In Darkness there is Light

YOGA

When unconscious became conscious this is Samadhi

Zoroastrians.net

Parsis, Iranis, Zarathushtis, All Under One Roof

Islamic Laws

Raising Awareness on Fiqh and the Ulema

Tech Cloud

Imagine | Innovate | Implement

Mujtaba Somji

Islamic sayings

%d bloggers like this: